Adverts

Jan 13, 2011

Pinda azindua mpango wa kuendeleza kilimo ukanda wa kusini

Pinda azindua mpango wa kuendeleza kilimo ukanda wa kusini: "
Waziri mkuu Mh. Mizengo Pinda akifanya uzinduzi wa mpango wa kuendeleza kilimo ukanda wa kusini m wa tanzania [SAGCOT ] kulia kwake ni waziri wa kilimo na ushirika Prof Jumanne Maghembe kushoto ni katibu mkuu ofisi ya waziri mkuu Peniely Lyimo.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akikata Utepe kuashiria uzinduzi wa Mpango wa Uendelezaji wa Kilimo katika eneo la Ukanda wa Kusini mwa Tanzania (SAGCOT) wenye lengo la kuwainua na kuwawezesha wakulima wadogo wanufaike na shughuli za kilimo hivyo kukuza sekta binafsi. Wanaoshuhudia uzinduzi huo kutoka kulia ni Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri mkuu Bw. Peniel Lymo na Bw. Frank Braeken mwenyekiti wa ukanda wa Mpango wa Kilimo Kwanza.
Baadhi ya Mawaziri wa Tanzania na Mabalozi wa Nchi mbalimbali wakifuatilia mambo mbalimbali wakati wa uzinduzi wa Mpango wa Uendelezaji wa Kilimo katika eneo la Ukanda wa Kusini mwa Tanzania (SAGCOT) leo jijini Dar es salaam.
Wadau wa sekta ya Kilimo wakiwemo wawakilishi wa mashirika yanayojihusisha na shuguli za kilimo, mabalozi wa nchi wahisani, mashirika binafsi na wakulima wakiwa ndani ya chumba cha mkutano kushiriki uzinduzi wa uzinduzi wa Mpango wa Uendelezaji wa Kilimo katika eneo la Ukanda wa Kusini mwa Tanzania wenye lengo la kuwainua na kuwawezesha wakulima wadogo wanufaike na shughuli za kilimo leo jijini Dar es salaam.Picha na Aron Msigwa – MAELEZO.
" indaba2010