Adverts

Apr 7, 2009

CHIFU NAYE YUMO KUPAMBANA NA UJINGA

Hii ni timu ya Mila na desturi iliyomkaribisha JK alipotembelea wilaya ya Mbozi, alivishwa pamba za kimila kumtambua kama "mwene" mzee huyu kutoka kijiji cha Hatelele anasisitiza kuwa pamoja na kupewa uchifu, jukumu kubwa ni kuhakikisha watoto wa Mbozi wanakwenda shule!

Jengo la kitegauchumi la NSSF Mbozi

Huu mjengo ndiyo sura ya Mbozi, tunawashukuru NSSF kwa kutambua umuhimu wa kuipa tafu Mbozi kwa kujenga jengo lenye kuleta sura nzuri, hapa bwana ndilo ghorofa lililopo barabarani unapoelekea Zambia!! Mbozi tumo.

KAMERA NAZO ZIPO BWANA

Waala huu sio mzigo ni tukamera tuchache, tena zinginenimeziacha nyumbani jumla ninazo arobaini na tisa!!!! ndivyo anavyonekana huyu mpiga picha akiwa na mzigo wa kamera kumvizia JK angalau apate ya ukumbusho!!! pembeni ni mpiga picha wa JK aliyepatikana jina moja la Lukuvi akiwa anamshangaa jamaa!!!! hii yote matunda ya amani ingekuwa nchi zingine haruhusiwi kusogea na vikamera vyake !!!!!!

Mbozi Nzuri bwana hata Jk ameipenda

Rais Jakaya Mrisho Kikwete siku alipotembelea wilaya ya Mbozi, kushoto kwake ni Mkurugenzi Mtendaji CRDB Bank Dr Charles Kimei, akifuatiwa na Mama Salma Kikwete. Wengine ni watumishi wa benki ya CRDB, hii ilikuwa ni tukio la uzinduzi wa tawi la CRDB mbozi

Jioni Mbozi huwa hiviiii

Hii yote ni madhari ya kuvutia katika wilaya ya MBOZI, jua linaelekea kuzama, lakini ni kwa kiasi gani tumetumia fulsa za utalii kuitangaza wilaya yetu? Karibuni Mbozi, nchi yenye neema na utajiri wa vivutio.

Danny

Timu ya veteran Simba katika mji wa Vwawa

Timu ya Veteran Mjini Vwawa katika Wilaya ya Mbozi ,imekuwa na utaratibu wa kuwafanyia mauaji ya mwaka kila mara inapokutana na wapinzani wao Veteran Yanga. Mechi ya hivi karibuni itafanyika wakati wa siku kuu za pasaka. Subiri Matokeo.
Danny

