Adverts

Aug 5, 2012

WAZEE WATAKA KIPAUMBELE KWENYE HAMASA YA SENSA

Mratibu wa sensa wilaya ya Mbozi Eliud Mwakibombaki akizungumza kwenye uzinduzi huo

Baashi ya watu waliohudhulia uzinduzi huo

Mzee Mdalavuma akifuatiwa na Mkuu wa wilaya wakiwa meza kuu

Dr Michael Kadeghe Mkuu wa wilaya ya Mbozi akiwahamasisha wananchi kushiriki kwenye zoezi la sensa

Kikundi cha Ngoma cha Ndili miongoni mwa vikundi vilivyoshiriki kwenye zoezi la uzinduzi wa kampeni ya hamasa  ya sensa jioni ya leo uwanja wa kituo cha mabasi cha Mlowo


Na Danny Tweve  

BAADHI YA WAZEE WILAYANI MBOZI WAMEPENDEKEZA KUSHIRIKISHWA WAKATI WA UHAMASISHAJI WA ZOEZI LA  SENSA KUTOKANA NA UKWELI KWAMBA BADO KUNA IMANI  NA MILA POTOFU KWA JAMII WILAYANI HUMO , HASA  INAPOFIKIA HATUA YA KUHESABU WATOTO KUWA NI UCHURO KWA KAYA ZAO.

AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA KAMPENI KWAAJILI YA HAMASA YA SENSA WILAYANI HUMO, MWENYEKITI WA CCM WILAYA MBOZI MZEE ALOYCE MDALAVUMA, AMESEMA NJIA PEKEE NI KWA WAZEE MAARUFU KUTUMIKA HASA MAENEO YA VIJIJINI KATIKA KUTOA UFAFANUZI JUU YA UMUHIMU WA ZOEZI HILO ILI KUPATA MWITIKIO MKUBWA NA KUWEZESHA MAFANIKO YA JUU YA ZOEZI LA SENSA

AMESEMA KWA JAMII YA WANYIHA KUHESABU WATOTO KATIKA HALI YA KAWAIDA HAIKUBALIKI, LAKINI KWAKUWA ZOEZI LA SENSA LINAFAHAMIKA VYEMA UMUHIMU WAKE NI VYEMA WANANCHI NA HASA WAZEE WAKAHAMASISHWA KUSHIRIKI VYEMA KWENYE UHESABUJI  ILI KUWEZESHA UPATIKANAJI WA TAKWIMU SAHIHI

KWA UPANDE WAKE MZEE BENNY MWANG’AMBA AMESEMA KUNA HAJA KWA VIONGOZI WA DINI WILAYANI HUMO KUTUMIA VITABU VITAKATIFU IKIWEMO BIBLIA AMBAPO KUNA ENEO INAZUNGUMZIA MAJIRA AMBAYO YESU ALIZALIWA ULIKUWA WAKATI WA SENSA YA WATU NA KWAMBA NJIA HIZO ZITAWEZESHA WATU KUFUNGUKA NA KUACHA USIRI KWENYE TAARIFA ZA FAMILIA ZAO

MAPEMA KATIKA TAARIFA YAKE MRATIBU WA SENSA WILAYA YA MBOZI BWANA ELIUD MWAKIBOMBAKI AMESEMA WILAYA YA MBOZI IMETEUA JUMLA YA MAKARANI 1471 WATAKAOSIMAMIA MAENEO YA UHESABUJI 230 AMBAPO MIONGONI MWAKE MAKARANI  460 WATAJIELEKEZA KATIKA DODOSO REFU

AMESEMA KATIKA MAANDALIZI YA ZOEZI HILO MAFUNZO YA WAHESABUJI YANATARAJIWA KUANZA JULAI TISA KATIKA VITUO VINNE VYA VWAWA, IGAMBA, ITAKA NA MAHENJE AMBAPO WAKUFUNZI WAMESHATENGWA KWA MAENEO HAYO ILI KUFANYA MAANDALIZI YATAKAYOFANIKISHA ZOEZI HILO
AKIZINDUA ZOEZI HILO KWA KUPIGA KING’ORA MKUU WA WILAYA YA MBOZI DR MICHAEL KADEGHE AMESEMA , PAMOJA NA KUANZISHA MASHINDANO YATAKAYOBEBA UJUMBE WA SENSA KUANZIA NGAZI YA KIJIJI PIA WILAYA IMEJIPANGA KUHAKIKISHA KUWA ZOEZI HILO LINAFANIKIWA NA HASA MAENEO YA VIJIJINI

