Na Danny Tweve
Dodoma
MAHUSIANO MABAYA BAINA
YA MADIWANI NA WATENDAJI KATIKA HALMASHAURI NYINGI ZA WILAYA NCHINI NI SEHEMU
YA MATOKEO YA MFUMO WA UGATUAJI MADARAKA AMBAPO UMEFANYIKA PASIPO KUBAINI
MAPENGO YA UELEWA KATIKA MAKUNDI HAYO MAWILI IMEBAINISHWA.
HAYO NI SEHEMU YA
MATOKEO YA UTAFITI WA MAHITAJI YA MAFUNZO ULIOFANYWA NA CHUO CHA
MIPANGO DODOMA KWA HALMASHAURI ZA WILAYA
NCHINI, NA KWAMBA KUTOKANA NA CHANGAMOTO HIYO, CHUO KIMEANDAA MTAALA UNAOLENGA
KUJENGA UWEZO KWA VIONGOZI WA VIJIJI, KATA NA HATIMAYE WILAYANI
ILI KUWEZESHA UTENDAJI USIO NA MIGOGORO
WAKIZUNGUMZA KWA
NYAKATI TOFAUTI MAKAMU MKUU WA CHUO HICHO SEHEMU YA RASLIMALI WATU NA UTAWALA
BW. TIBELIO MDENDEMI NA MKUU WA CHUO HICHO BWANA CONSTANTINO LIFURILO ,
WAMESEMA SAMBAMBA NA MAFUNZO HAYO, PIA CHUO KINAENDELEA NA UANDAAJI WA TAARIFA
ZA USURI WA HALI ZA KIJAMII NA KIUCHUMI ZA WILAYA ZA MKOA WA MOROGORO BAADA YA
KUKAMILISHA WILAYA ZOTE ZA MKOA WA DODOMA
CHINI YA MPANGO HUO,
HALMASHAURI ZA WILAYA NCHINI KAMA ENEO MUHIMU LA UGATUAJI WA MADARAKA KATIKA SERIKALI ZA MITAA LIMEWEKEWA MKAZO KATIKA
MAFUNZO HAYO YATAKAYOHUSISHA VIONGOZI
WA KUCHAGULIWA NA WATENDAJI WAAJIRIWA WA
HALMASHAUR AMBAPO WILAYA YA MBULU KATIKA
MKOA WA MANYARA IMETENGWA KAMA ENEO LA MAJARIBIO NA MPANGO HUO UTATEKELEZWA KWA USHIRIKIANO BAINA YA CHUO CHA MIPANGO DODOMA NA NA SERIKALI YA UHOLANZI
DANNY TWEVE DODOMA