Adverts

Apr 28, 2011

MTIKISIKO WA UCHUMI WAITIKISA POSTA YABAILIKA SURA KUWA VODA

NDIVYO jengo la Posta Mbeya linavyoonekana kusheheneza rangi za Vodacom wakati lingeweza kujitangaza lenyewe ili kuendelea kuokoteza fedha kidogo kidogo kutokana na biashara zake lakini sasa utadhani ni jengo la kampuni nyingine. Vodacom wametumia vyema fursa ya kujitangaza kwenye majengo kama haya  na hasa katika kuitangaza brand name yake mpya!!!!
Kajengo keupe pembeni ndizo ofisi za EMS Mbeya zilizonusurika kubadilishwa rangi - kweli kampuni ya Posta inaelekea kupteza utambulisho wake!