DK KADEGE AMESEMA KATIKA KUFANIKISHA ZOEZI HILO WILAYA IMESHATUMA TIMU YA UHAMASISHAJI AMBAPO PAMOJA NA MAMBO MENGINE TIMU HIYO INAPOKEA CHANGAMOTO NA MAPENDEKEZO YA KUFANIKISHA ZOEZI HILO KUTOKA KWA VIONGOZI WANGAZI ZA JUU NA WALE WA JAMII ILI HATIMAYE WAKATI WA UTEKELEZAJI ZOEZI HILO LIWEZE KUWA LA MAFANIKIO

Aug 4, 2012

Complete Baby Care Instructions for New Parents Video

: Complete Baby Care teaches new mothers how to care for their baby.

Mbunge wa Monduli(CCM)Atoa Katoni Za Tende na Jozi 100 Za Kanzu Kwa Ajili ya Waislam wa Monduli

Mh
Lowassa akimkabidhi sheikh Simba sehemu ya tende hizo.Wengine pichani
kushoto ni Sheikh wa Mto wa Mbu Sheikh Nasib Idd Nasib Mnyema Kkatibu wa
Bakwata wilaya ya Monduli Idd Idoya na Ustadh Swalehe Ramadhan .
Waziri
Mkuu aliyejiuzulu na Mbunge wa Monduli Mh Edward Lowassa, ametoa
katoni kadhaa za tende pamoja na jozi 100 za kanzu kwa ajili ya Waislam
wa Monduli.Akipokea msaada huo, sheikh wa wilaya ya Monduli Sheikh
 Mwinshehe Mwinyimgeni Salum Simba, alimshukuru mh Lowassa kwa utaratibu
wake huo ambao amekuwa akiufanya kila mfungo wa mwezi mtukufu wa
Ramadhan kwa Waislam wa Monduli.

kutoka swahili villa

KATIBU WA CCM TAWI LA NORTH LONDON NEEMA KUMBA AJITOSA UCHAGUZI UVCCM, TAIFA

 KADA  wa  Chama cha Mapinduzi (CCM) kupitia umoja wa vijana wa CCM
(UVCCM) na Msomi wa  digrii ya uchumi, Neema Kumba
Neema akikabidhiwa fomu jana na Sophia Duma Makao Makuu ya UVCCM jijini Dar es Salaam .
--
DAR ES SALAAM, TANZANIA

KADA  wa  Chama cha Mapinduzi (CCM) kupitia umoja wa vijana wa CCM
(UVCCM) na Msomi wa  digrii ya uchumi, Neema Kumba, amejitosa kwenye
uchaguzi mkuu wa umoja huo Taifa kwa kuchukua kugombea nafasi ya NEC na
uwakilishi UWT.



Akizungumza na waandishi wa habari mapema jana, Agosti 3, jijini Dar es
Salaam, muda mfupi baada ya kukabidhiwa fomu hiyo na Mkuu wa Idara ya
Oganizesheni na siasa UVCCM, Taifa, Sophia Duma,




Kumba ambae awali alikua Katibu wa CCM, tawi la North London, Nchini
Uingereza, alipokua akichukulia digrii yake ya uchumi, alisema lengo ni
kuakikisha mikakati thabiti  inajengeka kwa  kiwango kikubwa miongoni
mwa vjana na wanawake wote nchini.




“Kwa umakini wangu na maarifa niliyoyapata kwenye elimu na uwepo wangu
ndani ya chama, ndani na nje ya nchi, ni wakati sasa na mimi kuwasaidia
wenzangu hasa Vijana na wanawake ambao mara nyingi wamekua wakisahauriwa
 na huu ndio wakati wa kuwainua” alisema Kumba.




Mbali na kuchukua fomu hiyo ya NEC na uwakilishi UWT, Taifa, pia tayari
alisha chukua fomu ya kuwania nafasi ya Mwenyekiti Uvccm, Wilaya Ilala.




Mpaka sasa tayari wanachama mbalimbali wa UVCCM, wamejitokeza kuchukua
fomu za kuwania uongozi ambapo mwisho wa kurudisha fomu hizo, Agosti 6.

Gazeti la NIPASHE: Magufuli amtega Meya wa Arusha hoja ya Lema

Gazet
Hoja ya kukiondoa kituo kikuu cha mabasi katikati ya jiji ambayo ilitumiwa na aliyekuwa Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema (Chadema) kujinadi katika kampeni zake za uchaguzi mkuu ulipita, sasa ametwishwa Meya wa Jiji Gaudence Lyimo (CCM).

