Adverts

Oct 25, 2012

big4regions: STACO LTD GOWDON CLOSED TODAY AFTER ALLEGATION OF ...

big4regions: STACO LTD GOWDON CLOSED TODAY AFTER ALLEGATION OF ...: STACO LTD a  agency company selling fertilizers in Mbozi District, has closed today by officials from ministry of Agriculture who accompanie...

Oct 16, 2012

UCHAGUZI WA CCM MBEYA, ZAMBI AULA

Mmoja wa wapiga kura akiwa anatumbukiza kura yake kwenye kapu la uchaguzi


ELIMU YA KUJIKINGA NA MAAMBUKIZI YA UKIMWI KWA WAJENZI WA BARABARA TUNDUMA- SUMBAWANGA

Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya waelimisha rika kwenye eneo la ujenzi wa barabara ya Tunduma -Sumbawanga wakiwa kwenye picha ya pamoja katika shule ya JK Nyerere

Oct 12, 2012

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje akutana na Balozi wa India


Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirkiano wa Kimataifa, Mhe. Mahadhi Juma Maalim (Mb.) (kulia) akisalimiana na Balozi wa India hapa nchini, Mhe. Debnath Shaw aliyefika ofisini kwa Mhe. Naibu Waziri kwa lengo la kujitambulisha ambapo pia walizungumzia masuala mbalimbali ya ushirikiano baina ya nchi hizi mbili.
Mhe. Naibu Waziri (kushoto) akizungumza masuala mbalimbali na Mhe. Balozi Shaw wakati Balozi huyo alipofika ofisini kwake kwa lengo la kujitambulisha.
Mhe. Balozi Shaw (kushoto) akizungumza  huku  Mhe. Naibu Waziri akimsikiliza kwa makini.
Mhe. Balozi Shaw akisaini Kitabu cha Wageni mara baada ya kuwasili ofisini kwa Mhe. Naibu Waziri.
Mhe. Naibu Waziri akiendelea na mazungumzo na Mhe. Balozi Shaw. Wengine katika picha ni Bw. Charles Faini (kushoto kwa Mhe. Naibu Waziri), Afisa Mambo ya Nje na Bw. D.K. Pant (kulia kwa Mhe. Balozi) Afisa kutoka Ubalozi wa India hapa nchini.
KUTOKA BLOG YA MTAA KWA MTAA

ABBAS KANDORO AONYA WATAALAMU WA KILIMO KUFANYA KAZI KWA MAZOEA


MKUU wa Mkoa wa Mbeya Bw.Abbas Kandoro amewaonya wataalamu wa kilimo kuacha kufanya kazi kwa mazoea kwa kukaa maofisini badala ya kwenda mashambani waliko wakulima na ili waweze kusaidiana wakulima kujua mbinu za bora za kuboresha mazao yao kuliko kuendelea kufanya kazi za kilimo bila wataalamu kilimo kuwepo .

Mwandishi wetu Esther Macha anaripoti kutoka Mbeya kuwa Bw. Kandsoro alisema wataalamu wa kilimo wanapaswa kuwa karibu na wakulima wao waliopo vijijini kuliko mazoea yaliyojengeka miongonbi mwao yao ya kukaa maofisini kusubiri taarifa za kilimo wakati taaluma yao inawataka kufika mashambani waliko wakulima wenyewe.

 Mkuu huyo wa Mkoa aliyasema hayo baada ya kupewa taarifa ya idara ya kilimo ya halmashauri ya wilaya ya Mbeya alipofanya ziara na ndipo akakutana na madudu kama aliyosikia kwenye tarifa ya wilaya ya Mbozi na kuikataa.

 Alisema hatua iliyopo kwa wataalamu kutokuwa karibu na wakulima ndiyo chanzo kikubwa cha wachuuzi kupata fursa ya kwenda majumbani kwa wakulima na kununua mazo kisha wanaondoka nayo pasipo hata kulipa ushuru.


Bw. Kandoro alisema madudu hayo ni pamoja na kuwepo kwa takwimu zinazoonyesha taarifa za makadirio ya mavuno ya nafaka hali iliyoashiria mavuno bado yanaendelea ama hayajafanyika wakati umekwisha hivyo kulipaswa kuwepo takwimu sahihi na si matarajio tena.

“Ndugu zangu hatuwezi kwenda katika utaratibu kama huu haiwezekani kabisa.Unasema shughuli zinaendelea! Wapi wanaendelea kuvuna mpaka leo hii?.Hivi unajua tayari tuko katika msimu mwingine wa kilimo?” alihoji Bw.Kandoro.

