Adverts

Oct 12, 2011

ELIMISHA MBEYA (NGO) YATOA MAFUNZO YA UIBUAJI WA MIRADI KWA MASHIRIKA YA KIRAIA







Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya uibuaji wa miradi na uendeshaji wa asasi ya ELIMISHA Mbeya wakimsikiliza mwezeshaji> mafunzo hayo ni sehemu ya ufadhiri wa Foundation for Civil Society kujenga uwezo kwa asasi za kiraia ambapo Elimisha ni miongoni mwa asasi zilizonufaika mkoani Mbeya
Mshiriki wa mafunzo ya uongozi na utawala wa asasi ya ELIMISHA Mbeya Bi. Kissa Mwalukindi akiwasilisha kazi za vikundi
Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya uibuaji wa miradi na uendeshaji wa asasi wakiwa makini kumsikiliza mwezeshaji

Picha ya pamoja ya washiriki wa mafunzo ya uibuaji wa miradi> mafunzo hayo yamefadhiriwa na Foundation for Civil Society

UGOMVI WA MTOA HUDUMA NA MTEJA MJINI VWAWA

Vijana ambao hawakuweza kujulikana majina yao ambao mmoja wao ni mhudumu katika hoteli ya Moshi Tea room iliyopo Vwawa wilayani Mbozi na mteja wake wakianza kuzichapa kavukavu kisa sh 500 wanaodaiana
Sasa wamekamatana na kutwangana makonde
Jamaa almaarufu kama Mwampashe na mteja mwingine akijaribu kuwaamulia na inashindikana
Pambano linaendelea mhudumu mwingine akatupa chini koti lake na kuja kuchangia
Jamaa washatumbukizana kwenye mtaro Mweampashe hoi hawezi kuamlia tena anaangalia tu
Ugomvi hauishi nimeamua kuendelea na safari yangu

MSAKA WA WAPIGA NONDO IRINGA MJINI USIKU HUU ZAIDI YA WATANO WANASWA

Kijana mpiga nondo akionyesha juu vitendea kazi baada ya kukamatwa ndani ya chuo cha kanisa la Anglicana Kigamboni Iringa


Baba mzazi wa kijana huyo juu akiwa chini ya ulinzi wa polisi jamii


Vijana wapiga nondo wakiwa chini ya ulinzi mkali wakati wa msako ulioanza majira ya saa 2 hadi asubuhi eneo la Muungano, Kigamboni ,Frelimo n.k


Vibaka watano wanaodaiwa kuhusika na upigaji nondo wakiwa chini ya ulinzi wa sungusungu



Fedha ambazo wapiganondo hao wamesalimisha baada ya kujeruhi watu wawili majira ya saa 2 eneo Mawele wele mjini Iringa wakati msako ukiendelea

Msako mkali ukifanywa na wananchi wa kata ya Mwangata na Mkwawa leo huku mwanamke mmoja pekee akijitolea kushiriki msako huo



Sakata la wananchi kupigwa nondo katika kata ya Mkwawa na Mwangata Manispaa ya Iringa limeendelea kuchukuasura mpya baada ya wananchi wa kata hizo wakiongozwa na sungusungu na polisi kufanya msako mkali nyumba kwa nyumba na kufanikiwa kuwakamata washiriki wa mtandao huo zaidi ya wanne pamoja na mali mbali mbali ambazo wananchi walipokonywa.



Pamoja na msako huo kufanyika katika nyumba za wananchi hao pia mmoja kati ya vibaka amekutwa ndani ya chuo cha kanisa la Anglikana eneo la Mawele wele akiwa amefichwa na mzazi wake.


Pia kijana mmoja kati ya waliokamatwa katika msako huo ni mtoto wa mchungaji wa kanisa moja la kilokole mjini Iringa ambaye amekamatwa maeneo ya Muungano .


katika msako huo vijana hao walikuwa wakipokea kipigo kikali kutoka kwa wananchi hao wenye hasira kali na baada ya hapo vijana hao wamekuwa wakitaja orodha ya matukio na idadi ya watu ambao wamewapiga nondo na kutaja pia kushiriki kumuua kijana Damas Kisinga .


Vibaka hao ambao majina yao tunayo japo kwa sasa yamewekwa kapuni kwaq muda ili kuendeleza msako zaidi wapo wanafunzi ,mtoto wa askari mstaafu wa jeshi , mtoto wa mchungaji wa kilokole na wote ni vijana kati ya miaka 20 hadi 35 na kuwa kila wanapopiga mtu nondo mali hukabidhi wa wakubwa wao na wapo hupata mgao wa kati ya shilingi 5000 hadi 20000 kwa makusanyo yanayozidi kiasi cha shilingi 200,000.


