Adverts

Jul 9, 2013

MBOZI YAKABILIWA NA CHANGAMOTO KATIKA SEKTA ZA ELIMU NA AFYA



Na Angela kivavala
Halmashauri ya wilaya Mbozi ina kabiliwa na tatizo la ukosefu wa shule za sekondari za kidato cha tano na sita.

Wilaya ina jumla ya shule za sekondari 55 ambazo kati ya hizo 40 ni za serikali na 15 ni za binafsi.kati ya shule hizo ni sita tu zenye elimu ya kidato cha tano na sita ambapo ya serikali ni moja nane za watu binafsi.

Kutokana na hali hiyo watoto wanaohitimu kidato cha nne wanalazimika kwenda nje ya wilaya ya Mbozi hususani  katika jiji la Mbeya kujiunga na kidato cha tano hali ambayo inawaingiza kwenye gharama kubwa wazazi wao

Aidha changamoto nyngine ni kasi ya ongezeko la watu ambapo ni matokeo ya kuzaliana kwa kasi ambapo kulingana na takwimu za sensa ya mwaka 2012, Mbozi ina jumla ya wakazi 446,339  na kati yake 55% wakiwa ni vijana na watoto.

Kwa mwaka wa fedha  2012/2013 hadi kufikia  Januari, 2013 jumla ya vyumba vya madarasa 11 vilijengwa katika shule 4 zilizopo Wilayani Mbozi na  vyumba vyote vilikuwa vimekamilika na kupokea wanafunzi 398 waliofaulu ambayo ni sawa na asilimia 100 ya wanafunzi waliokuwa wamekosa nafasi. 
 
Wilaya ina shule za msingi 160 ambazo kati ya hizo 158 sawa na 99% zinamilikiwa na Serikali na shule mbili (2) ni za watu binafsi.  Shule hizo zina jumla ya wanafunzi 93,516, ambao 45,789 sawa na 49% ni wavulana na 47,727 sawa na 51% ni wasichana.  Aidha shule hizo zina jumla ya walimu 2,000

 Changamoto zinazo ikumba sekta hii ya elimu ni pamoja  na upungufu wa walimu 464 kati ya mahitaji ya walimu 2,564 na kuwa na shule moja tu yenye kidato cha tano na sita ya serikali na shule moja ya binafsi. 
Kwa upande wa Sera ya Afya ya Tanzania inataka kila kijiji kuwa na zahanati.  Wananchi wamejenga zahanati 20 ambazo zipo hatua mbali mbali za ujenzi na 3 zimekamilika na zimeanza kutumika mwezi Januari 2013.

  Hivyo, jumla ya vijiji vyenye zahati hadi sasa ni 72 kati ya vijiji 101 vilivyopo katika Wilaya ya Mbozi ifikapo 2015 takribani vijiji 82 vitakuwa na zahanati. 

Kulingana na taarifa iliyotolewa kwenye maadhimisho ya serikali za mitaa  wilayani humo ,Sekta ya afya ina changamoto ya upungufu wa wafanyakazi na vitendeakazi  vikiwemo vifaa tiba pamoja na watoa huduma kwa ujumla.

Hayo yalisemwa katika taarifa ya utendaji ya halmashauri ya wilaya ya Mbozi kwa wananchi wa wilaya ya Mbozi katika  maadhimisho ya siku ya selikari za mitaa  yakiwa na lengo la kutoa mwanya kwa jamii kutambua na kuzifahamu shughuli za huduma mbali mbali zinatolewa na Taasisi za Serikali za Mitaa yaani Halmashauri Majiji, Manispaa na za wilaya.
Mafanikio hayo yametokana na Kuhamasisha na kuhimiza wananchi kushiriki kikamilifu katika ujenzi wa madarasa, ushiriki wao ulitoa mchango mkubwa katika kufanikisha zoezi hiliMshikamano wa viongozi wakuu wa Serikali na halmashauri katika wilaya kufuatilia, kusimamia na hususani waheshimiwa madiwani.