Aliyemtwisha zigo hilo ni Waziri wa Ujenzi Dk. John Magufuli na alifanya hivyo wakati akifungua mkutano wa wadau wakuu wa Mfuko wa Bodi ya Barabara uliofanyika jijini hapa juzi.

Magufuli alikuwa akizungumzia mikakati ya kuondoa foleni inayoanza kulinyemelea jiji la Arusha ambapo alisema moja ya ufumbuzi ni kuihamisha stendi hiyo ya mabasi.

“Ni vizuri Meya upo hapa, wekeni mikakati ya kuhamisha ile stendi, hakuna haja ya mabasi yote yanayokuja Arusha lazima yaingie katikati ya jiji,” alisema na kuongeza, “tena katika jiji hili mnaweza kuwa na stendi tatu za mabasi makubwa katika maeneo tofauti kulingana na mahitaji.”

Alitaja maeneo hayo ambayo ni nje ya jiji kuwa ni kwa mabasi yanayotokea barabara ya Moshi, yanayotokea Dodoma na Babati na stendi nyingine ni kwa mabasi yanayotokea barabara ya Namanga.


Hoja ya kuhamisha stendi ilikuwa ni moja ya ajenda katika mikutano ya kujinadi kuwania ubunge wa Arusha Mjini iliyokuwa ikihubiriwa na Lema ambaye pamoja na stendi pia alizungumzia azma yake ya kuhamisha soko kuu lililopo katikati ya jiji.

Hata hivyo, Lema hakufanikiwa kutimiza azma yake baada ya Mahakama Kuu Kanda ya Arusha, kumvua ubunge mapema Aprili, mwaka huu, baada ya mahakama kuridhika kwamba alitumia lugha ya kashfa dhidi ya aliyekuwa mgombea kwa tiketi ya CCM, Dk. Batilda Burian.

Lema amekata rufaa kupinga hukumu hiyo na kesi bado haijapangiwa tarehe ya kusikilizwa.

Katika hatua nyingine Magufuli alisema wizara yake itahakikisha ujenzi wa barabara itakayounganisha kati ya barabara ya Arusha – Babati na Arusha – Namanga inajengwa na kukamilika ili magari yatokayo maeneo ya Babati kwenda Namanga na kinyume chake yasilazimike kupita katikati ya mji.

Alisema hayo wakati akijibu maelezo ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo, ‘aliyemchomekea’ ombi hilo katika maelezo yake ya awali kabla waziri huyo hajafungua mkutano huo.

“Najua Mkuu wa Mkoa Mulongo ‘amenichomekea’ ujenzi wa barabara hii ili kuhakikisha magari yatokayo Babati kwenda Namanga na kurudi yasilazimike kupita mjini ili kupunguza foleni…nasema wizara itasaidia ujenzi huo ili ikamilike,” alisema.

Chanzo Nipashe

Aug 2, 2012

KULIPIA FIRE SASA TRA


Kuna taarifa ambayo ilitolewa na imetangazwa kwenye vyombo vya habari kuhusu ulipaji wa kodi ya FIRE na ROAD LICENCE,tangazo hilo linawataarifu wamiliki wote wa vyombo vya moto wanapokwenda kulipia kodi yao ya mwaka ya Road Licence watakakiwa pia kulipia na kodi ya FIRE ambayo mwanzoni haikua inalipiwa hapo TRA 

  KUANZIA JULY 2012 HUDUMA ZA FIRE ZITAKUWA ZINALIPIWA TRA WAKATI WA KU-RENEW NA BEI NI;
CC 1 - CC 500 10,000/=

CC 501 - CC 1500 20,000/=

CC 1501 - CC 2500 30,000/=

CC 2501 na kuendelea 40,000/=

BARAZA LA MADIWANI MBOZI KUKETI IJUMAAM

Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya  wilaya ya Mbozi Levison Chilewa akizungumza wiki iliyopita baada ya baraza hilo kuahirishwa

Waheshimiwa madiwani wakiwa ukumbini kabla ya baraza la wiki iliyopita kuahirishwa

Katibu Tawala Mkoa wa Mbeya Bi Mtunguja akisikiliza maelezo ya Mkuu wa mkoa, anayemfuatia ni Mbunge wa Mbozi mashariki Mh Zambi

Mkuu wa mkoa wa Mbeya Kandoro akiwanyoshea vidole madiwani katika moja ya maeneo aliyoyasisitiza kuhusiana na kujibu hoja za mkaguzi na mdhibiti wa hesabu za serikali