Wamedai kuwa baadhi yao wamekuwa wakilazimishwa na viongozi wao hao kushiriki katika vitendo hivyo ,ambapo viongozi hao wao wamekuwa wakitoa maelekezo ya watu wa kuwavamia na wale wa kupigwa nondo hadi kufa ama kukatwa mapanga.


Wamedai kuwa hadi sasa kuna orodha ya nyumba zaidi ya 50 katika manispaa ya Iringa ambazo zilikuwa katika mpango wao wa kwenda kuzivamia na kufanya uporaji .


Hata hivyo walidai kuwa walikuwa katika maandalizi ya kufanya uporaji mkubwa katika maeneo mbali mbali ya mji wa Iringa na kuwa mtandao wao kwa sasa ni mkubwa zaidi.


Pia alisema kuwa mtandao huo umeendelea kukua zaidi baada ya kukamatwa na kuachiwa na polisi na kuwa baadhi ya washiriki wa mtandao huo ni wale waliopata kutumikia vifungo jela na baadhi ya wamekuwa wakikamatwa na kuachiwa na polisi .


Wakati kipigo kikali kikiendelea kwa vibaka hao mmoja kati yao amesalimisha fedha kwa sungusungu hao kwa madai kuwa fedha hizo kiasi cha zaidi ya shilingi 20,000 kuwa walikuwa wametoka kupora usiku wa leo.

Wakati huo huo wananchi wamelitaka jeshi la polisi mkoani Iringa kutoa waachia mapema watuhumiwa hao wa upigaji nondo na kuhoji sababu ya mmoja kati ya watuhumiwa aliyekamatwa juzi ambaye ni mzazi wa Msafiri Ilomo kuachiwa huru kabla ya upelelezi wa suala hilo kukamilika .



Msaka huo bado unaendelea usiku huu na mimi nitaendelea kuwapa taarifa kulingana na matukio yatakavyo jitokeza

Mwinyi-Viongozi wa dini mnanuka



I
Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi, amesema viongozi wa dini kutoka Tanzania wanatia aibu na kuchangia Watanzania kunuka nje ya nchi kwa tuhuma za kusafirisha dawa za kulevya.

Mzee Mwinyi alitoa kauli hiyo jana mbele ya viongozi hao na kusimulia mkasa uliomkuta yeye binafsi wa kupekuliwa kupita kiasi katika kiwanja cha ndege nje ya nchi, akishukiwa kuwa kiongozi wa dini kutoka Tanzania anayesafirisha dawa za kulevya.

Alikuwa akizindua Baraza la Viongozi wa Dini la Kupambana na Athari za Dawa za Kulevya jana Dar es Salaam katika hafla iliyoandaliwa na asasi ya kiraia ya American International Health Alliance (AIHA).

“Ninachokisema kuna maneno mengi ya aibu yanasemwa kuhusu Watanzania, aibu zaidi hata kwa wacha Mungu wa Tanzania sasa hawaaminiki, wanatumia fursa walizonazo kuficha na kusafirisha dawa za kulevya.

“Nilikuwa naenda Ujerumani hivyo nililazimika kubadili ndege katika moja ya nchi huko ughaibuni, wakati wa kupanda ndege ya pili tukaanza kukaguliwa. Ilipofika zamu yangu, nilikaguliwa sana, lakini hawakutosheka, nikaingizwa kwenye chumba cha pembeni, nikavuliwa viatu na koti wakanikagua kwa mashine na mwisho wakanipapasa mwili mzima,” alisema Mzee Mwinyi.

Alisema alikumbana na kadhia hiyo pamoja na hadhi yake ya kidiplomasia kwa vile tu alikuwa ameshikilia tasbihi (rozari) mkononi, jambo lililofanya ahisiwe kuwa ni kiongozi wa dini anayesafirisha dawa za kulevya.

“Yule aliyenikagua alikuwa akifanya kazi yake, amenifundisha, lakini nataka mjue Watanzania wenzangu kuwa tunanuka huko nje,” alisema Mwinyi maarufu kama Mzee Ruksa wakati wa utawala wake.



Mzee Mwinyi alilazimika kutoa mkasa huo uliompata miaka mingi iliyopita bila kutaja mwaka wala uwanja husika mbele ya viongozi hao wa dini mbalimbali ili kufikisha ujumbe kwao kuwa Tanzania inanuka kwa kuhusishwa na dawa za kulevya.



