PUGILISTIC
SYNDICATE OF TANZANIA
(PST)
SHERIA
ZA BOXING
Na Emmanuel Mlundwa
Ulingo wa
kupigania:
1
Mapambano yatafanyika ndani ya ulingo wa mraba usiopungua
futi 16 x 16na usiozidi futi 20 x 20 kwa ndani.
Kupima uzito,
Madaraja ya uzito (Weight classes) na gloves:
2
Mabondia wote ni lazima wapime uzito ili waruhusiwe
kupigana. Aidha ubingwa utapangwa kulingana na madaraja ya uzito:
(a) minimum weight 47.2
kgs.
(b) Light
Flyweight 48.89 kgs.
(c)
Flyweight 50.91 kgs.
(d) Super flyweight 52.27 kgs.
(e)
Bantamweight 53.64
kgs.
(f)
Super bantamweight 55.45
kgs.
(g) Featherweight 57.27 kgs.
(h) Super
featherweight 59.09 kgs.
(i)
Lightweight 61.36
kgs.
(j)
Super lightweight 63.63
kgs.
(k) Welterweight 66.67 kgs.
(l)
Super welterweight 70.00
kgs.
(m)Middleweight 72.72 kgs.
(n) Super
middleweight 76.36 kgs.
(o) Light
heavyweight 79.54 kgs.
(p) Cruiserweight 90.00
kgs.
(q) Heavyweight +96.6
kgs.
3
Uzito utapimwa siku moja kabla ya siku ya pambano.
4
Inapobidi mabondia watapima uzito siku ya pambano ambapo
wanaruhusiwa kuzidi ratili 5 ( 2.3 kgs) juu ya kiwango cha daraja la uzito
watakalopigania.
5
Ili liwe pambano la
ubingwa ni lazima mmoja wa wapinzani awe na uzito wa daraja lililoidhinishwa. Ubingwa
utapewa tu kwa bondia yule aliyefikisha uzito huo iwapo atashinda pambano hilo.
6
Gloves za wakia nane (8 oz) zitatumika kwa mapambano ya
mabondia wenye uzito usiozidi na mpaka kgm 67 Na gloves za wakia kumi (10 oz)
kwa mabondia wenye kuzidi uzito wa kgs 67.
Afya:
7
Ni lazima bondia apimwe afya siku ya pambano kabla hajaingia
ulingoni kushindana.
Vifaa vya Usalama:
8
Wakati wa pambano, ni lazima bondia avae kinga za mbeleni (
Protector cap) kabla ya kuvaa kaptura ya michezo.
9
Wakati wa pambano, ni lazima bondia avae kinga ya meno
(Gumshield).
10
Kabla ya kuvaa gloves ni lazima bondia avae bandeji.
11
Viatu visivyo na visigino.
12
Ni lazima avae kaptura ya michezo isiyozidi mwisho wa
magoti
Urefu wa Raundi ya Pambano:
13
Kila raundi ya pambano la ngumi za wanaume litakuwa ni
dakika tatu (3) za kupigana zikiwa na mapumziko ya dakika moja (1) kati ya
raundi na raundi.
14
Kila raundi ya pambano la ngumi za wanawake litakuwa ni
dakika mbili (2) za kupigana zikiwa na mapumziko ya dakika moja (1) kati ya
raundi na raundi.
15
Hakuna pambano lolote lile litakalopiganwa chini ya raundi
nne (4) na kutambuliwa kama shindano.
16
Hakuna pambano lolote lile litakalopiganwa zaidi ya raundi
kumi na mbili (12)
17
Pambano la ubingwa wa Tanzania litakuwa ni la raundi kumi
(10) tu.
18
Hakuna pambano ambalo la ushindani ambalo litapiganwa kwa
raundi zisizoganyika kwa mbili (2). Yaani kutakuwa na mapambano ya raundi nne
(4), raundi sita (6), raundi nane (8), raundi kumi (10) na raundi kumi na mbili
(12).
Muundo na jumla ya waamuzi wa pambano:
19
Mapambano yanaweza kuamuliwa na refa bila msaada ya waamuzi
wengine.
20
Mapambano mengine ni lazima yawe na watu watatu (3)
wanaotoa pointi.
21
Refa anaweza kutoa pointi akisaidiwa na waamuzi wawili (2)
AU refa asitoe pointi bali awe na waamuzi watatu (3) wa kutoa pointi.