Mbozi sasa macho kwenye elimu

HALMASHAURI YA WILAYA YA MBOZI (Barua zote ziandikwe kwa Mkurugenzi Mtendaji) Simu Na. 025 - 2580272 P.O. Box 3, Fax Na. 025 – 2580278 Mbozi – Tanzania E- Mail mbozi@iwayafrica.com Wilaya ya Mbozi imekiri kunufaika na utekelezaji wa mradi wa maendeleo ya Jamii TASAF kutokana na mchango wake katika maendeleo ya sekta ya elimu. Kiasi cha shilingi million 412,664,558.00 zimeelekezwa kwenye utekelezaji wa miradi ya Ujenzi wa mabweni, Nyumba za walimu, na madarasa katika vijiji 25 vya wilaya ya Mbozi. Akizungumza na balaza la madiwani la Halmashauri ya wilaya ya Mbozi, Mkuu wa wilaya ya Mbozi amesema moja ya mambo ya kujivunia ni hatua ya kuongezeka kwa shule za sekondari kutoka 12 wakati akiingia wilayani Mbozi hadi kufikia shule 52 sasa. Anaeleza kuwa hatua hiyo kwa sehemu kubwa inatokana na wananchi kudhamilia katika kujikomboa na ujinga kulikochangiwa na kuungwa mkono na miradi ya Maendeleo kama TASAF na mipango mingine. Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Mbozi bwana Levison Chilewa anaesema mafanikio hayo ni sehemu ya mikakati iliyowekwa na watendaji wa halmashauri ya wilaya kwa ushirikiano na madiwani wao kuhakikisha kuwa angalau watoto wanaohitimu darasa la saba na kufaulu kwenda sekondari wanapata nafasi. Kwa mwaka 2009/2010 halmashauri ya wilaya ya Mbozi inakusudia kukamilisha ujenzi wa mabweni 13 katika shule za sekondari za kata kupitia fedha za Mfuko wa maendeleo ya jamii TASAF na nguvu za wananchi. Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Mbozi bwana Aden Mwakyonde anasema ukombozi wa wananchi utatokana na elimu kwakuwa maeneo mengine kama uwezo wa kipato tayari yameshaonyesha mafanikio kutokana na pato la zao la kahawa ikilinganishwa na wilaya zingine za mikoa ya nyanda za juu kusini. Ni ukweli usiopingika kuwa wilaya ya Mbozi imekuwa na utajiri wa fedha miongoni mwa nwananchi wake unaochangiwa na kipato kikubwa cha zao la kahawa ,lakini bado wananchi wake wamekuwa wakiishi maisha ya ujima kutokana na mfululizo wa matukio ya kinyama yanayoripotiwa na vyombo vya habari yakiwemo mauaji ya uchunaji ngozi. Hali hii inadhihirisha kuwa bado suala ya elimu lipo nyuma na ndiyo sababu wilaya imeweka suala la elimu kama kipaumbele chake katika kuwezesha mazingira ya kusomea yanaimarishwa na shule kuwa eneo la kuvutia watoto kuikimbilia elimu badala ya kuikimbia elimu. Takwimu za ubora wa majengo zinaonyesha kuwa wilaya ya Mbozi ni miongoni mwa wilaya nchini zinazoongoza kwa kuwa na shule bora za msingi (majengo) ambapo wastani wa halmashauri za wilaya, manispaa na miji 15 hutembelea kwa mwaka kujifunza na kuona ujenzi huo. Katika kufanikisha jitihada hizo wilaya ya Mbozi imeanza harakati za kupanua mfuko wa elimu ambapo inakusudia kukusanya kiasi cha shilingi Bilion 12 kwa awamu tatu, awamu ya kwanza ikilenga kukusanya kiasi cha shilingi billion 3 kwa mwaka. Wanananchi wanaeleza kuwa kuimarishwa kwa miundombinu hasa barabara zinazofika vijijijini mwao ni mwanzo mzuri wa kufanikisha mpango wa kuinua elimu vijijini mwao kwasababu sasa watoto wataweza kwenda na kurudi kwenye shule za kata tofauti na mazingira ya awali. Kiasi cha shilingi Bilion 1.4 zilizoelekezwa na mfuko wa maendeleo ya jamii TASAF wilayani Mbozi zinakusudia kuchangia mabadiliko makubwa ya ukuaji kiuchumi kwakuwa sehemu kubwa ya fedha hizo zimeelekezwa katika maeneo chochezi ya uchumi ingawa yapo katika huduma za jamii anaeleza afisa mipango bwana Nyarubamba. Chini ya mpango huo barabara 8 na madaraja matano vimejengwa kwa kiasi cha shilingi million 428 kiwango ambacho anaeleza kuwa ni mrija muhimu katika kuchavusha uchumi wa wilaya ya Mbozi hasa katika kupeleka pembejeo wakati wa uzalishaji na kusafirisha mazao baada ya kuvunwa tayari kwenda sokoni. Mkuu wa wilaya anayemaliza muda wake Bi Halima Kihemba anasema kuwa moja ya maeneo ambayo bado yanahitaji msukumo wa pekee ni vita dhidi ya matukio ya ushirikina ambayo yameiweka wilaya kwenye sura ya ujima. Anasema kura za maoni juu ya watu wanaojihusisha na vitendo vya kishirikina, mauaji ya albino na wizi na uuzaji wa dawa za kulevya ni viashiria dhahiri kuwa wananchi wamechoshwa na matukio hayo ni kwamba takwimu za waliopigiwa kura zinaonyesha majina mengi kujirudia rudia dalili zinazoonyesha kuwa wananchi wanataarifa zitakazosaidia kazi ya kuwachunguza watuhumiwa hao. Hata hivyo yapo maeneo yanayohitaji zaidi msukumo hasa matumizi ya utajiri uliopo mara baada ya kwisha kwa msimu wa kuuza kahawa yao, wengi wa wakulima wanaelekeza kwenye matumizi yanayochochea migogoro miongoni mwao. Mfano ni ongezeko la kesi za ugoni kila mara baada ya msimu wa kuuza kahawa, hii inadhihirisha kuwa sehemu kubwa ya mapato hayo hutumika katika masuala yasiyo changia tija na maendeleo moja kwa moja. haya yote yanabaki kuwa ni sehemu ya changamoto za mafanikio yaliyopo,lakini kubwa zaidi ni wananchi kutambua fulsa zilizopo katika kujiletea maendeleo kwa wao kupokea program za elimu zinazohamasishwa sasa ili waweze kupiga hatua kama ilivyo kwa mikoa mingine kama Kilimanjaro. Kuwepo kwa mpaka wa Tunduma iwe fulsa nyingine kwa wananchi wa mbozi kujifunza ustaarabu wa maendeleo kwa pande zingine kama Zambia, DRC kongo nk, haya yote yanazidi kupanua fulsa za kukimbia kimaendeleo wakati wilaya zingine zikienda mwendo wa kinyonga. Dhamira ipo na wananchi wanania, chamsingi ni kusimamia dhima na moto wa wilaya ya Mbozi wa Mbozi maendeleo, maendeleo yataletwa na sisi wenyewe kwa ushindani!!!!!!!!!!!!!! Danny Tweve

