Sep 26, 2010
WANAHABARI WATAHADHARISHWA KULINDA MAISHA YAO
Wandishi wa habari wametahadharishwa kuwa wasijiweke katika mazingira ambayo yatawafanya wapoteze maisha kwa dhana kuwa wanaripoti ukweli hasa nyakati hizi za uchaguzi kwa kuzingatia kuwa bado vyombo vingi vya habari havijatengeneza mazingira ya kulinda maisha ya wanahabari na familia zao.
Akizungumza katika mafunzo ya siku moja ya kupitia Maadili ya uandishi wa habari za uchaguzi 2010, afisa habari kutoka shirika la umoja wa mataifa la maendeleo-UNDP bwana Sebastian Sanga amesema wandishi wa habari wanapaswa kujali maisha yao zaidi kuliko kujiweka mbele wakati hawana bima za maisha yao.
alisema kazi ya uandishi wa habari haitakuwa bora ikiwa mwandishi atajihatarishia maisha yake kwa kujiweka mbelembele wakati ambapo mazingira wanamofanyia kazi hakuruhusu hali hiyo.
alihoji kama kuna mwanahabari miongoni mwa wandishi 50 waliohudhulia mafunzo hayo kama yupo aliyekatiwa bima na chombo chake cha habari anachoandikia.
hata hivyo ilibainika kuwa wengi wa wandishi hao hawana bima na akaendelea kuwaeleza kuwa maisha ni bora kuliko kitu chochote kile na kwamba si lazima mtu akapoteza maisha yake eti kwakuwa anakitumikia chombo chake cha habari kwa kufanya uchokonozi wakati ambapo chombo anachokiandikia hakijaweka mazingira mazuri kwake ya kufanya kazi hizo.
Alisema kuna umuhimu mkubwa wa kujali zaidi maisha na uhai wa mwandishi binafsi badala ya kujiweka mbele kujali maslahi ya chombo unachoandikia kwakuwa miongoni mwa wanahabari wenyewe wamekuwa wakiuzana.
Wakati akizungumzia hali hiyo wengi wa wanahabari walionekana kupoteza pumzi hasa kwa kukumbuka mazingira wanayofanyia kazi kuonekana kuwa ya manyanyaso makubwa kutoka kwa vyombo wanavyovitumikia ikiwa ni pamoja na utaratibu wa kupima habari zao kwa kutumia rula ili walipwe.