Adverts

Apr 21, 2009

Mandela ahimiza umaskini ufekwe

Rais mstaafu wa Afrika Kusini,Nelson Mandela amehudhuria kikao cha mwisho cha kampeni ya uchaguzi ya chama chake cha ANC hii leo,siku tatu kabla ya uchaguzi wa bunge nchini humo.Maelfu ya wafuasi wa kiongozi mpya wa ANC,Jacob Zuma,wamemshangiria Nelson Mandela alipoingia katika uwanja wa michezo mjini Johannesburg."Katika wakati ambapo tunataka kuhakikisha ushindi kwa chama chetu,tunabidi tukumbuke kwamba jukumu letu la mwanzo ni kuung'owa umaskini" amesema mwanasiasa huyo mwenye umri wa miaka 90,mshindi wa zawadi ya amani ya Nobel.Chama kilichojitenga cha Congress kinafanya kampeni yake ya mwisho ya uchaguzi leo pia katika mkoa wa Limpopo na kile cha upinzani cha Democratic Alliance kilikutana jana mjini Cape-Town. ANC kinapewa nafasi nzuri ya kuibuka na ushindi,katika uchaguzi huo wa nne tangu tangu tukio la kihistoria la mwaka 1994 lililomleta madarakani Nelson Mandela.Wapiga kura milioni 23 watatakiwa jumatano ijayo walichague bunge jipya la taifa na mabunge ya kimkoa.