Adverts

Apr 30, 2009

MCHUNGAJI ALIYEJIFANYA KUIBANIA MAHAKAMA, YAMKUTA HATIMAYE AREJEA KUAPA

Hatimaye Mchungaji Simon Kitwike wa Kanisa la EAGT Ichenjezya wilayani Mbozi mkoa wa Mbeya, aliyekataa kuapa mahakamani na kupelekea kufungwa kifungo cha miezi sita jela, amekubali kuapa na hivyo kuruhusiwa kuendelea kutoa ushahidi wake.Marchi 23,mwaka huu kesi yake ilipotajwa kwa mara ya pili
Mchungaji huyo ambaye anatumikia kifungo chake akiwa nje ya Gereza, alifika mahakamani hapo alipoulizwa kama atakuwa tayari kuapa alikubali kufanya hivyo kasha alipewa Biblia na kuapa kwa mujibu wa sheria.Kesi hiyo inawakabili washitakiwa watatu akiwemo mwanamke mmoja ambao ni Telezia Mtega, Hekima Simkoko na Emmanuel Lwinga ambao walikutwa na baadhi ya vifaa vya wizi ambavyo vinasadikiwa kuwa mali ya mchungaji Simon Kitwike.Hata hivyo baadqa ya kutoa ushahidi wake kesi iliahirishwa hadi Marchi 31 itakapotajwa tena, na kuwa washitakiwa wawili wako nje kwa dhamana, ambapo mshitakiwa mmoja anashikiliwa kutokana na kuwa na kesi nyingine inayomkabili.Februari 4, mwaka huu mchungaji huyo alifika katika mahakama ya wilaya ya Mbozi ili kutoa ushahidi kwa watuhumiwa watatu waliokamatwa na baadhi ya bidhaa zilizoibiwa nyumbani kwake Oktoba 25 mwaka jana, lakini kutokana na imani ya dini yake alikataa kuapa mahakamani kwa mujibu wa kifungu katika Biblia cha Injili ya Mathayo 5:33 – 37 ambacho kinaeleza kuwa “Tena mmesikia watu wa kale walivyoambiwa usiapa uongo ila mtimizie Bwana nyapo zako lakini mimi nawaambia msiape kabisa hata kwa Mbingu kwa maana ndicho kiti cha enzi cha Mungu”.Baada ya kukataa na kusoma kifungu hicho Hakimu Nyasige Kajanja aliahirisha kesi hiyo kwa muda ili akajiridhishe na sheria, hata hivyo alipporejea tena mahakamani hakimu huyo alimsomea sheria kuwa asiyeapa anatenda kosa la kuidharau mahakama ambalo adhabu yake ni kifungo cha miezi 12 jela kwa kutumia kifungu cha sheria namba 198(1) kama ilivyorekebishwa mwaka 2002.Hata hivyo Hakimu Kajanja alimtaka Mchungaji huyo kusoma kitaBU CHA Warumi 12;1-2 kinachoeleza kuwa;” Kila mtu na aitii Mamlaka iliyo kuu kwa maana hakuna mamlaka iliyopo imeamriwa na Mungu, hivyo amwasiye mwenye Mamlaka hushindana na agizo la Mungu nao washindanao hujipatia hukumu”Mchungaji huyo alifungwa jela miezi sita kufuatia kukataa kuapa mahakamani ambako alitakiwa kuapa kabla ya kuanza kutoa ushahidi wake juu ya kuvunjiwa nyumba yake na kuibiwa mali zenye thamani ya shilingi milioni 2.2.Akizungumzia mkasa uliompata alisema kuwa Oktoba 25 mwaka jana majira ya saa sita za usiku kundi la majambazi lilifika nyumbani kwake na kumuamuru kutoa fedha la sivyo wangemuua.Mchungaji huyo alitaja mali alizoibiwa kuwa ni pamoja na fedha taslimu shs. 1.212 milioni, godoro moja, seti moja ya luninga, radio mbili masanduku mawili ya safari (Brief case) na simu za mkononi mbili na rewinder moja, hata hivyo majambazi hayo hayakuwadhuru