Adverts

Sep 3, 2009

WAZO LA UTAFITI +UTENDAJI WA WAHUDUMU KLINIKI

Ninafikiria kufanya utafiti kuchunguza hali ya utendaji kazi wa watumishi wa afya kwenye eneo la uandikishaji wajawazito. Wazo hili limekuja baada ya kukutana na kadi kama nne za wajawazito zikiwa zimejazwa particular nyingi zinazoonyeshwa wamepimwa wakati hawakupimwa. Matokeo yake ni kwamba rekodi za mimba husika zinaendelea kuonyesha ipo salama kumbe kuna matatizo. Mfano kwenye kadi hiyo inaonyesha mjamzito huyo amepimwa 1.Mapigo ya moyo ya mtoto( Kitu ambacho hakupimwa kwa mujibu wa mja mzito mwenyewe) 2.Kwamba kuna kidokezo cha miguu kuvimba kwamba hana tatizo(wakati mjamzito huyo ana tatizo la kuvimba miguu tangu apate ujauzito. 3.Mtoto anacheza tumboni(ikaandikwa hachezi) wakati mjamzito katika maelezo yake inaonyesha mtoto anacheza. Hii ikaongezewa na maelezo kuwa kumekuwa na msongamano mkubwa wa wajawazito kliniki na matokeo yake wahudumu hao wamekuwa wakijaza kadi hizo bila kuwapima wakati kuna vidokezo vya hatari vinavyopaswa kurekodiwa vyema kwaajili ya kufuatilia maendeleo ya makuzi ya mimba na hali za wajawazito hao. Utafiti huu ninadhani unaweza kuibua mengi kwani bado vifo vya wajawazito vimekuwa vikiripotiwa kuendelea kutokea licha ya takwimu za serikali kuendelea kueleza kuwa vinapungua. ninahitaji mawazo yenu. nitumie kwenye dtweve1@yahoo.com