Jul 5, 2013

KILIMO CHA MAZAO YA CHAKULA CHA SISITIZWA


Na  Angela Kivavala dsj

Wana nchi wa wilayani mbozi wameshauliwa kujijengea utamaduni wakuhifadhi akiba ya chakula kwenye kaya zao ili kuziwezesha kaya zao kuwa na chakula cha hakiba kwa msimu

Hayo yalisemwa katika maadhimisho ya siku ya selikali za mitaa yaliyofanyika katika wilaya ya mbozi kata ya igamba kijiji cha hatelele  yaliyo kuwa na kaulimbiu isemayo amani uadilifu na uwajibikaji ninyenzo muhimu katika mchakato wa katiba mpya na ustawi wa serikali za mitaa.

Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo alikuwa Makamu mwenyekiti wa Halimashauri ya wilaya ya Mbozi   Ndugu Allan Mgula  alipokuwa ana hutubia wananchi wa wilaya ya mbozi katika maadhimisho hayo

“ nawaomba wananchi wa wilaya hii ya Igamba mshirikiane katika kulima  na kuhifadhi mazao ya chakulatuogope kuwa ombaomba keani ni aibu kuomba chakula”

Pia aliwapongeza wanakijiji wa Hatelele walio jitangaza kuwa ni waadhilika wa ugonjwa wa ukimwi na kwamba kuwa wa wazi kuta punguza kasi ya maambukizi ya ugonjwa huu wa ukimwi wilayani

Aidha aliwasisitizawananchi wa wilaya ya Mbozi kushirikiana katika mikutano ya hadhara ili wawezekusomewa taarifa za mapato na matumizi kila baada ya miezi mitatu.

Ndugu Mgula aliwataka wananchi wa wilaya ya Mbozi kuudhuria katika vikao vya mabaraza ya mchakato wa kupata katiba mpya ya Tanzania

Aliwataka wananchi wa wilaya ya Mbozi kuwapeleka watoto wa kiume”kutahiliwa” kufanyiwa usafi kwani kufanya hivyo kutapunguza magonjwa ya zinaa kwa watoto wa kiume na pia huduma hizo hutolewa bure kwenye hospitali ya wilaya

Maadhimisho hayo yali hudhuriwa na wa fanya kazi wa Halmashauri ya wilaya Madiwani wa kata Wenyekiti wa wa vijiji wenyeviti wa matawi watendaji wa vijiji makatibu wa tawi naChifu wa kijiji na wananchi wa wilaya ya Mbozi.

Jul 2, 2013

ZIARA YA OBAMA KATIKA VIDEO-CHANZO MICHUZI BLOG

Jun 30, 2013

KIMONDO SUPER SPORT CLUB YAINGIA DARAJA LA KWANZA KWA KUIGAGADUA POLISI JAMII BAO 3-1


PICHA ZOTE NA CAPTIONS KWA HISANI YA MWANAFASIHI(MAHIRI WA SIMULIZI BLOG).


WACHEZAJI WA TIMU YA KIMONDO WAKIPEANA MIKONO NA WACHEZAJI WA TIMU YA POLISI JAMII, KABLA YA KUANZA KWA MECHI YA LIGI YA MABINGWA WA MIKOA KATIKA UWANJA WA SOKOINE LEO JIONI


TIMU YA POLISI JAMII YA BUNDA-MARA


TIMU YA KIMONDO FC YA MBOZI-MBEYA


GOLIKIPA WA TIMU YA POLISI JAMII  EMANUEL DAUD AKISHANGAA GOLI LILILOFUNGWA NA MCHEZAJI WA TIMU YA KIMONDO CHARLES HIZA DK YA 12