Apr 3, 2009

WACHINA WAKABIDHI MAJENGO YAO

Kampuni ya ujenzi barabara na Madaraja ya China imekabidhi majengo yake manne yenye thamani ya shilingi million 33 ili yatumike kwaajili ya makazi ya walimu sita wa shule ya sekondari Ihanda katika wilaya ya Mbozi mkoani Mbeya. Majengo hayo ni sehemu ya raslimali za kampuni hiyo baada ya kuvunja kambi yake ya ujenzi wa barabara ya Songwe hadi Tunduma hivyo kuombwa na serikali ya wilaya kuyaachia majengo hayo ili yaweze kutumika kama makazi ya walimu. wa kwa mradi wa barabra mwaka 2005.ambikabidhiano hayo yaliyofanywa kati ya mwakilishi wa kampuni hiyo Luteni Mstaafu Michael Esanju na Mwakilishi wa mkuu wa wilaya ya Mbozi bwana Leornard Magacha na Mkurugenzi wa wilaya Bwana Levision Chilewa pia yamehudhuliwa na wanafunzi wa shule hiyo ambao wameyapokea kwa shangwe. Wakizungumzia hatua hiyo Mwakilishi wa mkuu wa wilaya Bwana Leonard Magacha, Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya bwana Levison Chilewa na baadhi ya wanafunzi wamesema hatua hiyo inakwenda sambamba na mkakati wa wilaya wa kuboresha mazingira ya kusomea na kufundishia na kwa upande wa halmashauri itahakikisha majengo hayo yanakarabatiwa kukidhi ubora Kwa upande wake afisa elimu wa wilaya ya Mbozi bwana Juma Kitabuge na mwakilishi wa kampuni ya China Road and Bridge Cooperation Luteni mstaafu Michael Esanju wamesema msaada huo unaifanya kampuni kuwa sehemu ya mafanikio yatakayofiwa katika siku za baadaye katika kuandaa vijana walioelimika kutoka kwenye kata ya Ihanda Danny
SHIRIKA la viwango nchini TBS limezindua maabara Ugezi (inayotembea) katika mikoa ya Nyanda za juu ikiwa ni hatua ya kuhakikisha ubora wa bidhaa zinazolengwa kuuzwa nje unalindw. Sambamba na hilo maabara hiyo inalenga pia kuwapunguzia gharama wateja wake ambao kwa sehemu kubwa ni viwanda vilivyopo kwenye mikoa hiyo ambapo huduma tano zitatolewa na maabara hiyo katika hatua mbali mbali za uzalishaji wa bidhaa za viwanda. Uzinduzi huo umefanywa kwenye kiwanda cha saruji cha Mbeya na Maafisa Ubora waandamizi wa TBS bwana Ingramu Kisamo na Alfonce Kagoma ambao kwa pamoja pamoja na kutembelea na kukagua maabara ya kiwanda hicho pia wameelezea faida zitakazopatikana kutokana na matumizi ya maabara hiyo ikiwemo viwanda kufahamu ubovu na hitilafu za mitambo yao ya uzalishaji, kufuatilia mifumo ya umeme, msukumo na hali joto Kwa upande wake afisa uhusiano wa TBS Bi Roida Andusamile pamoja na afisa Uzalishaji wa kiwanda cha saruji Mbeya bwana Usiri ELILIA wamesema msaada wa gari hilo kutoka UNIDO ni hatua nyingine muhimu itakayoongeza mahusiano baina ya watumiaji wa huduma za TBS na wazalishaji katika kujihakikishia bidhaa zinazozalishwa zinazingatia viwango vya kimataifa. Chini ya maelekezo ya shirika la afya Ulimwenguni bidhaa zinazozalishwa na kuuzwa nje zinapaswa kupitishwa na taasisi za ubora za ndani na upande wa tatu ambao ni huru na kwakutumia vifaa vilivyopitishwa, na kwamba gari hilo ni sehemu ya mitambo iliyopitishwa kwa umahiri katika kuhakiki viwango tangu wakati wa uzalishaji. Danny

