Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) Mama Salma Kikwete akihutubia  katika mkutano wa wadau mbali mbali wa  shirika la CAMFEDTanzania, mkutano uliofanyika leo katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam. Akihitubia katika mkutano huo Mama Salma Kikwete alisema kuwa WAMA ipo tayari kushirikiana na wadau mbali mbali katika kumsaidia mwanamke kiuchumi.  Kushoto ni Kaimu  Mkurugenzi Mtendaji wa CAMFED Tanzania  Msaada Daudi Balula. Shirika la CAMFED Tanzania limejikita katika kutoa huduma zake katika Wilaya kumi za Tanzania ambazoni ni Kibaha,Kilolo ,Iringa  Vijijini,Rufiji, Bagamoyo,Morogoro Vijijini, Kilombero, Pangani na  Handeni. |