Waziri wa Maji Mh.Mark Mwandosya amemtembelea nyumbani kwake kada wa C.CM Mustafa Sabodo na kumshukuru kwa msaada wake wa kusaidia uchimbaji wa visima vya maji 600 nchi mzima.Akimshukuru kwa niaba ya Serikali Waziri Mwandosya alisema kuwa, yeye binafsi anashukuru kwa mchango mkubwa ambao bwana Sabodo anasaidia Serikali katika kutatua matatizo ya maji. ‘’Kimsingi msaada wako unaendeleza tuu sera ya kuwapatia wananchi maji safi na salama kwa hilo mzee Sabodo tunakushukuru’’ alsema Mh. Waziri.
Kwa upande wake Mustafa Sabodo alimueleza Mh.Waziri kuwa ,ili kukamilisha azma hiyo ametenga bajeti ya Sh 1.8 bilioni kugharamia uchimbaji wa visima hivyo. ’’kawa sababu umekuja kunishukuru basi nasema nakupa visima 100 kwa Mbeya pekee hivyo kufanya idadi ya visima vitavyochimmbwa kuwa 700 nchi mzima’’ alisema mzee Sabodo.Baada ya mazungumzo mafupi Mh Wazri alimkabdhi Mzee Sabodo nakala ya Sera ya maji na pamoja na makakati wa maendeleo ya sekta ya maji.Hata hivyo, Mh Waziri alimhakikishia mzee Sabodo kuwa Wizara ya Maji itashirikiana kwa na kamati aliyoounda kwa kutoa ushauri na watalaama pale watakapo hitajika.
"