Adverts

Jun 22, 2011

KIATU CHA WANAWAKE CHA HARUSI

Kiatu hiki kinaitwa Gorgeous  kwaajili ya shughuli za harusi mwaka 2012

JAMANI KWA WANAOTARAJIA KUOA HII NDIYO SUTI YA 2011 HADI 2012

Suti ya harusi kwa mwaka 2011 hadi 2012 ni Single Button  koti lake hivyo zingatieni hilo siyo unakuja na suti zako za miaka ileeee, hii ni kwa wenye vijihela tu manake sisi tunaoishi na mifugo yetu hapana tutashona tunazomudu!!

LIBENEKE LA MY AFRICAJOBS KWA WANAOSAKA KAZI

www.MyAfricaJobs.com

OFISI YA BUNGE YATOA TAARIFA JUU YA HABARI ILIYOCHAPISHWA NA GAZETI LA DIRA YA MTANZANIA…

YAH: TAARIFA POTOFU YA GAZETI LA DIRA YA MTANZANIA TOLEO LA JUMATATU, 20 – 26 JUNI, 2011 ‘ SAKATA LA POSHO ZA WABUNGE’ SPIKA MAKINDA MBUMBUMBU ‘Utafiti wabaini anasimamia asichokijua magwiji wa Bunge washangaa tamko lake’.

1.0UTANGULIZI

Pamoja na Vichwa vya habari hiyo, Katika taarifa hiyo Mwandishi wa gazeti hilo amedai kuwa;
i.Spika wa Bunge, Anne Makinda hana uelewa wa kutosha wa jinsi mbunge anavyoweza kupoteza wadhifa wake
ii.Pia Spika wa Bunge haelewi mfumo wa malipo ya Posho za Wabunge
iii.Spika hana mamlaka ya kumfukuza Mbunge yeyote anayekataa kusaini Fomu za kuchukua posho ya kikao.

2.0MAJIBU YA HOJA POTOFU ZILIZOTOLEWA
Ofisi ya Bunge ingependa kuwaarifu wananchi kwamba habari hiyo iliyoandikwa na gazeti la Dira ya Mtanzania ni ya dharau na haina ukweli wowote na imeandikwa kwa nia mbaya ya uchochezi na kuharibu sifa aliyonayo Mhe. Spika Bungeni na kwa watanzania kwa ujumla.
Ili kuondoa upotofu wa taarifa iliyotolewa na gazeti hili, Ofisi ya Bunge ingependa kutoa ufafanuzi wa hoja zilizotolewa kama ifuatavyo;

i. Sio kweli kwamba Mhe. Anne Makinda hana uelewa kuhusu uendeshaji wa shughuli za Bunge. Mhe. Makinda amekuwa mbunge kwa zaidi ya miaka 30 Bungeni na kwa kipindi hicho chote ameshika nyadhifa mbalimbali Bungeni na Serikalini. Aidha akiwa Naibu Spika ameongoza kamati ya Bunge iliyoshiriki marekebisho ya Kanuni za Kudumu za Bunge toleo la 2007.

Kwa mantiki hiyo anazifahamu vyema Kanuni za Bunge na ana uzoefu na uendeshaji wa shughuli za Bunge kwa muda mrefu kuliko hata idadi kubwa ya wabunge wapya waliopo Bungeni. Katika utendaji wake, hafanyi kazi kwa kuvutwa na hisia bali husimamia uendeshaji wa Bunge kwa Mujibu wa Kanuni za Bunge ambazo tunashaka hata kama mwandishi wa gazeti hili anazifahamu vyema.
Ni kwa kuzingatia hilo aliwaeleza bayana Waandishi wa habari siku alipofanya nao mahojiano ambapo mwandishi wa gazeti hili pia hakuwepo, kuwa taratibu la kuchukua posho kwa Mbunge huenda sanjali na kusaini mahudhurio Bungeni (Mbunge anayehudhuria Bunge ndiye anayelipwa posho), kwa maana huwezi kumlipa posho Mbunge asiyekuwepo Bungeni. Mahudhurio ya Mbunge ni pale anaposaini fomu ya Mahudhurio. Kwa mantiki hii, kanuni zinamtaka bayana kila mbunge kuhudhuria vikao vya Bunge.

Kanuni ya 143 inatamka kuwa:
(1) kuhudhuria vikao vya Bunge na kamati ni wajibu wa kwanza wa kila mbunge.
(2) Mbunge yeyote atakaeshindwa kuhudhuria mikutano ya Bunge mitatu mfululizo bila ruhusa ya Spika iliyotolewa kwa maandishi, atapoteza Ubunge wake kwa mujibu wa ibara ya 71 (1) ya katiba na Spika ataiarifu Tume ya Uchaguzi.