“Kwa nini mnafanya kazi ya kukokotoa takwimu mkiwa maofisini?Na hili nimeliona mahala pengi eneo la kilimo lin a ubabaishaji mkubwa.Mabwanashamba wapo lakini kila kukicha wanacheza na takwimu maofisini.Vijijini waliko wakulima hawaonekani”


Alisisitiza kuwa  utaratibu maalumu wa ukusanyaji takwimu zinazohusiana na kilimo ikiwemo kupeleka maaofisa takwimu katika magulio ili waweze kujua ni kiasi gani cha mazao kinauzwa.

KUTOKA FRANCIS GODWIN BLOG

UCHAGUZI WA CHAMA CHA SOKA MKOA WA MBEYA, MKWE KIONGOZI ANYANYULIWA NJE




Na francisgodwin.blogspot.com

USAILI wa wagombea wanaowania nafasi  mbalimbali  za uongozi  katika chama cha soka  mkoa wa Mbeya, (MREFA), jana uligubikwa na vituko vya aina yake,  baada ya mmoja wa wagombea wa nafasi ya Uenyekiti,  kumkataa mjumbe wa kamati ya uchaguzi kwa madai kuwa ana mgongano wa kimasilahi na mpinzani wake.

Mjumbe wa Kamati ya uchaguzi aliyekataliwa na kulazimika kutolewa ndani ya chumba cha usaili ili haki itendeke kwa mgombea ni Katibu, Prince Mwaihojo, ambaye anadaiwa kuwa ni Mkwe wa mgombea mmoja wa nafasi ya Uenyekiti John Mwamwaja.

Mtandao  huu umeshuhudia katibu huyo wa Kamati ya uchaguzi, akitoka nje muda mfupi tu baada ya mmoja wa wagombea ya nafasi ya uenyekiti Elias Mwanjala, alipoitwa ndani ya chumba cha usaili.

Alisema kuwa haiwezekani mimi nihojiwe na mtu ambaye anamafungamano ya kidamu na mpinzani wangu, ndio maana nilipofika ndani ya chumba cha usaili nilitoa angalizo na nashukuru Mwenyekiti alielewa na kukubali kumtoa nje.

Kwa upande wake, Mwaihojo alipoulizwa juu ya sakata hilo la kukataliwa,  alikiri kuwa lilitokea na si la ajabu katika mahala popote ambapo haki inaafutwa, hivyo kitendo hicho hakizuii mchakato wa kuwapata viongozi wa chama hicho.

Akitoa taarifa ya mchakato wa zoezi hilo baada ya kumalizika, Mwaihojo alisema zoezi hilo la usaili kwa limefanikiwa kwa asilimia 90 kwa kuwa wagombea 14 walifanyiwa usaili na kubakiza wagombea wanne tu ambao watamalizia hawakufanyiwa.

Kwa mujibu wa Mwaihojo, wagombea wanne ambao hawajafanyiwa usali ni Katibu anayemaliza muda wake Lawrence Mwakitalu, Andongwisye Panja, Thomas Kasombwe Sinkwembe ambao wote walitoa udhulu kutokana na kukabiliwa na shughuli mbalimbali ikiwemo kusimamia mitihani ya kidato cha nne inayoendelea hivi sasa.

Uchaguzi wa MREFA unatarajia kufanyika oktoba 27, jambo litakalowezesha kupatikana kwa uongozi mpya utakaohudumu kwa miaka mine kama katiba ya chama hicho inavyoeleza.

 Amewataja watu waliojitokeza kuomba nafasi za uongozi  kwa nafasi ya Mwenyekiti kuwa ni John Mwamwaja ambaye ni makamu Mwenyekiti wa uongozi unaomaliza muda wake, wakati wengine ni Majuto Mbuguyo aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji katika Halmashauri ya Wilaya ya Tanga, pamoja na Elias Mwanjal ambaye katika uchaguzi Mkuu uliopita aligombea ubunge katika jimbo la Kyela na kuangushwa vibaya na mbunge wa sasa Dk. Harrison Mwakyembe, ambaye pia ni Waziri wa Uchukuzi.


Makamu Mwenyekiti ni  Omary Mahinya, wakati nafasi ya Katibu Mkuu, Lawrence Mwakitalu, anayemaliza muda wake,Suleiman Haroub na Redson Kaisi, ambapo Katibu Msaidizi ni William Mwamlima na nafasi ya Mkutano Mkuu wa Taifa Tahdeo Kalua na Danny Korosso.

