Adverts

Nov 26, 2011

CHUO CHA RIADHA KIKO TAYARI KUINUA MCHEZO HUO

Mwanariadha mkongwe aliyewahi kuipeperusha vyema bendera ya Tanzania kimataifa, Gidamis Shahanga (kulia) akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na kuanzishwa kwa Taasisi ya Michezo ya Gidamis Shahanga (SSI) yenye lengo la kuinua michezo, hususani riadha, jana kwenye hoteli ya Courtyard Protea, Upanga jijini Dar es Salaam. Kushoto ni mwanariadha wa zamani, John Haygahimo.
(Na Mpigapicha Wetu)