Adverts

Jul 30, 2012

WANAFUNZI WAANDAMANA KWENDA OFISI ZA MKUU WA WILAYA KUDAI HAKI YA KUFUNDISHWA

Mgomo wa walimu ulioanza leo, umeanza kuota matawi baada ya wanafunzi wa shule za msingi katika mji mdogo wa Vwawa na Tunduma katika wilaya ya Mbozi kuandamana huku kukiripotiwa kutokea uhalibifu wa mali katika mji wa Tunduma.
katika mji wa Vwawa wanafunzi wa shule ya msingi ya Ichenjezya waliandamana majira ya saa tatu hadi kwenye ofisi za mkuu wa wilaya mbozi wakitaka kuonana na mkuu huyo wa wilaya ili wapate haki yao ya kufundishwa aambayo wanadai wameikosa siku ya leo kwa mgomo wa walimu.

wakizungumza mbele ya mkuu wa kituo cha polisi cha Mbozi, wanafunzi hao wamesema hawaondoki mpaka waelezwe namna watakavyopata huduma ya kusomeshwa, hata hivyo baada ya mbinu za hapa na pale watoto hao walilainika na kuondoka kuelekea shuleni kwao ili yakazungumzwe huko.\

Mbinu ya polisi kwa kushirikiana na idara zingine za serikali iliwezesha watoto hao kutoka kwa staili ya mchaka mchaka na kurejea shuleni kwao, na dadkika chache baadaye kundi jingine la wanafunzi kutoka shule ya msingi ya Haloli lilitia timu mbele ya geti la halmashauri ya wilaya ya Mbozi kutaka kumwona afisa elimu.
Hapa napo ikawa kazi kutengeneza maneno ya kuwafurahisha, ambapo baada ya zuga zuga ya muda mrefu hatmaye watoto hao walilegea na kuondoka,
 MLINZI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA MBOZI AKIJARIBU KUWATULIZA WANAFUNZI HUKU AKIFUNGA LANGO KUU LA KUINGIA HALMASHAURI YA WILAYA MMBOZI
Huko Tunduma taarifa zinaaeleza kuwa uhalibifu wa mali na majengo ya serikali umetokea katika ofisi za mamlaka ya mji wa Tunduma ambapo gari jipya limevunjwa vioo na vifaa kama kompyuta na laptops vimeibiwa katika ofisi za mamlaka hiyo