Adverts

Oct 4, 2010

BARUA YA MTOTO KWA MWENYEZI MUNGU

Mtoto mmoja mwenye umri wa miaka 9 alikuwa anahitaji sana shilingi 100,000
(Laki moja). Akamuuliza mama yake ni jinsi gani anaweza kupata pesa hizo. Mama yake
akamwambia "muombe Mungu atakupatia.  Mtoto alianza kuomba kila siku na kila
mara lakini  hakupata hiyo pesa toka kwa Mungu. Hatimaye akafikia  uamuzi wa
kumuandikia barua Mungu ili asome maombi  yake.

Kisha akai-post barua ile.  Wakati wafanyakazi wa posta wakichambua barua
kwa
ajili ya kuzipeleka sehemu husika, walishangazwa kuona  bahasha iliyoandikwa
"Kwa Mwenyezi Mungu" na wakashindwa kuelewa mahali pa kuipeleka, Wakaamua
kuifungua.

Barua ilisomeka hivi:
"Mpendwa Mungu,

Jina langu ni EMMANUELEY, nina umri wa miaka 9 na ninasoma darasa la tatu
katika
jiji la Dar es salaam ambalo liko katika nchi ya Tanzania ,  bara la Africa .

Nimeamua kukuandikia barua hii kukuomba kiasi cha shilingi laki moja baada ya
kuomba bila kupata majibu toka kwako.
Naomba sana unisaidie kwani mimi ni mtoto mdogo na sina uwezo wa kufanya
kazi na
kupata pesa. Pia wazazi wangu hawana uwezo kwani hata nchi yetu ni maskini
sana .

Natanguliza shukrani.

Wako mtiifu,
EMMA."


Wafanyakazi wa posta walifurahishwa sana na barua hiyo na kisha wakaamua
waipeleke kwa Rais . Rais  naye alipoipokea ilimfurahisha
sana na
kisha akamwambia Secretary wake achukue sh. 2000 amtumie mtoto huyo akidhani
kuwa pesa hizo ataziona kuwa nyingi sana .
Mtoto huyo alipopokea hizo shilingi 2000 alijibu hivi:
"Mpendwa Mungu wangu,

Nashukuru sana kwa kusikiliza maombi yangu na kunitumia pesa nilizokuomba.
Lakini nimebaini kuwa uliamua kuzituma kupitia serikali yetu ya Tanzania .Kama ilivyo kawaida yao, wamekata kiasi cha sh. 98,000 kwa ajili ya kodi , kwa hiyo wameniletea Sh. 2000 tu