Adverts

Nov 30, 2011

Waziri wa mambo ya nje Kenya apingana na uamuzi mahakama kuu!kulikoni?

Waziri wa mambo ya nje wa Kenya ameelezea wasi wasi wake mkubwa katika maamuzi ya mahakama kuu ya kuamuru kukamatwa kwa rais wa Sudan Omar al Bashir.
Kwa mujibu wa VOA Mosses Wetangula alisema katika taarifa jumanne kuwa amri hiyo haisaidii kitu na inasababisha msuguano wa moja kwa moja juu ya msimamo wa kwamba wakuu wa nchi hawawezi kushitakiwa kwa mashitaka ya uhalifu. Ameongeza kuwa serikali ya Kenya inatafakari juu ya kukata rufaa.
Rais Al Bashir anatafutwa na mahakama ya kimataifa ya uhalifu kwa mashitaka ya uhalifu wa kivita katika eneo la Darfur Sudan ambapo serikali yake imekuwa ikipambana na waasi tangu 2003.
Hivi karibuni Mahakama kuu ya Kenya ilitoa uamuzi kwamba serikali ya nchi hiyo lazima imkamate Bashir kama akiingiza mguu wake” nchini humo. Lakini Waziri wa mambo ya nje anapopinga hilo serikali inatoa picha gani tunageukia maneno ya mwimbaji aitwaye Jaguar na kusema hili si kigeugeu?!!! Habari hii kwa hisani ya sundauSumari
Sikiliza katuni ya wimbo huo ukiongozwa na Raila!

WANA RUVUMA, RUKWA NA KATAVI WAITEMBELEA MAKUMBUSHO NA NYUMBA YA UTAMADUNI DAR ES SALAAM

Mkuu wa mkowa wa Rukwa Mh Eng Stella Manyanya (MB) (alie simama) akimsikiliza kwamakini Mkurugenzi wa Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Dar es Salaam, Dkt Pual Msemwa, wengine ni wanakikundi wa Ngoma kutoka Ruvuma walio kuja kuhudhuria Tamasha la watani zao la Jamii ya watu wa Rukwa na Katavi lililo fanyika Kijiji cha Makumbusho hivi karibuni.
Watani wa Wangoni jamii ya watu wa Rukwa na Katavi nao walipata wasaa wakuitembelea makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Dar Es Salaama. Hapa wakiangalia magari ya Kihistoria.
Wanakikundi wa ngoma toka Mkoa wa Ruvuma wakimsikiliza kwa makini mtaalam wa Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni juu ya Mwenge Uliopandishwa mlima wa Kilimanjaro miaka ya 60.
Chifu Emanuel Zulu Nkosi wa Wangoni na wanakikundi cha Ngoma cha mkoa wa Ruvuma wakipata maelezo toka kwa Mama Shayo walipo tembelea makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Dar es Salaam, Dkt Paul Mswemwa akiwakaribisha wanajamii wa Rukwa na Katavi walipo wasili makumbusho hapo.
Kikundi cha Ngoma kutoka Ruvuma kikiwa katika picha ya pamoja na Chifu wa Wangoni alie shika mtoto katikati. kutoka swahili villa

Nov 29, 2011

HALI YA TUNDUMA BAADA YA AJALI YA MOTO NI MAJONZI, RC AWAPA POLE

Mkuu wa mkoa wa Mbeya akizungumza na wafanyabiashara wa Tunduma baada ya tukio la ajali ya Moto  leo jioni ambapo amewapa pole kutokana na maafa hayo.

Watu wakiokota mabaki ya vitu vilivyoungua kwenye maduka ya eneo la TUNDUMA maarufu kama Mansese

Mkuu wa mkoa wa Mbeya Abas Kandoro akitembelea eneo ambako moto umetekeza maduka katika mji wa Tunduma

Moto ukiendelea kuwaka kutokana  na ajali iliyotokea jana jioni na kusababisha hasara ya mabilion  ya fedha katika mji wa Tunduma wilayani Mbozi

Anadarko touts East Africa natural gas prospects Shares surge on news.Kusini kutashikika!!!!