TIGO YAELEKEZA NGUVU MASHULENI -MBOZI

Mbozi Kampuni ya simu za mkononi ya TIGO imezindua mfuko wa elimu ujulikanao kama TIGO elimu kwa taifa la Tanzania na kukabidhi vitabu 500 vya hisabati kwa shule 10 za sekondari wilayani Mbozi mkoani Mbeya ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wake. Akikabidhi vitabu hivyo kwa mbunge wa jimbo la Mbozi Mashariki Mh Godfrey Zambi, Meneja wa Tigo kanda ya Kusini bwana Willy Mwakiema amesema chini ya mpango huo, maeneo ya sekta za michezo, afya na hata uchangiaji vifaa vya elimu mashuleni yatazingatiwa ili kuwezesha mazingira bora ya upatikanaji wa elimu kwa watoto. Kwa upande wake bwana Mbunge wa Mbozi Mh Zambi ameelezea kufurahishwa na mpango huo kuzinduliwa kitaifa jimboni kwake na kuelezea hatua hiyo kama Ukombozi kwa watoto walio vijiji hasa kwa kuzingatia mazingira ya shule nyingi zilizo kwenye ngazi ya kata yanafanana, na kukabiliwa na ukosefu wa vitabu husunani somo la hisabati ambalo ni msingi muhimu kwa wasomi wa baadaye. Kwa upande wake kaimu mkurugenzi wa halmashauri hiyo bwana Lingson Ngaikwela na kaimu Katibu Tawala Bwana Salehe Simba wameeleza kuwa matunda ya Mpango wa MEM yanatarajiwa kuanza kuonekana katika matokeo ya mitihani ya darasa la saba mwaka huu na kwamba wilaya ya Mbozi inatarajiwa kufaulisha watoto 13,000 kiwango ambacho nyenzo kama vitabu ni suala la msingi katika kuwaendeleza Makabidhiano hayo yamehudhuliwa na viongozi wa halmashauri ya wilaya na mwakilishi ofisi ya mkuu wa wilaya pamoja na wadau wa elimu wilayani humo ambapo vitabu hivyo kuanzia kidato cha kwanza mpaka cha tatu vina thamani ya shilingi millionTano Danny