Adverts

Jan 24, 2013

MAZINGIRA YA KUSOMEA YA CHUO CHA MIPANGO YAZIDI KUBORESHWA



 wadau pamoja na mtendaji wa Mtandao huu wakiwa ukumbi wa maktaba ya Chuo cha Mipango ghorofa ya pili ambako ni maalumu kwa majadiliano ya vikundi
Ilikuwa ni wakati wa kukimbizana na reseach paper

Kazi inaendelea kila mtu akiwa kainamia kazi!

Mkuu wa chuo cha Mipango Constantine Lifurilo

Mkurugenzi sehemu ya raslimali watu Bw Tibelio Mdendemi akisisitiza jambo wakati wa mahojiano na mtandao wa indaba africa

Jan 23, 2013

MAKETE NA MAZINGIRA YAKE YANAVYOVUTIA KWA VIUMBE MBALI MBALI

Hili ndilo eneo la Kitulo ambapo sasa ni miongoni mwa mbuga za wanyama zenye mvuto wa aina yake kutokana na kusheheni aina mbali mbali za maua  na ndege ambao hutua  mara moja katika kipindi cha mwaka mzima 

Hivi ndivyo makete inavyoonekana kwa mbali  katika baadhi ya vijiji 

Hii ni sura ya miongoni mwa vijiji vya wilaya ya Makete hapa ni Isapulano 

Bado Makete mazingira yake hayajaharibiwa na ikiwa wananchi wataendeleza ile mipango ya miaka mingi ya upandaji miti, hali ya misitu huenda ikarejea katika kipindi cha miaka michache ijayo

Wanyama hawa maarufu kama simbilisi hufugwa kwa wingi katika wilaya ya Makete na wanafaa kwa lishe ! wana sifa za kuzaliana sana hasa kwenye mazingira yenye moto  karibu(jikoni)

Hapa ni wilayani Makete na kwa mbali kinaonekana chuo kipya cha VETA MAKETE , wilaya ya Kazi ndiyo motto wa wilaya Makete

PICHA ZOTE KUTOKA KWA TITO NGAJILO WA MAKETE PLATFORM

VACANCIES UNIVERSITY OF DAR ES SALAAM

VACANCIES UNIVERSITY OF DAR ES SALAAM:



The university of Dar es salaam invites applications from suitably qualified Tanzania to be considered for immediate employment to fill the following vacant post.
  • Security Guard 11 ( 6 posts)
  • Office Attendant ( 6 posts)
  • Office Management Secretary(7posts)
  • Assistant Accountant (1 post)
  • Accounts Assistant ( 3 posts)
  • Transcriber 11 (1 post)
  • Principal Technician (2 posts)
  • Chief laboratory Technician (1 post)
  • Principal Administrative Officer 1 ( 4 Post)
  • Laboratory Assistant II (2 posts)
  • Telephone Operator II (1 post)
  • Senior Administrative Officer III (2 posts)
  • Chief Laboratory Scientist (1 Posts) 
  • Office Supervisor III (1 posts)
  • Chief technician (4 Posts)
  • Principal Artisan (2 posts) 
  • Library Officer II (4posts)          
  • Waiter (1 post)
  • Chief Workshop instructor-Welding,Forging and Casting(1 post)
  • Editor II (2 posts)
  • Library Assistant II(2 posts)
  • Nursing Officer III (2 posts)
  • System Administrator II (1 Post)
  • Principal Internal Auditor I (2 post)
  • Auxiliary Policy (1 post)
  • Chief Public Relations Officer (1 post)
  • Driver II (4 Posts)
  • Administrative Assistant II(3 posts)
  • Janitor II (1 post)
  • Accountant II (1 post)
  • Optometrist (1 post)
TERMS OF SERVICE.
Permanent and Pensionable

REMUNERATION
Attractive package will be offered to the right candidate commensurate with his/her qualifications and experience.

MODE OF APPLICATION
Interested candidates should apply in confidence to the undersigned enclosing

  1. Detailed Cv
  2. Photocopy of relevant certificates and transcripts
  3. Names and address of two referees
  4. Mode of communication eg Telephone,Fax,Email.
NOTE
  • Candidate should indicate the permit reference number ie. (BC.10/87/01/E/73) in their letter
  • For the position of Technicians, Artisans and workshop instructor candidate should indicates the sections and department which they apply.
  • Applicants for all positions should be below 45 years.

Deadline.
Two weeks from the date of First appearance of this advertisement

Interested applicants should submit their applications to the:

Deputy Vice Chancellor ( Administration)
University of Dar es salaam,
P.o Box 35091,
Dar es salaam.

