Adverts

Apr 25, 2011

UKARABATI WA IFUNDA WAFANYWA NA WALIOSOMA SHULE HIYO

Ujumbe wa watu waliosoma Shule ya sekondari ya ufundi Ifunda, wiki iliyopita walipiga kambi katika shule ya mazingira ya shule ya sekondari ya Ifunda iliyopo mkoani Iringa kwa lengo la kuchangia ukarabati wa shule yao ya zamani.
Zaidi ya watu watano walioongoza ujumbe huo ambapo kazi mbalimbali zilifanyika ikiwemo kukarabati jengo la utawala na jengo lililokuwa likitumika kama karakana ya fani ya umeme.
Timu hiyo iliongozwa na Huruma Mahenge mmoja wa wahitimu wa miaka ya tisini ambapo wahitimu mbalimbali waliweza kuchangia ujenzi huo na kufanikisha kubadili sura ya shule hiyo ambayo imetoa baadhi ya wataalamu walioajiriwa na kufanya kazi kwenye viwanda mbalimbali duniani vikiwemo viwanda vikubwa nchini Japan.
Miongoni mwa walioko nje na wanafanya kazi katika viwanda vikubwa ni panmoja na Christopher Ntyangiri anayefanya kazi katika moja ya viwanda vya japan vya masuala ya elctronikia ambaye alimaliza Ifunda mwaka 1994, Ismail Mwilenga anayefanya kazi katika moja ya viwanda vya mitambo ya kupozea viwandani na majumbani nchini Afrika kusini.
Aidha wapo walioanzisha makampuni yanayochukua heshima duniani kutokana na utendaji wake nchini Ujerumani, Uingereza na Marekani.
Aidha wapo wapiganaji na wataalamu wa kijeshi ndani na  nje ya nchi wanaoendelea kuwakilisha vyema taifa letu kutokana na ujuzi wa kiufundi waliopata katika shule hiyo wakiwemo marubani, wataalamu wa mizinga na medani nyingine za kivita.
Aidha Ifunda ni miongoni mwa shule zilizotoa mafundi ambao sasa ni wahandisi katika idara mbalimbali za serikali na hasa katika halmasahauri za wilaya nchini, makampuni binafsi na ya kimataifa ambapo miongoni mwao wanasimamia miradi mikubwa inayohusisha nchi na nchi .
zifuatazo ni sehemu ya picha ya kazi iliyofanywa na wahitimu hao wiki iliyopita...




Jengo hili litakumbukwa sana kwakuwa hapa ndipo ilipokuwa assembly , kila mtu ana la kusimulia kuhusiana na mahala hapa!!!!!!!!!! bado michango inaendelea kukusanywa kupitia kwa dada Huruma Mahenge, ingia kwenye face book bofya