GOLI LILIPITILIZA NA KUPENYA KWENYE NYAVU NA KUSABABISHA REFARII NA VIONGOZI WA CHAMA CHA MPIRA WA MIGUU MKOA WA MBEYA KUREKEBISHA NYAVU HIZO KWA DAKIKA KADHAA KABLA YA MPIRA HAUJAWEKWA KATI












Add caption








GOLI LA TATU KWA UPANDE WA KIMONDO BAADA YA MPIRA WA PENALT GOLI LILIFUNGWA NA MCHEZAJI LUKA MPOSHI DK 59


WACHEZAJI WA TIMU YA KIMONDO WAKISHANGILIA GOLI








KIPUTE KINAENDELEA UWANJANI




PATASHIKA KATIKA GOLI LA POLISI JAMII




NDEREMO NA HOI HOI ZILITAWALA BAADA YA KIPYENGA CHA MWAMUZI KUPILIZWA HUKU KIMONDO FC IKIWA MBELA KWA MABAO 3-1


POLISI WALILAZIMIKA KUMTOA NJE YA UWANJA REFARII KUTOKANA NA KUZONGWA NA WACHEZAJI WA TIMU YA POLISI JAMII MARA BAADA YA KUMALIZIKA KWA MCHEZO




HOI HOI ZA FURAHA ZINAENDELEA


MASHABIKI WAKIWA WAMEMNYANYUA JUU MWENYEKITI WA TIMU HIYO ELICK AMBAKISYE BAADA YA TIMU HIYO KUJIHAKIKISHIA KUCHEZA LIGI KUU TANZANIA BARA








SHANGWE NA HOI HOI ZINAENDELEA KATIKA DIMBA LA KUMBUKUMBU YA SOKOINE MKOANI MBEYA






KOCHA WA TIMU YA POLIS JAMII MADENGE OMAR AKILALAMIKIA UTARATIBU WA UENDESHAJI WA LIGI HIYO


PONGEZI ZINAENDELEA


'TUMESHINDA TUNAMSHUKURU MUNGU TUMEPITIA VIGINNGI NA VIKWAZO VINGI'' AKIONEKANA ANASEMA MWENYEKITI WA TIMU HIYO ELICK MINGA






SHABIKI WA TIMU YA KIMONDO MBEGU MOJA AKIWAZAWADIA WACHEZAJI WA TIMU HIYO SH. 200,000 BAADA YA USHINDI






Na DannyTweve

Timu ya Kimondo super sports club ya Mbozi mkoani Mbeya imeungana na ... kuingia daraja la kwanza Tanzania bara baada ya kumaliza mchezo wake jana kwa kuifunga timu ya Polisi jamii ya Bunda mkoani mara mabao 3 -1.

Katika mchezo mzuri na wakasi uliofanyika uwanja wa sokoine jijini Mbeya ulishuhudia Polisi Jamii wakicheza kufa na kupona licha ya maelezo ya kocha wao kuwa walishtukizwa mchezo huo kwani TFFA awali walitangaza kuwa ungechezwa siku ya jumapili.

Bao la kwanza la Kimondo liliwekwa wavuni mnamo dakika ya 12 kupitia kwa Charles Hiza baada ya kupokea pasi kutoka kwa Geofrey Mlau na kumchungulia mlindamlango wa Polisi Jamii Emmanuel Daud na hatimaye kumchambua na kuhesabu bao la kwanza

Mashambulizi ya hapa na pale yaliendelea kwa timu zote ambapo mnamo dakika ya  17 Cosmas Mwazembe wa Kimondo SSC aliunganisha wavuni kwa kichwa krosi ya Charles Hiza na kuifanya Kimondo kuongeza hamasa kwa mabao 2 ya haraka haraka waliyoyapata.

Hata hivyo sherehe hiyo ilidumu kwa dakika 30 tu kwani Polisi jamii kupitia kwa Joseph Onyango waliweza kuihada ngome ya Kimondo na kuachia shuti kali lililodakwa na kutemwa kwenye nyavu na kipa wa Kimondo Daud Pius ha hivyo kuwafanya Polisi Jamii kutoka kipindi cha kwanza wakiwa na matumaini ya kurejesha bao la jingine katika kipindi cha pili.

