Adverts

Apr 3, 2009

SHIRIKA la viwango nchini TBS limezindua maabara Ugezi (inayotembea) katika mikoa ya Nyanda za juu ikiwa ni hatua ya kuhakikisha ubora wa bidhaa zinazolengwa kuuzwa nje unalindw. Sambamba na hilo maabara hiyo inalenga pia kuwapunguzia gharama wateja wake ambao kwa sehemu kubwa ni viwanda vilivyopo kwenye mikoa hiyo ambapo huduma tano zitatolewa na maabara hiyo katika hatua mbali mbali za uzalishaji wa bidhaa za viwanda. Uzinduzi huo umefanywa kwenye kiwanda cha saruji cha Mbeya na Maafisa Ubora waandamizi wa TBS bwana Ingramu Kisamo na Alfonce Kagoma ambao kwa pamoja pamoja na kutembelea na kukagua maabara ya kiwanda hicho pia wameelezea faida zitakazopatikana kutokana na matumizi ya maabara hiyo ikiwemo viwanda kufahamu ubovu na hitilafu za mitambo yao ya uzalishaji, kufuatilia mifumo ya umeme, msukumo na hali joto Kwa upande wake afisa uhusiano wa TBS Bi Roida Andusamile pamoja na afisa Uzalishaji wa kiwanda cha saruji Mbeya bwana Usiri ELILIA wamesema msaada wa gari hilo kutoka UNIDO ni hatua nyingine muhimu itakayoongeza mahusiano baina ya watumiaji wa huduma za TBS na wazalishaji katika kujihakikishia bidhaa zinazozalishwa zinazingatia viwango vya kimataifa. Chini ya maelekezo ya shirika la afya Ulimwenguni bidhaa zinazozalishwa na kuuzwa nje zinapaswa kupitishwa na taasisi za ubora za ndani na upande wa tatu ambao ni huru na kwakutumia vifaa vilivyopitishwa, na kwamba gari hilo ni sehemu ya mitambo iliyopitishwa kwa umahiri katika kuhakiki viwango tangu wakati wa uzalishaji. Danny