Hili ndilo bwawa la kuogelea lililojengwa enzi hizo ikiwa shule ya Malkia, lakini sasa lina kidimbwi kidogo cha kufugia Vyura wanaojifunza kuogelea!!!!
|
Haya basi nyie mliosoma Iyunga mmefanya nini kuhakikisha mazingira ya shule hii yanaanza kurejea kama enzi zenu? Wenzenu wa Ifunda wameshafanya vitu pale Ifunda, kuna ukarabati unaendelea kupitia alumin yao ya waliomaliza IFUNDA huko nyuma!. |
|
Mkuu wa shule ya sekondari ya Iyunga, yeye bila shaka ukimuuliza atakwambia Capitation haitoshi, sijui hakuna fedha za kutosha kufanya hivi na vile, lakini una jumuiya ya wasomi waliotokea shule ya Iyunga hapo umewaaalika wachangie? bila shaka bado, basi changamka sasa hili bwawa lianze kutumika! |
nakwambia ni shule chache zenye maisha ya ulaya ulaya kama hivi lakini sasa imekuwa sehemu ya kutupia masalia ya ugali na vigunzi vya mahindi mweeee!!!!!