Aug 1, 2012

ASKARI TRAFIKI AFARIKI KATIKA AJALI YA ROLI JIONI HII

 ASKARI POLISI WA KIKOSI CHA USALAMA BARABARANI ANAYEFAHAMIKA KWA JINA LA JOSEPH AMEFARIKI DUNIA KWENYE AJALI YA ROLI ILIYOTOKEA JIONI HII KATIKA ENEO LA SENJELE WILAYANI MBOZI BAADA YA GARI HILO KUHARIBIKA MFUMO WA BREKI LIKIWA MTELELEMKONI NA KUMLAZIMU DEREVA WA GARI HILO KURUKA

INAELEZWA KUWA ASKARI HUYO ALIKUWA AMEOMBA LIFT KWENDA MJINI MBEYA AKITOKEA KITUO CHAKE CHA KAZI ENEO LA MLOWO WILAYANI MBOZI AMBAPO AKIWA NJIANI NDIPO AKAKUMBWA NA MASAIBU HAYO



PICHA ZOTE NA INDABA BLOG

Jul 30, 2012

WANAFUNZI WAANDAMANA KWENDA OFISI ZA MKUU WA WILAYA KUDAI HAKI YA KUFUNDISHWA

Mgomo wa walimu ulioanza leo, umeanza kuota matawi baada ya wanafunzi wa shule za msingi katika mji mdogo wa Vwawa na Tunduma katika wilaya ya Mbozi kuandamana huku kukiripotiwa kutokea uhalibifu wa mali katika mji wa Tunduma.
katika mji wa Vwawa wanafunzi wa shule ya msingi ya Ichenjezya waliandamana majira ya saa tatu hadi kwenye ofisi za mkuu wa wilaya mbozi wakitaka kuonana na mkuu huyo wa wilaya ili wapate haki yao ya kufundishwa aambayo wanadai wameikosa siku ya leo kwa mgomo wa walimu.

wakizungumza mbele ya mkuu wa kituo cha polisi cha Mbozi, wanafunzi hao wamesema hawaondoki mpaka waelezwe namna watakavyopata huduma ya kusomeshwa, hata hivyo baada ya mbinu za hapa na pale watoto hao walilainika na kuondoka kuelekea shuleni kwao ili yakazungumzwe huko.\

Mbinu ya polisi kwa kushirikiana na idara zingine za serikali iliwezesha watoto hao kutoka kwa staili ya mchaka mchaka na kurejea shuleni kwao, na dadkika chache baadaye kundi jingine la wanafunzi kutoka shule ya msingi ya Haloli lilitia timu mbele ya geti la halmashauri ya wilaya ya Mbozi kutaka kumwona afisa elimu.
Hapa napo ikawa kazi kutengeneza maneno ya kuwafurahisha, ambapo baada ya zuga zuga ya muda mrefu hatmaye watoto hao walilegea na kuondoka,
 MLINZI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA MBOZI AKIJARIBU KUWATULIZA WANAFUNZI HUKU AKIFUNGA LANGO KUU LA KUINGIA HALMASHAURI YA WILAYA MMBOZI
Huko Tunduma taarifa zinaaeleza kuwa uhalibifu wa mali na majengo ya serikali umetokea katika ofisi za mamlaka ya mji wa Tunduma ambapo gari jipya limevunjwa vioo na vifaa kama kompyuta na laptops vimeibiwa katika ofisi za mamlaka hiyo

Jul 28, 2012

JK AFUNGUA KONGAMANO LA CHINA NA AFRIKA



Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika mazungumzo rasmi na Waziri wa China anayeshughulikia Umaskini Mhe Fan Xiaojian, jijini Dar es Salaam Jumamosi Julai 28, 2012.  Kongamano la tatu la Jukwaa la Uhusiano wa China na Bara la Afrika katika kuondoa umaskini katika hoteli ya White Sands jijini Dar es salaam leo July 28, 2012.

(PICHA ZOTE NA IKULU)




Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimsikiliza  Waziri wa China anayeshughulikia Umaskini Mhe Fan Xiaojian(kuhsoto) na  Balozi wa China hapa nchini Mhe L.V. Youqing. baada ya  akifungua Kongamano la tatu la Jukwaa la Uhusiano wa China na Bara la Afrika katika kuondoa umaskini katika hoteli ya White Sands jijini Dar es salaam leo July 28, 2012.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifungua Kongamano la tatu la Jukwaa la Uhusiano wa Chinana Bara la Afrika katika kuondoa umaskini katika hoteliya White Sandsjijini Dar es salaamleo July 28, 2012