Jan 19, 2013

GARI LAPINDUKA NA KUUA NG'OMBE 25 PAPO HAPO, WANANCHI WACHANGAMKIA VIBUDU

Mama huyu akiwa eneo la Tukio kusubiria nyama ya bei chee iliyokuwa inauzwa na vijana waliojiajiri kuchinja  ng'ombe waliokufa kwenye ajali hiyo iliyotokea eneo la Old Vwawa wilayani Mbozi

Hapa jamaa akibeba kichwa cha ng'ombe baada ya kujimegea vipande vyake tayari kupeleka nyumbani

Hapa akipeleka nyumbani kwake kwa mwendo wa pole! vichwa viiwili mkononi e bwana eeee

Hapa maini yalishachambuliwa yamebakia mapupu huku ng'ombe huyu aliyehai akishuhudia wenzake wanavyocharangwa mautumbo yao mbele yake! ngombe huyu amevunjika miguu yote kwenye ajali hiyo

Hili ndilo gari lililotumbukia kwenye mto Old Vwawa na kuua ng'ombe 25 kati ya 46 waliokuwa wakisafirishwa kutoka sumbawanga kwenda mbeya,

Katika ajali hiyo ng'ombe mmoja kama anavyoonekana amening'inia kwenye bodi alishindwa kuchomolewa hapo, wakati huo pia watu watano wamejeruhiwa kwenye ajali hiyo ambapo walitibiwa na kuruhusiwa

Afisa mifugo wilaya ya Mbozi bwana Thabit Rukarisha akizungumzia wananchi kuuziwa mizoga ya Ng'ombe ambao hawajapimwa katika miji ya Tunduma,VWAWA na Mlowo wilayani MboziPuch

SAFARI YA MWISHO YA MDAU WETU CLETUS MUNISHI

mara baada ya mwili kuwasili nyumbani kwake mwenge (PICHA ZOTE NA MWAIPULA PRODUCTION MBOZI)

Mwili ukishushwa kutoka kwenye gari









Familia ya NMB walikuwa pamoja wakati wa msiba wa mwenzao ambaye atakumbukwa kwa ucheshi wake



Mwisho wa maisha yake katika mazingira ya mbozi ulikuwa huu hapa mara baada ya misa ya kumwombea (picha zote na MWAIPULA PRODUCTION)

Jan 18, 2013

KANDORO AKATAA SOKOMATOLA KUNYANG'ANYWA VIWANJA


MKUU WA MKOA MBEYA ABAS KANDORO AKIONGEA NA WAHESHIMIWA MADIWANI HIVI KARIBUNI
MKUU WA WILAYA MBEYA NORMAN SIGALLA AKIWA NA MKURUGENZI WA JIJI LA MBEYA IDDI WAKIMSIKILIZA MKUU WA MKOA
WAHESHIMIWA MADIWANI
HIZI NDIZO NYUMBA ZA SOKOMATOLA JIJINI MBEYA HUU NI MTAA WA KANISA
HUU NI MTAA WA NONDE

HALMASHAURI ya jiji la Mbeya imeshauriwa kumaliza mgogoro kati yake na wakazi wa eneo la Sokomatola kwa kuruhusu wakazi hao kufanya mazungumzo na wafanyabiashara wakubwa wao wenyewe ili waweze kukubaliana na kuuziana nyumba.
Kwa muda mrefu halmashauri imekuwa ikilumbana na wakazi wa eneo hilo ambapo ilitaka kuwahamisha na kisha ichukue ilichukue na kugawa viwanja upya kwa watu walio na uwezo wa kujenga maghorofa lengo likiwa ni kupendezesha mji. Hali hiyo inatokana na nyumba nyingi zilizopo katika eneo la Sokomatola kuwa za kizamani na zilizochakaa hali isiyoendana na madhari ya kisasa yaliyopo kwenye kituo cha mikutano cha Mkapa cha halmashauri ya jiji la Mbeya kilichopo maeneo hayo. Lakini Mkuu wa mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro ameshauri halmashauri kuwaruhusu wamiliki wa nyumba katika eneo hilo kufanya maamuzi wao wenyewe kwa kukubaliana na watu walio na uwezo wa kujenga magorofa na si kuwaingilia. “Tumeona mahala kwingi wafanyabiashara au wawekezaji wakubwa wanawafuata watu walio na viwanja na kufanya mazungumzo nao na wanakubaliana vizuri.Wengine wanawajengea nyumba mbali kisha wanawaachia viwanja ama wanakubaliana ikijengwa ghorofa huyu amiliki vyumba kadhaa na mwenzake vinavyobaki”. “Halmashauri isiingilie makazi ya watu.Mnadumaza eneo la Sokomatola.Na mnatudanganya kusema ninyi mtalinunua kasha muuze viwanja upya pesa hamna mtazitoa wapi.” Kandoro pia alishauri halmashauri kufanya mazungumzo na kituo cha utafiti wa kilimo cha Uyole jijini hapa ili ili iweze kupewa eneo la mbele lililo pembezoni mwa barabara ili litumike kwa ujenzi wa makazi badala ya kilimo kama linavyotumika hivi sasa. Alisema ili kuwa na mji wenye mwonekano mzuri ni vema halmashauri ikajipanga na kuhakikisha hakuna vichaka katikati ya mji badala yake iwezeshe wakazi kupata viwanja kwenye maeneo yaliyo wazi na kujenga
MBEYA YETU