Bao la tatu kwa Kimondo lilifungwa mnamo dakika ya 59  kwa njia ya penati kupitia kwa Lucas Baraka baada ya mshambuliaji Geofrey Mlau kuangushwa eneo la hatari katika purukushani za kumdhibiti akiwa njiani kwenda langoni mwao.

Mnamo dakika ya 57 mwalimu wa Polisi jamii Bunda  Madenge Omary alitolewa eneo la benchi la ufundi baada ya kumtukana  mwamuzi wa mchezo huo Daudi Ahadi kutoka jijini Dar es Salaam  na akizungumza baada ya mchezo huo, alisema wachezaji wake wamechezeshwa wakiwa wamechoka kutokana na kuwasili asubuhi jijini Mbeya na kulazimishwa kucheza wakati TFF ilikuwa imetangaza mchezo huo kuchezwa siku ya jumapili na si jumamosi.

Akizungumzia kupanda daraja kwa timu yao Mkurugenzi wa Timu ya Kimondo Erick  Minga ndoto za wilaya ya Mbozi kuwa mkoa zinakwenda sambamba na ukuzaji wa soka wilayani humo ambapo watahakikisha timu yao inapanda daraja na kuingia ligi kuu msimu ujao na kuwataka wananchi wa mkoa wa mbeya kwa ujumla kushiriki katika kuchangia mafanikio ya timu zao.

Alisema tayari sasa mkoa utakuwa na michezo mfululizo katika uwanja wake wa sokoine kwa kuwa kuna timu mbili za ligi kuu, pia Kimondo itavuta michezo ya daraja la kwanza hatua ambayo wananchi watafadi uhondo wa soka mkoani mwao kwa mwaka  mzima.



Jun 27, 2013

MBOZI YAENDELEA KUKABILIWA NA CHANGAMOTO ZA MAJI SAFI NA SALAMA


Na Angela Kivavala- Mbozi   

Asilimia 44   wakazi wa wilaya ya Mbozi ndiyo wanaopata huduma ya maaji safi na salama imefahamika

Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari mkugenzi mtendaji halmashauri ya wilaya ya Mbozi Levison Chillewa amesema kwa sasa wilaya inategemea aina tatu za vyanzo vya maji vikiwemo  visima, mitiririko na maji ya chemichemi zilizo boreshwa.

Akifafanua  Chillewa amesema  kuna  jumla ya  visima virefu na vifupi 105 chemichemi za asili 40 mitiririko 5 na matanki 6 yanayotumika kuvuna  maji ya mvua.

Chillewa amesema kupitia programu ya maji na usafi wa mazingira vijijini (RWSSR),wilaya inatekeleza  miradi ya ujenzi  wa  miundombinu  ya maji katika wilaya ya mbozi ambapo hadi sasa visma vitano vinajengwa ikiwa ni vyanzo vya usambazaji wa maji katika vijiji vitano vya wilaya ya mbozi

Aidha Kupitia mfuko wa maendeleo ya jamii TASAF, halmashauri ya wilaya ya Mbozi   imewezesha baadhi ya shule za sekondari na  hususani miradi ya ujenzi wa hosteli pamoja na baadhi ya huduma kama zahanati na nyumba za walimu kuwa na  mfumo wa uvunaji wa maji ya mvua  kwa kuwekewa  tanki za plastiki (SIMTANK) zenye ujazo wa kati ya lita 5000 hadi lita 10,000.

Kuhusiana na uhifadhi wa mazingira, Mkurugenzi huyo amesema wilaya ya mbozi vyanzo vya 23 tayari vimepimwa na vipo kwenye hatua za kuwekewa alama za kudumu.

 aidha halmashauri ya wilaya imeanzisha mfumo wa  kuifadhi takwimu  za vyanzo vya maji ambapo hadi mwezi mei jumla ya vyanzo vya maji 471 vilikuwa vimetambuliwa pia vyanzo vya maji vimepewa kipaumbele na kamati za maendeleo za vijiji na kata.

