Meneja Mauzo Kanda ya Pwani wa kampuni ya simu ya Airtel, Aluta Kweka (kushoto), akikabidhi sehemu ya msaada wa vitabu kwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Morogoro, Alfred Shayo vilivyotolewa na kampuni hiyo kwa Shule za Sekondari za SUA, Mwembesengo, Mji Mpya na Mgulasi Mkoani Morogoro mwishoni mwa wiki. Wa pili kushoto ni Mkuu wa Sekondari ya SUA, Khalfan Millongo, Meneja Huduma za Jamii wa Airtel Tunu Kavishe na Diwani wa Kata ya Mbuyuni, Samuel Msuya. Vitabu hivyo vina thamani ya shs milioni 4.
Meneja Huduma za Jamii wa Airtel Tanzania, Tunu Kavishe (wa tatu kushoto) akikabidhi sehemu ya msaada wa vitabu kwa mmoja wa wanafunzi wa Shule ya Sekondari SUA, Rogers Shempemba vilivyotolewa na kampuni hiyo kwa Shule za Sekondari za SUA, Mwembesengo, Mji Mpya na Mgulasi Mkoani Morogoro mwishoni mwa wiki. Kushoto ni Meneja Mauzo wa Airtel Kanda ya Pwani, Aluta Kweka na Mkuu wa Sekondari ya SUA, Khalfan Millongo.
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel imekabidhi msaada wa vitabu vya kiada na ziada kwa shule za sekondari nne za mkoani Morogoro, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kusaidia jamii hapa nchini.
Shule zilizopata msaada wa vitabu ni shule za sekondari ya Mwembesongo, Mji mpya, SUA na Mgulasi.
Akizungumza wakati wa kukabidhi vitabu hivyo, Meneja Huduma za jamii wa Airtel, Tunu Kavishe, alisema "shule hizi nne za jijini Morogoro ni kati ya shule zaidi ya 800 nchini ambazo zimeshanufaika na kampeni maalum ya Airtel Shule yetu inayoendeshwa na airtel kwa lengo la kusaidia elimu nchini Tayari tumeshatoa msaada wa vitabu vyenye thamani ya zaidi ya bilioni moja nab ado tunaendelea!!
Alisema Tunu "Tumeamua kuweka uwiano sawa wa shule kila mkoa ili kuhakikisha kuwa vitabu hivi vinawafikia wanafunzi katika maeneo yote nchini. mkakati wetu ni kwamba kila shule nchini inayoingia kwenye kampeni yetu ya airtel shule yetu ipate vitabu vyenye thamani ya Shilingi milioni moja", alisema Kavishe.
Aliongeza kuwa, kwa kuzingatia ya kwamba kila shule ina mahitaji ya vitabu tofauti tofauti kulingana na mitaala waliyonayo, shule zote zimepewa vitabu kutokana na mapendekezo waliyotoa juu ya aina gani ya vitabu wanahitaji ili kuziwezesha shule hizo kukabiliana na uhaba wa vitabu na kufukuza adui ujinga.
"Tunayo malengo ya dhati kabisa katika kusaidia kuinua kiwango cha elimu hapa nchini na kuhakikisha kinaongezeka, hasa kupitia upatikanaji wa vitabu kwa wanafunzi wa shule za sekondari. Kavishe.
Kampuni ya simu ya Airtel imekuwa mstari wa mbele katika kuchangia sekta ya elimu hapa nchini.
"Mbali na zaidi ya shule hizo 800 za sekondari ambazo zimeshanufaika na mpango huu wa kusaidia vitabu vya ziada na kiada ujulikanao kama Airtel shule yetu, Airtel Tanzania tayari tunao mradi wa kusaidia shule za msingi hapa nchini ambapo hivi karibuni tutauweka wazi ili kila mzazi na shule kuutambua na waweze kunufaika nao" alimalizia Kavishe!
Akipokea vitabu hivyo Katibu Tawala wa Wilaya ya Morogoro, Alfred Shayo aliishukuru Airtel na kutoa wito kwa makampuni mengine kuiga mfano huo na kuhimiza wanafunzi kuvitumia kiuhakiki na kwa uangalifu ili vidumu zaidi "Airtel tunawashukuru sana!
Lakini niombe waalimu na wanafunzi shule zote muwe makini na kutunza nyenzo hizi za elimu kwa kuwa zitasaidi sana kwanza kumuondo adui ujinga na baada ya hapo itasaidia kuinua maendeleo ya mkoa wetu kwa kuwa na wasomi bora" alisema Katibu Tawala wa Wilaya ya Morogoro, Alfred Shayo Nae Mkuu wa Sekondari ya SUA, Khalfan Millongo.
Akipoke msaada huo kwa niaba ya waalimu wakuu wa shule zilizofaidika na kampeni ya Airtel shule yetu alishukuru na kusema " tunawashukuru sana airtel kwa kuchangia elimu hii ni kuonyesha jinsi gani mnawajibika na jamii
Thamani ya msaada huu huwezi kuipima kwa kuangalia gharama ya vitabu bali thamani halisi ipo katika maarifa yaliyomo ndani ya vitabu hivi. Hivyo ni msaada ambao hautaisha thamani. Tunasema asante san.
Vitabu hivi vitahakisha kufikia lengo la Serikali kupitia mpango wake wa MMES II ambao umelenga kuwa na uwiano wa 1:3 kwa vitabu vya kiada yaani kitabu kimoja kwa wanafunzi watatu Mwisho naomba niwahakikishe vitabu hivi vitatumika kama ilivyokusudiwa! alimaliza kusema Mkuu wa Sekondari ya SUA,Khalfan Millongo.