Adverts

Sep 29, 2010

RIDHIWAN AKUTANA NA MAGUMU IRINGA- WANYALU WASEMA SWELA


Na Francis Godwin,Iringa


MTOTO wa mgombea urais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Jakaya mrisho Kikwete ,Ridhiwan Kikwete leo ameonja joto la jiwe katika ziara zake za kampeni ndani ya CCM baada ya kutimuliwa mbio zaidi ya mara moja wakati akitaka kufanya kampeni za CCM katika taasisi za umma.
Ridhiwani ambaye ni mjumbe wa kamati ya utekelezaji ya baraza kuu la umoja wa vijana wa chama cha mapindunzi (UVCCM) Taifa akiwa na viongozi akiwemo aliyekuwa mshindi wa kura za maoni jimbo la Iringa mjini Frederick Mwakalebela na washiriki wengine wa kura za maoni kama Jescar Msambatavangu walifika katika shule ya msingi Ipogolo wakitaka kukutana na vijana wa eneo hilo ili mjumbe huyo aweze kumuunganisha mgombea ubunge wa jimbo hilo Monica Mbega na Mwakalebela japo mkakati huo uligonga ukuta.
Kabla ya msafara wa Ridhiwan kufika shuleni hapo kwa ajili ya kikao chake cha ndani ya vijana wa CCM kwa lengo la kuvunja makundi ndani ya chama hicho ,aliyekuwa mmoja kati ya wana CCM 12 walioingia katika kinyang'anyiro cha ubunge jimbo hilo Msambatavangu alipita mitaani kujaribu kuwaomba vijana kwenda kumsikiliza mtoto huyo wa Rais Kikwete japo waligoma kwa madai kuwa hawadanganyiki na ujio wake.
Hata hivyo baada ya vijana hao wa vijiweni kugoma kwenda katika shule hiyo kwa ajili ya kutana na mjumbe huyo kwenye chumba cha darasa la pili katika shule hiyo ya msingi Ipogolo bado msafara huo uliweza kufika katika eneo hilo kwa ajili ya mkutano japo idadi ya vijana waliokuwa wamefika ilikuwa ni kama vijana 10 pekee.