Pamoja na mafanikio wilaya imekuwa ikikumbanana changamoto mbalimbali ikiwemo uharibifu wa vyanzo vya maji unaotokana na kulima kujenga kuchoma moto na kuchunga mifugo kwenye vyanzo vya maji na gharama kubwa za uchimbaji na ujenziwa miundombinu ya maji.

Wilaya imeweza kuwekamikkati ya kuzikabili changamoto hizo ikiwa nipamoja na  kuelimisha jamii kuusu umuhimu wa tuunzaji wa vyanzo vya maji kulinda na kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchiikiwa ni pamoja na upandaji wa miti  katika vyanzo vya maji, vijiji vyote vyawilaya vimepewa jukumula kudhibiti uharibifu katika vyanzo vya maji

Kwa mwaka 2013/ 2014 halmashauri imetengewa TSH 1,425,470,049 kwaajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo ya maji wilaya ya mbozi

Mwisho

 

Jun 23, 2013

KIMONDO YA MBOZI YAZIDI KUPETA LIGI YA MABINGWA RAUNDI YA PILI, YATOA SARE UGENINI MUSOMA

Timu ya Kimondo ya wilayani Mbozi imeendeleza wimbi la kujitengenezea mazingira mazuri kuingia ligi daraja la kwanza  Tanzania bara baada ya kuilazimisha sare ya bao 2-2 Timu ya Polisi Jamii ya Musoma katika uwanja wake wa Nyumbabi wa Karume mjini Msoma
Polisi jamii ambao walianza kupata bao lao la kwanza walijikuta wakishindwa kubana na badala yake wakaachia mnamo dakika ya 36 baada ya Kimondo kupanga mashambulizi huku wakiwasiliana kwa kutumia kiwemba, kindali na kinyiha huku wakiwaaacha maafande wakishangaa hadi Geofrey Mlau akiandika bao la kwanza na lakusawazisha.
Nyumbani ni nyumbani ilidhihirika baada ya kipindi cha kwanza kumalizika kwa nguvu sawa kwa kufungana bao moja kwa moja, kipindi cha pili kilianza kwa mashambulizi ya kasi kutoka polisi jamii ambao waliweza kupata bao la pili mnamo dakika ya 67 lakini halikudumu muda mrefu kwani mnamo dakika ya 75 hali ilikuwa mbaya kwa wenyeji
Alikuwa Imani Wilson aliyewainua mashabiki wa Musoma bila kujali uzalendo kwa timu yao na kuamua kushangilia timu ya wageni Kimondo SC baada ya kutungua shuti la kufa mtu lililomfanya mlindamlango wa Polisi Jamii kujifanya kama vile alikuwa akisikiliza simu kwa jinsi lilivyoingia na kumchanganya kabisaa.
Ikiongozwa na mlezi wao ERICK MINGA Kimondo iliendelea kufanya mashambulizi yenye lengo la kuwadharirisha wenyeji kwenye uwanja wao wa nyumbani hata hivyo mashambulizi hayo yaliiishia kwa kosa kosa, hadi timu inatoka uwanjani wananchi wa Musoma walishindwa kuvunga na badala yake wakajikuta wakitoa mikono ya pongezi kwa mtanange mtamu ulioonyeshwa na Kimondo Sc.
Katika kudhihirisha nia ya kupata mkoa mpya wa Songwe, Wilaya ya Mbozi kupitia wadau wake imeendelea kusukuma mbele ajenda ya michezo ambapo miongoni mwa wadau FULL DOSE ambaye amejitokeza mbele kuidhamini timu hiyo anaeleza kuwa tutaingia mkoa mpya tukiwa na timu mpya ya ligi kuu!!
 