Alisema mmoja wa wasaidizi wake alijaribu kumnusuru katika hali hiyo kwa kumtahadharisha ofisa wa uwanja huo wa ndege kuwa huyo anayemkagua ni mwanadiplomasia.



“Lakini bwana yule alimjibu tena kwa ukali ‘I don’t care’ (sijali), wakaendelea kunikagua wanavyotaka baadaye nikajiuliza kwani imekuaje wakanikagua vile, nikagundua kuwa ni kwa vile nimebeba tasbihi,” alisimulia Mzee Mwinyi.


Alisema alionekana kama mwanadini anayetumia alama ya tasbihi ili apitishe dawa za kulevya kirahisi, jambo ambalo lilimsikitisha na wakati anaondoka uwanjani hapo, alilazimika kumkabidhi yule ofisa aliyemkagua tasbihi yake kama zawadi.



Kauli hiyo ya Mzee Mwinyi, imetolewa baada ya Rais Jakaya Kikwete kuwataka viongozi wa dini kukemea uhalifu huo na kutahadharisha kuwa sasa biashara hiyo imeaanza kuvutia viongozi wa dini.



Rais Kikwete alitoa kauli hiyo alipokuwa akiwahutubia waumini wa Kanisa Katoliki Jimbo la Mbinga, kwenye ibada maalumu ya kupewa kuwekwa wakfu Mhashamu Askofu John Ndimbo wa Jimbo hilo.



Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi, alisema Serikali imejipanga kuhakikisha kunakuwa na sheria moja yenye nguvu itakayoziba mianya yote inayojitokeza katika sheria za dawa za kulevya.



Alisema kwa sasa sheria zilizopo zina mianya mikubwa ambayo inasababisha mapapa wa biashara hiyo na vipapa vidogo vinavyokamatwa kuishia kulipishwa faini ya Sh. milioni moja na kutoka.



“Sheria inasema wazi ukikamatwa na dawa za kulevya unalipishwa mara tatu ya gharama ya mzigo wa dawa hizo, kifungo cha miaka 30 au maisha lakini hivi kweli mmeshawaona watu wakifungwa kwa kosa hilo, lazima kuwe na marekebisho katika sheria hizi,” alisema



Kamishna wa Tume ya Kuratibu Udhibiti wa Dawa za Kulevya, Christopher Shekiondo, alisema kikosi kazi maalumu kilichopo chini ya Tume hiyo kimekamata watu wengi wanaotuhumiwa kufanya biashara hiyo.



Takwimu zinaonesha mwaka 2008 hadi mwaka huu, watuhumiwa 22,814 walikamatwa nchini na 67 nje ya nchi huku idadi ya dawa zilizokamatwa ikiongezeka.



Kwa mujibu wa Shekiondo, dawa zilizokamatwa zimeongezeka kutoka heroine kilo 100 kutoka mwaka 2000 hadi 2009 hadi kilo 154 mwaka jana na mwaka huu; na cocaine kilo 57 mwaka 2000 hadi 2009 hadi kufikia kilo 191 mwaka 2010 hadi mwaka huu.



Baraza hilo la Viongozi wa Dini kazi yake ni kuhamasisha vijana kuepuka biashara na matumizi ya dawa za kulevya na linaongozwa na Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Salum.




Oct 11, 2011

MALISA AZINDUA TAWI LA CCM JIPYA MKOANI ARUSHA

Kaimu mwenyekiti wa umoja wa vijana wa CCM taifa (UVCCM),Benno Malisa akifungua tawi la chama hicho eneo la Majengo juzi wakati wa ziara ya uzinduzi wa matawi ya chama hicho wilayani Arusha,pembeni yake kushoto ni mbunge wa viti maalumu kupitia umoja huo mkoani Arusha,Cathwrine Magige.
Kaimu mwenyekiti wa umoja wa vijana wa CCM (UVCCM) ngazi ya taifa,Benno Malisa akizungumza na wafuasi wa umoja huo nje ya jengo la makao makuu ya umoja huo mkoani Arusha juzi kabla ya ziara ya uzinduzi wa matawi mbalimbali ya chama hicho mjini hapa,pembeni yake ni mwenyekiti wa UVCCM mkoani Arusha,James Ole Milya
Mbunge wa viti maalumu kupitia UVCCM mkoani Arusha,Catherine Magige akiwapungia mkono wafuasi wa umoja huo nje ya jengo la makao makuu ya chama hicho mkoani Arusha wakati wa ziara ya uzinduzi wa matawi ya chama hicho wilayani Arusha,zaidi ya matawi 20 ya chama hicho yalifunguliwa katika sehemu mbalimbali.picha na Moses Mashalla -Arusha.

