Mbozi
Kupanda ovyo kwa gharama za mafuta kumetajwa kuwa na athari
za kiwango cha juu katika uendeshaji wa kilimo cha kisasa na hasa matumizi ya
zana kama trekta na vikokotozi maarufu kama powertillerkwenye wilaya maarufu
kwa kilimo cha mahindi imefahamika.
Katika taarifa ya utafiti
aliyoiwasilisha Chuo cha Mipango Dodoma kwaaajili ya kuhitimu stashahada ya uzamili katika mipango ya
Mikoa, mtafiti Danny Tweve ameeeleza kuwa, katika sampuli ya watu 103 walioshiiriki kwenye
utafiti huo ni watu 4 tu waliokiri
kutumia teknolojia ya kisasa katika kulima mashamba yao.
Asilimia 98 ya washiriki wa utafiti walikiri kutumia jembe
la mkono na wanyama kazi , na walipohojiwa sababu za kutotumia trekta ama
powertiller kwa sehemu kubwa sababu zilizotolewa zilielekezwa kwenye gharama za
mafuta kutovutia watu kuendelea kutumia teknolojia hiyo licha ya kutambua
ukweli kwamba hurahisisha kazi.
Ingawa katika miaka ya 80 wilaya ya mbozi iliweza kupandisha
idadi ya watumiaji wa teknolojia ya trekta kupitia mipango ya vijiji vya
Ujamaa, gharama za mafuta, ukosefu wa vipuli na gharama za bidhaa hizo
zilirejesha nyuma mwitikio wa wananchi hatua ambayo wengi wa wakulima walihamia
kwenye matumizi ya jembe la mkono na wanyama kazi.
Utafiti huo uliofanywa katika vijiji vya Ivwanga na Mbimba
unaonyesha kuwa kutokana na hali hiyo wananchi wengi wanapenda kubadili kilimo
chao kutoka kile cha jembe la mkono kwenda kilimo cha kutumia zana za kisasa,
hata hivyo suala la bei ya mafuta linaendelea kuwa kikwazo kwakuwa Dar es
salaam ambako hawalimi ndiko mafuta yanakouzwa kwa bei ya chini ikilinganishwa
na mikoani ambako mahitaji kwa shughuli za kilimo ni makubwa zaidi.
Bei ya Diesel katika wilaya ya Mbozi kwa wakati ambapo
utafiti huo ulikuwa unafanywa ilikuwa ni shilingi 2300 ilihali mafuta hay ohayo
jijini Dar es salaam ilikuwa 2005
kiwango ambacho kinathibitisha kuwa serikali haijaweka nia ya dhati
kumsaidia mkulima kuondoknaana kilimo cha jembe la mkono.
Kutokana na gharama
kubwa za vilainishi, trekta bado limeendelea kuwa zana ya usafirishaji zaidi
kuliko kutumiwa kama zana ya uzalishaji shambani ambapo idadi ya matrekta 79
yaliyopo wilayani humo kwa sehemu kubwa yanatumiwa kwaajili ya kusafirisha
mizigo na kubebea mazao baada ya kuvuna, huku wamiliki wakillalamikia kukosa
watu wa kukodisha hasa wananchi wa kawaida.
“ili uwe na uhakika na kurejesha mkopo wa trekta, ni lazima
kwanza uwe na eneo la kutosha kwaaajili ya kujilimia mwenyewe na kuzalisha mahindi
mwenyewe kwani ukitegemea kukodishwa kwa wananchi hawa wa kawaida itakula kwako”
anaeleza mmoja wa wamiliki wa zana hizo bwana Mwazembe.
Aidha ufuatiliaji mdogo miongoni mwa makampuni yanayosambaza
mbegu za mahindi umetajwa kuchangia kupunguza mwitikio wa wananchi katika
kutumia mbegu za kisasa . Inaelezwa kuwa huduma za ugani kwa makampuni hayo na
hasa ushauri umekuwa ukisitishwa mara tu wanapofanikiwa kutangaza mbegu wanazozizalisha na kutoweka.
Hatua hiyo inapoteza dhana ya mwendelezo kwa mkulima hasa
pale anapokumbana na changamoto mpya kutokana na matumizi ya mbegu husika,
hivyo kupendekeza kuwepo kwa mfumo wa uratibu wa makampuni yanayosambaza mbegu
kwa wakulima kama njia ya kuyafanya
yawajibike kwa bidhaa yanazozisambaza hii ikiwa ni pamoja na dawa za kuulia wadudu na uhifadhi wa nafaka.
Changamoto zingine zilizobainishwa kwenye utafiti huo ni
pamoja na ongezeko la malalamiko ya
usambazaji wa bidhaa feki msimu hadi msimu ambapo mbegu za mahindi, Mbolea na
dawa za kuulia wadudu vimekuwa vikiwaingiza hasara wananchi kutokana na
usimamizi mbovu wa soko la bidhaa hizo katika mikoa iliyopo mipakani.
Baadhi ya mbinu ambazo zimebainishwa na wananchi kwa upande
wa mbegu za mahindi ni pamoja na wafanyabiashara kuchanganya mahindi
yaliyohifadhiwa kwenye magunia na kuyaweka rangi zinazofanana na mbegu
zinazopendwa na wakulima na hatimaye kuchapisha mifuko katika nchi jirani
ambayo hutumia kusambaza mbegu hizo zikiwa na sura halisi ya mbegu
zinazozalishwa na makampuni ya ndani
Kwa upande wa Mbolea imedaiwa kuwa wafanyabiashara wamekuwa
wakichanganya na chokaa, chumvi na majivu ili kupata mifuko mitatu ya mbolea
kutoka katika mfuko mmoja halali, wakati ambapo kwa upande wa dawa za kuulia
wadudu, majivu, unga wa mahindi na rangi vimekuwa vikitumika kuwahadaa
wakulima.
sehemu ya matokeo ya utafiti huo yamo kwenye taarifa ya utafiti "adoption of improved maize technologies among farmers in Ivwanga and Mbimba Villages in Mbozi District.