MABALOZI WAPYA WAWASILISHA HATI ZAO ZA UTAMBULISHO NCHINI


Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete leo amepokea hati za utambulisho kutoka kwa Mabalozi wa Msumbiji na Indonesia Ikulu jijini Dar es Salaam.Pichani ni Balozi mpya wa Msumbiji nchini Tanzania Dkt.Vicente Mebunia Veloso. 


Balozi Mpya wa Indonesia nchini, Mhe.Zakaria Anshar wakiwasilisha hati zao za utambulisho kwa Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete ikulu jijini Dar es Salaam leo.

INDOMA TOURS ZANZIBAR INAWALETEA MCHEZO WA KIRAFIKI WA KIMATAIFA


Kampuni ya Utalii ya Indoma Tours ya Mjini Zanzibar, inawaleate mchezo mkali wa Kirafiki wa Kimataifa wa Soka, kati ya timu ya Skonda Flota kutoka Barani Ulaya na Timu ya Sale Mdosi Hardware, ya mjini Zanzibar, mchezo utakaochezwa Februari 9, mwaka huu katika Uwanja wa Uzi Football Yard, kuanzia saa 10:00 jioni.

BLACK LEOPARDS KUTOKA AFRIKA YA KUSINI YATUA DAR KUKIPIGA NA YANGA

Kikosi cha  Wachezaji 28 na viongozi 11 wa timu ya Black Leopards ya Afrika Kusini,wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kuwasili mchana wa leo kwa ndege ya shirika la Afrika Kusini, kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, kwa ajili ya mchezo wao wa kirafiki wa kimataifa na Yanga ya Dar es Salaam, mchezo utakaochezwa kesho kwenye Uwanja wa Taifa jijini.
Kikosi cha  Wachezaji 28 na viongozi 11 wa timu ya Black Leopards ya Afrika Kusini,wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya waratibu wa mchezo huos, kutoka kampuni ya Prime Time Promotions Ltd,Pichani kushoto ni Shaffih Dauda, Mmoja wa Wakurugenzi wa Prime Time Promotions Ltd,Godfrey Kusaga,Mtangazaji wa kipindi cha Sports Extra,Mbwiga Mbwiguke,Mdau Juma pamoja na Stuart
 Nahodha wa timu ya  Black Leopards ya Afrika Kusini akizungumza na wanahabari kutoka vyombo mbalimbali mara baada ya kuwasili na kikosi chake kizima leo mchana tayari kwa kupambana na timu ya Yanga Sports Club,kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar.
 Waratibu kutoka Prime Time Promotions Ltd,Shaffih Dauda pamoja na mmoja wa wakurugenzi wa Kampuni hiyo Godfrey Kusaga wakifanya mawasiliano leo mchana mara timu ya  Black Leopards ya Afrika Kusini ilipowasili kwenye uwanja wa  ndege wa Kimataifa wa Mwalimu J.K.Nyerere.
 Shaffih Dauda akiwa ameambatana kocha wa timu ya  Black Leopards ya Afrika Kusini,Abel Makhubele mara baada ya kuwasili leo mchana kwenye uwanja wa  ndege wa Kimataifa wa Mwalimu J.K.Nyerere.
 Wachezaji wa timu ya Black Leopards ya Afrika Kusini,wakiingia kwenye basi kubwa la timu ya Yanga,wayatarajia kumenyana nayo hapo kesho kwenye uwanja wa Taifa,Jijini dar.
Kikosi cha  Wachezaji 28 na viongozi 11 wa timu ya Black Leopards ya Afrika Kusini,wakiwasili mapema leo mchana kwa ndege ya shirika la Afrika Kusini, kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere. Picha zote na JIACHIE