Kwa upande mweka Hazina ni Asajile Kavenga, Uswege Luhanga, wakati wajumbe wa kamati ya utendaji ni Lwitiko Mwamndela, Thomas Kasombwe, Boniface Sinkwembe.
Mwisho.

UTAPELI WA KUTUMIA MAJINA YA VIONGOZI KWENYE M-PESA WAWAUMIZA WANANCHI

Wizi mpya ulioanza hivi sasa kwenye mifumo ya fedha ya kielektronikia ikiwemo MPESA, umewaliza wananchi wengi wilayani Mbozi ambapo jana jioni mmoja wa viongozi wa chama cha walimu alilizwa kiasi cha zaidi ya Milion Moja imefahamika.
Akizungumza wakati akifuatilia kwenye kituo kimojawapo kinachotoa huduma za MPESA katika mji wa Vwawa, kiongozi huyo wa kike alifikwa na tukio hilo baada ya kupigiwa simu na mtu aliyejitambulisha kuwa ni George Lubeleje ambaye ni Mbuge wa jimbo mojawapo la mkoa wa DODOMA akimtaka amsaidie kiasi cha shilingi 600,000 za mafuta wameishiwa wakiwa mikumi wakisafirisha maiti kwenda sumbawanga.
Inaelezwa kuwa kwakuwa anamfahamu, aliomba pia mwenyeji huyo amfanyie booking ya hoteli katika mji wa Vwawa ili ujumbe huo uweze kupumzika angalau usiku mmoja kabla ya kuendelea na safari ya kupeleka maiti Sumbawanga.
Mama huyo alifanya haraka kutoa fedha benki na kuzituma kwenye simu ya mheshimiwa huyo akijua ndiye Lubeleje halisi, na baada ya kutuma fedha hizo ripoti ya fedha kutumwa kwa njia ya MPesa ilionyesha kuwa jina ambalo fedha zimepokelewa ni George Lubeleje.
Hata hivyo dakika chache baada ya fedha kuingia kwenye simu hiyo, inaelezwa kuwa mh huyo feki alipiga simu tena kwa mwalimu huyo na kumweleza kuwa zimeingia lakini bahati mbaya tangu asajiri simu yake hajawahi kutumia huduma ya mpesa, hivyo alimwomba awapigie voda ili wazirejeshe fedha hizo na badala yake atumie simu ya dereva wake ambaye ana uzoefu wa kutumia huduma hizo za Mpesa.
Mwanamke huyo alisisitizwa kuwa angekopa mahala popote ili waweze kuondoka pale walipo waendelee na safari wakati yeye akiendelea kushughulikia kurejesha fedha hizo kutoka Vodacom, hata hivyo baada ya kutuma fedha hizo mara ya pili alienda kufuatilia kwenye kituo cha kutolea fedha lakini ikabainika kuwa fedha za awali zimechukuliwa.
Licha ya kuwasiliana na kampuni ya vodacom, majibu ya mtoa huduma hayakuonyesha kutii kiu ya mama huyo na kuamua kwenda kituo cha polisi cha Vwawa ili kutoa taarifa kuwezesha uchunguzi kufanyika kwakuwa inaonyesha kuwa mtandao huo umeingia kwa kasi wilayani mbozi na tayari watu wengi wamelizwa kutokana na aina hiyo ya utapeli.
Watu wanajiuliza imekuwaje watu wajisajiri kwa majina ya viongozi na mawaziri na makampuni ya simu yameendelea kukaa kimya bila kufuatilia taarifa za usajiri zinazofanywa hivi sasa na mawakala maarufu kama freelancers na kudanganywa na matapeli kutokana na uelewa mdogo walio nao baadhi yao.

Oct 8, 2012

MPISHI MAARUFU KUTOKA INDIA ATIA TIMU BONGO NA KUTOA SOMO

Mpishi maarufu Duniani kutoka nchini India Sanjeev  Kapoor (kulia) akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam jinsi vyakula vya asili vinavyoweza kuwavutia watalii kwenda kutembelea nchi mbalimbali na hivyo kukuza utalii wa nchi husika huku Mkurugenzi Mwendeshaji wa Bodi ya Utalii Nchini Dkt. Aloyce Nzuki akimsikilia kwa makini. Mpishi Kapoor amekuja nchini kwa ajili ya kuandaa vipindi vya runinga ambavyo vitahusu mapishi ya vyakula vya  asili ili kutangaza utalii wa kiutamaduni nchini India.


