Adverts

May 21, 2011

BREAKING NYUUUZ: MAUAJI MENGINE YATOKEA MBOZI

Hiki ndicho kituo cha mabasi alipochukulia kipigo cha hadi kufa kijana ajulikanaye kama Kefa mkazi wa Vwawa wilayani Mbozi

Na Mwandishi wa Indaba Africa blog.

Taarifa zilizotufikia hivi punde zinaeleza kuwa kijana mmoja anayejulikana kwa jina la Kefa ameuwawa mjini Vwawa katika wilaya ya Mbozi kutokana na kutuhumiwa kufanya uhalifu na kuwa kero katika jamii.
Licha ya polisi kufanya jitihda za kumwokoa kutoka kwa wananchi wenye jazba waliokuwa wameshamwagia mafuta ili wamuunguze, tayari kutokana na kupondo alichopewa na wananchi hao kilikuwa kimemfikisha hatua ya kuanza kuona mauti.
Habari zaidi zinaeleza kuwa licha ya kukimbizwa hospitali ya wilaya ya Mbozi Kefa alishindwa kurejesha pumzi na hatimaye kukata roho.
Hata hivyo taarifa zaidi zinaonyesha kuwa kijana huyo mwanzoni mwa mwaka huu katika mazingira yasiyoeleweka alijichongea sanduku lake la kuzikiwa na kutangaza wazi kuwa anahisi kuwa asingemaliza mwaka 2011.
Inaelezwa na baadhi ya vijana wanaoshinda stendi ya eneo la Makaburini kuwa wakati mwingine kijana huyo amekuwa akilala kwenye sanduku lake hilo na asubuhi kuendelea na shughuli zake za kupiga debe stendi.
Atakumbukwa kwa uendeshaji wa pikipiki kwa kasi, huku piki piki yake hiyo ikiwa imepigwa marufuku kutotumika tena kutokana na ubovu wake, ambao ulikuwa pia ukisababisha kuwa na mlio wenye kelele na hivyo kuwa kero kwa wananchi wa mji huo.
yatakayojiri mtaarifiwa kupitia www.dtwevetz.blogspot.com