 
Add caption


May 29, 2013

MBOZI SHWARII

 Naibu waziri wa Elimu Kassim Majaliwa akisalimiana na Mbunge wa Mbozi Godfrey Zambi siku alipofika wilayani Mbozi, wilaya ya Mbozi imo kwenye mchakato wa kupata mkoa wake
 Mkuu wa wilaya ya Mbozi Dr Kadeghe akimtambulisha naibu waziri kwa kaimu Mkurugenzi Mbozi Dr Charles Mkombachepa
 Walimu wakimsikiliza naibu waziri

walimu wakifuatilia majadiliano

May 28, 2013

MGAWANYO WA MKOA WA MBEYA WAJIELEKEZA KUVUTIA KIMAKABILA


Na Mwandishi wa Indaba Africa,

Mnyukano wa ugawaji wa mkoa wa Mbeya umeendelea kujenga sura ya uasilia wa waliopo kwenye madaraka kutokana na wanasiasa kuvutia maeneo walikotoka bila kujali vigezo vya msingi ikiwemo idadi ya watu.

Kulingana na vikao vinavyoendelea, wilaya ya Rungwe tayari imeshajitengenezea mazingira mazuri ya kupigiwa debe kuwa mkoa kwa kile kinachobainishwa kuwa madiwani wengi katika mkoa wa Mbeya asili yao ni wilaya ya Rungwe

Dhana ya “kumitu kukhaja ” inaonekana wazi wakati huu  kwenye mchakato wa kutoa mapendekezo ya wapi na maeneo yapi yaunganishwe kuunda mkoa wa mpya  baada ya Mh Rais Kikwete kutamka wazi na kubariki mchakato huo wakati wa maadhimisho ya siku ya wafanyakazi mei mosi.

Mfano wa kujipigia debe unaonyesha kuwa Mwenyekiti wa halmashauri ya Mbarali Keneth Ndingo ni mkazi wa Rungwe hivyo maamuzi ya baraza la madiwani la Mbarali yanaonekana kuwa na msukumo wa nyumbani, ambapo wamependekeza makao makuu yawe Rungwe

Maajabu ya musa yanajitokeza katika ugawaji unaopendekezwa ambapo inaelezwa kuwa Mbarali wanapendekeza halmashauri za Busokelo, Rungwe, Kyela, Ileje na Mbozi ziunde mkoa mpya wakati kijiografia havina uwiano kati ya Mbozi na Rungwe.

Kulingana na takwimu za sense ya mwaka2012, wilaya ya Mbozi kabla ya kugawanywa kupata Momba ilikuwa na wakazi 740,719 idadi ambayo ni sawa na idadi za wakazi wa wilaya za Kyela, Rungwe na Ileje ambazo kwa pamoja ni wakazi 685,098 hivyo kuwepo kwa pengo la 55621 zaidi kwa upande wa Mbozi

Kulingana na jiografia ya mkoa wa Mbeya, Mkoa ambao kwa sasa ungeweza kuundwa kwa kuunganisha wilaya za  Ileje, Mbozi, Momba  na sehemu ya wilaya ya Chunya  (jimbo la Songwe) ambalo limejitenga na eneo la Lupa kwa umbali wake.

Kwa takwimu hizo hizo mkoa wa  huo ungeweza kuwa na idadi ya wakazi 1,201,327 ambao  ni asilimia 44.4 ya takwimu za sasa za wakazi wa mkoa wa Mbeya wanaofikia 2,707,410.

Ingawa jitihada za kujipanga zimeanza kwa upande wa wilaya za Rungwe, Mbarali na Kyela kwa kufanya ushawishi wa mbinu,ukweli unabakia kuwa wilaya ya Mbozi peke yake inavigezo vyote vya kupata mkoa mpya kuanzia idadi ya watu, eneo la utawala,makazi, uwezo wa raslimali za ndani kujiendesha na fulsa za kiuchumi zilizopo na zinazoweza kupatikana.