Mpishi maarufu Duniani kutoka nchini India Sanjeev  Kapoor (kulia) akimkabidhi Mkurugenzi Mwendeshaji wa Bodi ya Utalii Nchini Dkt. Aloyce Nzuki leo jijini Dar es Salaam kitabu kinachoonyesha aina mbalimbali za mapishi alizoziandaa katika kipindi cha mapishi kijulikanacho kama Khana Khazana kinachorushwa na Televisheni ya Taifa ya India.  Mpishi Kapoor atakuwepo nchini kwa muda wa wiki mbili kwa ajili ya kuandaa vipindi vya runinga ambavyo vitahusu mapishi ya vyakula vya  asili ili kutangaza utalii wa kiutamaduni nchini India. 

Mkurugenzi Mwendeshaji wa Bodi ya Utalii Nchini Dkt. Aloyce Nzuki akiwaonyesha waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam kitabu alichopewa na mpishi maarufu Duniani kutoka nchini India Sanjeev  Kapoor  kinachoonyesha aina mbalimbali za mapishi alizoziandaa katika kipindi cha mapishi kijulikanacho kama Khana Khazana kinachorushwa na Televisheni ya Taifa ya India. Mpishi Kapoor atakuwepo nchini kwa muda wa wiki mbili kwa ajili ya kuandaa vipindi vya runinga ambavyo vitahusu mapishi ya vyakula vya  asili ili kutangaza utalii wa kiutamaduni nchini India. 


Mkurugenzi Mwendeshaji wa Bodi ya Utalii Nchini Dkt. Aloyce Nzuki (kushoto) akimkaribisha mpishi maarufu Duniani kutoka nchini India Sanjeev  Kapoor ili aweze kuongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es salaam ili aweze kuongea nao kuhusu umuhimu wa vyakula vya asili katika sekta ya utalii wa utamaduni. Kulia ni Naibu Meneja Mkuu wa Hoteli ya Serena Daniel Sambai ambayo imegharamia gharama za  chakula na maladhi kwa mpishi huyo kwa kipindi chote  atakachokuwepo nchini. 
Picha na Anna Nkinda - Maelezo

SHIMIWI IKULU SPORTS YAWIKA NA KUTWAA VIKOMBE KIBAO



Mgeni Rasmi Katibu Mkuu Ikulu Bw Peter Ilomo Akikagua timu ya Ikulu sports club ya kamba wanaume aliyemwakilisha Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue kwenye kilele cha mashindano ya Shimiwi mkoani Morogoro jumamosi tarehe 6.10 2012.
Timu ya Netball ya Ikulu sports club wakiwa kwenye picha ya pamoja na Viongozi wao kabla ya fainali na timu ya Wizara ya Afya Ikulu sports club ilishida kwa magoli 50- 25 kuwa washindi wa kwanza.
Wachezaji wa Ikulu sports club na Wafanyakazi wenzao ambao walienda kushangilia timu yao wakifurahia baada ya kushinda na kupata vikombe vitano kwenye michezo ya Mpira wa pete, kamba wanaume, kamba wanawake, kuendesha baiskeli, na mshindi wa pili Riadha.
Ikulu sports club Kamba wanaume wakifurahia kikombe baada ya kukabidhiwa na mgeni rasmi.
Ikulu sports club yaongoza Yapata vikombe vitano kwenye mashindano ya Wizara na Taasisi za serikali (SHIMIWI) Mashidano hayo yalifanyika Mkoani Morogoro na kufungwa na Katibu Mkuu Ikulu Bw Peter Ilomo. 
KUTOKA MICHUZI BLOG

Tuzo za Uandishi wa Habarai za Utalii wa Ndani na Uhifadhi yaanzishwa na TANAPA



Meneja Uhusiano wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Bw. Pascal Shelutete akiongea na wanahabari mjini Arusha mwishoni mwa wiki ambapo aliatangaza kuanzishwa kwa Tuzo za Uandishi wa Habarai za Utalii wa Ndani na Uhifadhi ambapo kuanzia mwaka huu amesema TANAPA itakuwa ikikitambua, kutahmini na kutoa tuzo kwa waandishi watakaoandika habari zitakazohamasisha Utalii wa Ndani na Uhifadhi katika HIFADHI ZA TAIFA. Namna ya kuingia kwenye shindano hilo 
HABARI ZAIDI NENDA KWENYE BLOG YA MUHIDIN MICHUZI