Adverts

Sep 19, 2011

CHADEMA Wawapokea Kwa Shangwe Wabunge Wao Walioswekwa Rumande

CHADEMA Wawapokea Kwa Shangwe Wabunge Wao Walioswekwa Rumande:
Wanachama wa CHADEMA mjini Igunga, jioni hii walijawa na furaha kubwa wakati wakiwa wanawapokea wabunge wao waliokamatwa hivi karibuni na kuwekwa rumande mjini Igunga na baadae kuhamishiwa kituo cha polisi mkoani Tabora kwa kosa la kumsukasuka mkuu wa Wilaya ya Igunga Fatuma Kimario. Wabunge hao ni Sylivester Kasulumbai, mbunge wa Maswa Mashariki, Suzani Kiwanga, ambae ni mbunge wa viti maalumu. Mwingine ni kada wa chama hicho. Kwa pamoja wamepata dhamana na kesi yao itatajwa tarehe 12.10.2011. Pichani wakiwa katika maandamano jioni hii mjini Igunga. Picha na Victor Makinda. kutoka Mjengwa Blog