Adverts

Sep 28, 2010

ENZI ZA MIGOWE UNAZIKUMBUKA? AAH WAPI LABDA KAMA ULIKULIA KIJIJINI

Enzi zetu kuna mtu alikuwa anapita na ngoma ama kijembe nyakati za jioni akipiga kelele " kesho wananchi wote kumaendeleo!!!!! namkumbuka mzee mmoja alikuwa anashindwa kutamka neno "kwenye maendeleo" basi akawa ana tamka kama nilivyoandika hapo nyuma, basi kesho yake inakuwa nyomi kama hivyo yaani hakuna anayekosa kwakuwa kuna faini na pia mgambo wetu walikuwa wanapewa jukumu la kukamata na kufungia kwenye ofisi ya kijiji, siye huku kwetu bado shughuli za maendeleo zinafanyika kama hivi sijui huko mjini? manake unaweza kusikia hata kufagia uwanja wako unasubiri serikali ikufagilie  watu bwana!!!