By Steve Gelsi, MarketWatch NEW YORK (MarketWatch) — Anadarko Petroleum Corp. on Monday doubled its reserve estimate for natural gas fields off the coast of East Africa and said it’s moving toward an investment decision on a proposed liquefied natural gas operation in the region. Anadarko APC +0.38% said it could recover up to 30 trillion cubic feet from waters near Tanzania and the island nation of Madagascar — an area that the company hailed as possibly “one of the most important natural gas fields discovered in the last 10 years.”
Nearly 4 trillion cubic feet were in storage in the United States as of last week, according to the Energy Information Administration. The U.S. consumes about 2 trillion cubic feet of natural gas per month Shares of Anadarko jumped 5.5% as energy stocks rallied amid a 291-point jump in the Dow Jones Industrial Average DJIA +2.59% . Read the latest news on stocks in the energy sector. Anadarko said the latest in a series of exploration wells, the Barquentine-3, encountered more than 600 feet of natural gas pay and helped it lift its reserve estimate for the area. In discussing its findings, the company also presented a conceptual design for an LNG processing facility envisioned for the region, with a preliminary design by KBR Inc. KBR +5.40% . Analysts at Canaccord Genuity Energy Research reacted to the news by reiterated their buy rating and $103 price target for Anadarko. The announcement amounts to a positive for the company since it suggests a bigger resource, even as analysts said exports from Mozambique won’t likely start until 2018, beyond its usual five-year horizon for profit estimates. “This announcement has no impact in our model though reinforces our view that Anadarko’s deepwater exploration portfolio and execution is world-class,” Canaccord Genuity said. The Barquentine discovery comes after Anadarko announced in 2010 two of the largest deepwater discoveries in the world at its Windjammer and Lagosta wells in Mozambique. All told, Anadarko holds stakes in 13 million gross acres in Mozambique and Kenya in East Africa. Anadarko is the operator of the fields in Mozambique, with an ownership stake of 36.5%. The remainder is divided by ENH Hydrocarbonetos de Mozambique, Mitsui & Co. Ltd. JP:8031 +1.16% , Videocon, Bharat Petro Resources, and Cove Energy PLC. Anadarko’s update on Mozambique comes less than a month after the company announced a find of up to 1.5 billion barrels of oil in the Wattenberg shale in northeast Colorado. See: Anadarko’s strike in the Rocky Mountains

SOKO LA KISIMANI MJI MDOGO WA TUNDUMA LILIVYOTEKETEA KWA MOTO.

Soko la Kisimani lililopo mji mdogo wa Tunduma
Mkuu wa wilaya ya Mbozi Gabriel Kimolo akiwa eneo la Tukio