(3) Mbunge atakapokosa kuhudhuria nusu ya vikao vya Mkutano mmoja bila ya sababu ya msingi atapewa onyo.

Hivyo basi kwa mantiki hiyo, Mbunge atakayeshindwa kusaini fomu za mahudhurio kwa mtiririko huo hapo juu atakuwa amepoteza sifa zake za kuwa Mbunge kwa mujibu wa Kanuni.
ii. Aidha ni kwa uvivu wa kufikiri au kwa makusudi kabisa, mwandishi wa gazeti hili ameandika yale aliyohisi ni sahihi na kufanya utafiti katika kiwango ambacho hajaeleza ni kwa kutumia vigezo gani bila hata kujaribu kuuliza misingi halisi aliyoizungumzia Mhe. Spika kuhusu uhalali wa mahudhurio ya Mbunge sanjali na ulipwaji wake posho awapo kazini.

Hivyo madai ya kuwa Spika hana madaraka ya kumfukuza Mbunge Bungeni hayana mantiki na wala madaraka ya Spika kuhusu kumfukuza Mbunge hayakuwa sehemu ya mahojiano na waandishi na Spika wa Bunge kama anavyodai, na Kanuni zimeeleza bayana kazi za Spika Bungeni. Kumbuka madaraka ya Spika, wajibu wa Wabunge na hata Miongozo mingine Bungeni huratibiwa kwa mujibu wa kanuni za Kudumu za Bunge.

Hatujui lengo la mwandishi ni lipi hasa kwa kuweza kutoa taarifa zenye upotoshaji mkubwa kwa umma na zenye kuleta dharau kwa kiongozi wa Bunge na Bunge kwa ujumla kwa kuzingatia kuwa kiongozi huyu amechaguliwa na Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano.

3.0 HITIMISHO
Ofisi ya Bunge inapenda kuwaarifu wanahabari wote kuwa Idara yake ya Habari imekuwa ikitoa ushirikiano wa kutosha kuwaarifu waandishi kwa taarifa zozote wanazohitaji na inasikitishwa kwa kiasi kikubwa na uandishi unaojali hisia na wenye kulenga uchochezi badala ya kuelemisha.
Licha ya mwandishi wa habari hii kutokuwepo Dodoma na wala hakushiriki mahojiano hayo na Mhe. Spika, habari husika iliyoandikwa imelenga kutoa taarifa potofu bila kushirikisha hata upande wa pili kwa ufafanuzi. Kwa kuzingatia hilo Ofisi ya Bunge inamtaka Mhariri wa Gazeti la Dira ya Mtanzania kuomba radhi kwa uzito ule ule waliotoa habari yao ya kupotosha umma.

Deogratios Egidio
Kny: KATIBU WA BUNGE
21 Juni, 2011

ELIMU YA KILIMO INAENDELEA> KANUNI ZA KILIMO BORA


TUENDELEE KUWASAIDIA WATU WENYE ULEMAVU HASA HUKU VIJIJINI AMBAKO MISAADA NI NADRA!

Tumezoea kuona taasisi, mifuko ya kijamiina mashirika mbalimbali na hata watu wenye huruma wakiongoza na kamera za wandishi kwenda kutoa misaada hasa mijini na Dar es salaam ni mfano wa mambo haya, lakini ni mara chache kusikitia watu hao hao wakielekeza misaada yao kwenye maeneo ya vijijini kama Kigala huko makete, Chitete huko Mbozi na Nguliko huko Ileje! sasa hii ni changamoto kwenu tuone wote hawa ni viumbe wa mungu tuwasaidie ili nao waafaidi matunda ya nchi yetu.

HII NDIYO RAMANI YA WILAYA YA MBOZI


Francis Godwin ni mzee wa matukio daima: WAJUMBE WA MCT NA UCHAGUZI

Zoezi la uchaguzi wa wajumbe wa baraza la habari Tanzania (MCT) linaanza sasa huku mwenyekiti wa muda wa uchaguzi huu Beny Mwaipaja ..."

Francis Godwin ni mzee wa matukio daima: BREAKING NEWS....NI JAJI KISANGA NA RAIS WA UTPC ...

"Jaji Kisanga Rais wa MCT Keneth Simbaya mjumbe wa bodi Rais wa bodi ya MCT aliyemaliza muda wake jaji Robert Kisanga amepita kwa kishin..."

GARI MADE IN TANZANIA

"Gari jipya aina ya Nyumbu lililotengenezwa na Kampuni ya Mzinga ya JWTZ, likioneshwa jana kwenye maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma y..."