KUMBE BUNGE LILISHATUMIA MAJENGO YA FREEMASON

MABALOZI WATEMBELEA KABURI LA KARUME, NGORONGORO CRATER

Mabalozi wakiangalia meza ambayo ilivunjwa wakati akiuawa kwa risasi Rais wa kwanza wa Zanzibar, Hayati Abeid Amani Karume. (PICHA NA TAGIE MWAKAWAGO) Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, akiweka shada la maua kwenye kaburi la Rais wa kwanza wa Zanzibar, marehemu Abeid Amani Karume, eneo la Kisiwandui, Zanzibar. (PICHA NA TAGIE MWAKAWAGO) Kiongozi wa mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao nchini,Juma Mpango, akisoma dua kwenye kaburi la Rais wa kwanza wa Zanzibar, Hayati Abeid Amani Karume, mabalozi walipotembelea kaburi hilo mwanzoni mwa wiki.(PICHA NA TAGIE MWAKAWAGO) Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe (katikati waliokaa), akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao nchini, pamoja na mtoto wa hayati Karume, Balozi Ali Karume (kulia waliokaa). Picha hiyo walipiga katika lango la kaburi la Karume, mjini Zanzibar.(PICHA NA TAGIE MWAKAWAGO) Mnyama kiboko akiwa kwenye maji wakati mabalozi wakitembelea Hifadhi ya Ngorongoro,mkoani Arusha. (PICHA NA ASSAH MWAMBENE)

MWANAMZIKI ALIYETUNGA DONT KUBEBA ZAMBIA ATAKA SATA AMKUMBUKE


Dandy Krazy al maarufu kama ZED
LINK YA WIMBO HAPO JUU
na Danny Tweve  -Lusaka
Mwanamziki Dandy Krazy wa nchini Zambia Maarufu kama ZED ambaye hivi karibu wimbo wake wa Don’t kubeba(donch kubeba) ukimaanisha tunza siri! Ameibuka akimtaka rais mpya Michael Sata ampe madaraka kwakuwa wimbo wake ulifanya kampeni zilizomwezesha kuingia madarakani.
Akizungumza katika moja ya taarifa za Televisheni ya nchini humo ya Muvi, Kratzy amesema wimbo huo ambao ulitumika kama slogan ya chama cha Patriotic Front ulikuwa ujumbe mhimu katika mafanikio ya rais Sata baada ya kutumika katika kipindi chote cha kampeni.
Mmoja wa wanaharakati nchini Zambia ambaye pia ni mwandishi wa habari Henry Kabwe, serikali ya Zambia imelichukulia jambo hilo kama kitu cha kawaida, ingawa mwanamziki huyo bado ameendelea kusisitiza kuwa anategemea kudra za rais kumpa madaraka katika teuzi zake zinazoendelea.
ZED anatumia msemo huo ambao rais Satta alikuwa akisisitiza wakati wa kampeni za kimya kimya kabla ya kutangaza nia yake ya kugombea urais kwa mara ya kwanza baada ya kuacha kazi kwenye shirika la Reli la Uingereza .
Kutokana na madai hayo ya ZED wananchi wa Zambia wamekuwa nyuma yake wakieleza kuwa mwanamziki huyo alijitoa moja kwamoja na kuonyesha wazi kutunga nyimbo za kumpamba Sata na kwamba hatua yake ya kudai ujira wa madaraka ni muhimu iungwe mkono
Staili ya wimbo huo inachezwa kama kiduku kwa mapaja kutawanyika na baadaye kukutanishwa, imekuwa maarufu nchini Zambia na wimbo huo umekuwa ukipigwa  kwenye maduka ya kanda na yale ya kawaida licha ya kampeni na uchaguzi kwisha.
Donch kubeba imemfanya ZED kuwa adui wa chama cha MMD ambacho kilikuwa kimemsimamisha mgombea wake kwa mara ya pili Rupia Banda.
Kwa ujumla mali zilizokuwa zikimilikiwa na chama hicho ambazo zilitokana na michango ya wananchi zimenyang’anywa na serikali ya sata ikiwa ni pamoja na michango iliyokuwa ikichukuliwa kwenye masoko na ushuru mwingine.

GOOD MORNING MY SON


Ulimwengu wa 001011000 - no analog

Ulimwengu wa leo tekinologia ya digital inaenea kwa kasi ya ajabu, kwani haichagui nahali, watu, rika nk KUTOKA JAMII FORUMS