Soko la Mji wa Tunduma wilaya ya mpya ya Momba mkoani Mbeya limeteketea kwa moto hapo jana kuanzia majira ya Saa 10 jioni na kusababisha hasara kubwa ambapo vibanda vya biashara na maduka yameteketea kwa moto huo. Chanzo hakijaweza kubainishwa lakini inadaiwa kuwa Umeme uliporudi baada ya kukatika ndipo moto ulipoanza katikati ya Soko hilo
Vibanda vilivyokuwa vimejengwa kwa mbao vimeteketea na kubakia masalia ya mabati yaliyotumika kuezekea vibanda hivyo katika Soko la Kisimani lililopo mji mdogo wa Tunduma, wilaya ya mpya ya Momba mkoani Mbeya, jana kuanzia majira ya Saa 10 jioni na kusababisha hasara kubwa ambapo vibanda vya biashara na maduka yameteketea kwa moto huo.
Kijana mmoja aliyevalia mwenye fulana ya Bluu akiwa amekamatwa wakati akijaribu kutorosha baadhi ya mali zilizokolewa katika moja ya maduka yaliyoteketea kwa moto katika soko la Kisimani lililopo mji mdogo wa Tunduma, wilaya ya mpya ya Momba mkoani Mbeya , jana kuanzia majira ya Saa 10 jioni na kusababisha hasara kubwa ambapo vibanda vya biashara na maduka yameteketea kwa moto huo.
Baadhi ya wafanyabiashara wakiwa wamebeba mizigo ya mali zao mara baada ya kufanikiwa kuokoa mali zao katika Soko la Kisimani lililopo mji mdogo wa Tunduma, wilaya ya mpya ya Momba mkoani Mbeya lililoteketea kwa moto hapo jana kuanzia majira ya Saa 10 jioni na kusababisha hasara kubwa ambapo vibanda vya biashara na maduka yameteketea kwa moto huo.
Baadhi ya wafanyabiashara wakipakia mizigo ya mali zao katika gari mara baada ya kufanikiwa kuokoa mali zao katika Soko la Kisimani lililopo mji mdogo wa Tunduma, wilaya ya mpya ya Momba mkoani Mbeya lililoteketea kwa moto hapo jana kuanzia majira ya Saa 10 jioni na kusababisha hasara kubwa ambapo vibanda vya biashara na maduka yameteketea kwa moto huo.
Askali wa kampuni ya Ulinzi akitizama mali iliyookolewa katika moja ya maduka ambapo wananchi waligombania mali hizo na kuzichukua wakati Soko la Kisimani lililopo mji mdogo wa Tunduma, wilaya ya mpya ya Momba mkoani Mbeya likiendelea kuteketea kwa moto hapo jana kuanzia majira ya Saa 10 jioni na kusababisha hasara kubwa ambapo vibanda vya biashara na maduka yameteketea kwa moto huo.
Mbao zilizokuwa zimetumika kujengea vibanda vya biashara zikiwa zimevunjwa ikiwa ni moja ya njia ya kudhibiti moto kutoendelea kuteketeza vibanda, maduka na mali za wafanyabiashara katika soko la soko la Kisimani lililopo mji mdogo wa Tunduma, wilaya ya mpya ya Momba mkoani Mbeya lililoteketea kwa moto hapo jana kuanzia majira ya Saa 10 jioni na kusababisha hasara kubwa ambapo vibanda vya biashara na maduka yameteketea kwa moto huo.
Pichani ni duka ni moja wapo ambalo halikuweza kuteketea kwa moto, ambapo ukitazama juu ya paa Paka aliyekuwa na rangi Nyeusi hakuweza kutoweka hapo, licha wa moto kuendelea kuteketeza maduka na vibanda vya biashara katika soko la Kisimani lililopo mji mdogo wa Tunduma, wilaya ya mpya ya Momba mkoani Mbeya lililoteketea kwa moto hapo jana kuanzia majira ya Saa 10 jioni na kusababisha hasara kubwa ambapo vibanda vya biashara na maduka yameteketea kwa moto huo.
Magari ya kampuni ya Ujenzi wa barabara ya Tunduma mpaka Sumbawanga yalifika kutoa msaada wa kudibiti moto katika Soko la Kisimani lililopo mji mdogo wa Tunduma, wilaya ya mpya ya Momba mkoani Mbeya lililoteketea kwa moto hapo jana kuanzia majira ya Saa 10 jioni na kusababisha hasara kubwa ambapo vibanda vya biashara na maduka yameteketea kwa moto huo.
Gari la zimamoto likiwasili eneo la tukio kudhibiti moto kutoendelea kuteketeza maduka, vibanda vya biashara na bidhaa katika soko la Kisimani lililopo mji mdogo wa Tunduma, wilaya ya mpya ya Momba mkoani Mbeya lililoteketea kwa moto hapo jana kuanzia majira ya Saa 10 jioni na kusababisha hasara kubwa ambapo vibanda vya biashara na maduka yameteketea kwa moto huo.

Mzee huyu alishikwa na bumbuwazi la kutoamini duka lake likiteketea kwa moto ambapo hivi karibuni aliingiza mzigo wa bidhaa kutoka jijini Dar es salaam uliogharimu shilingi milioni Ishirini.
Na Ezekiel Kamanga
Moto mkubwa umeteketeza kabisa soko la Kisimani lililopo mji mdogo wa Tunduma wilaya mpya ya Momba mkoani Mbeya, jana na kusababisha hasara kubwa ya mali kuteketea na baadhi ya watu kujeruhiwa.

Zaidi ya wafanyabiashara elfu moja wameathiriwa kiuchumi kutokana na moto huo ulioanza majira ya saa 10 jioni mara umeme ulipo rudi baada ya kukatika na hivyo kusababisha moto kuzuka katikati ya vibanda ndani ya soko.

Juhudi za kuuzima moto huo zilichukua muda kutokana na mji huo wa kibiashara kukosa gari la zima moto, hali iliyolazimu magari ya maji(boza) yanayotumika kujenga barabara kutoka Mji wa Tunduma kwenda mkoani Rukwa kusaidia kudhibiti moto huo na kusaidiwa na magari mawili ya zima moto kutoka wilaya ya Nakonde ya nchini Zambia ambapo nayo yalishindwa kuzima moto huo.

Hata hivyo magari mawili kutoka jijini Mbeya yalifika eneo la tukio majira ya saa moja na robo usiku ili kudhibiti moto huo.

Uhaba wa maji katika mji huo umechangia kwa kiasi kikubwa kukwamisha shughuli za uzimaji moto huo kwani magari kutoka nchini Zambia yaliishiwa maji mapema.

Mkuu wa wilaya ya Mbozi Bwana Gilbert Kimolo alifika mapema kutoa pole kwa wahanga na kuwaomba kuwa watulivu kutokana na janga kubwa lililowakuta na kwamba serikali inafanya uchunguzi ili kuweza kubaini chanzo hicho cha moto.