Wasifu wa refa
anayechezesha pambano:
22
Jukumu kuu la refa ni kulinda usalama wa mabondia na
kutunza heshima ya mchezo wa boxing kwa kuhakikisha kuwa sheria zinafuatwa.
23
Ni refa pekee ndiye mamlaka ya mwisho juu ya mwenendo wa
pambano ndani ulingo. Aidha ni refa tu ndiye aliye na mamlaka ya kusimamisha
pambano.
24
Ni refa pekee ndiye mwenye mamlaka ya kuamua iwapo tukio ni
bahati mbaya au ni kusudio.
25
Ni wajibu wa refa kusimamisha pambano iwapo bondia ataumia
kiasi cha kuharibu maana nzima ya boxing kama
mchezo. Hata hivyo ni vizuri refa atafute maoni ya daktari wa pambano.
26
Kuvuja damu kutokana na kuchanika juu ya jicho ni moja ya
sababu ambazo zinamruhusu refa kusimamisha pambano.
27
Refa ataheshimu na hatakiwi kuupinga uamuzi wa marefa
wengine wa pambano (judges) au kamisaa wa pambano inapotokea utata.
28
Ni wajibu wa refa kuhakikisha kuwa hakuna bondia anaanza
raundi ya kupigana bila kuwa na gumshield.
29
Ni wajibu wa refa kumhesabia mpinzani aliyeangushwa chini
na kipigo halali.
Kusimamisha
pambano kwa ajili ya usalama wa mpiganaji:
30
Bondia anapohisi amezidiwa na kipigo cha mpinzani anaweza
kusimamisha pambano kwa kuinua mikono juu au kwa kumuarifu refa.
31
Msaidizi wa bondia anaweza kusimamisha pambano kumwokoa
bondia wake asiendelee kupata kipigo kwa kutupia taulo ndani ya ulingo.
32
Ni wajibu wa refa kusimamisha pambano ili kumwokoa bondia
asiumie kwa kuendelea kupata kipigo baada ya kuzidiwa na mpinzani.
Mtindo wa kutoa
pointi za boxing :
33
Kila mshindi wa raundi atapata pointi kumi (10 points
system) na atakayeshindwa atapata pungufu ya pointi lakini siyo chini ya pointi
7 kwa raundi.
34
Kufanyika kwa faulo kunaweza kufanya bondia apewe onyo na
refa au kutolewa pointi au kushindwa kwa disqualification.
35
Kila mwamuzi (judge) anayo ruhusa ya kumpunguza pointi kwa
mpiganaji anayefanya faulo bila kungojea onyo la refa.
Faulo za msingi
katika boxing:
36
Hairuhusiwi kupiga mgongoni wala kisogoni.
37
Hairuhusiwi kupiga
sehemu ya kinena.
38
Hairuhisiwi kupiga
kwa kutumia kichwa.
39
Hairuhusiwi kumpiga
mpinzani aliyeanguka chini. Mpinzani atahesabiwa kuwa ameanguka chini iwapo
sehemu yoyote ile zaidi ya nyayo itagusa turubai la ulingo.
40
Hairuhusiwi kupiga
ngumi za kelebu wala makofi.
41
Hairuhusiwi kupiga
baada ya kengele ya kuashiria kuisha kwa raundi.
42
Hairuhusiwi kutumia lugha ya matusi.
43
Hairuhusiwi kujiangusha bila ya kupigwa.
44
Hairuhusiwi kutia kabali wakati wa kipiga au kupigwa.
45
Hairuhusiwi kupiga iwapo refa atasema STOP.
46
Kukimbia kwa woga ulingoni kukwepa mpambano.
Kushindwa kwa
Disqualification:
47
Bondia akimuumiza mpinzani kwa faulo kiasi refa kulazimika
kusimamisha pambano, basi bondia huyo atashindwa pambano kwa disqualification.
48
Kitendo cha kupigwa kwenye kinena si sababu ya msingi ya
kupata ushindi kutokana na disqualification.
49
Uamuzi wa kutoa ushindi kwa disqualification uko mikononi mwa refa tu.
Knockdown,
knockout (KO) na Technical knockout (TKO):
50
Bondia atafahamika kuwa ameangushwa chini iwapo atagusa
canvas ya ulingo kwa sehemu nyingine yoyote ya mwili wake zaidi ya nyayo au
amesimama wima kwa kuwa tu amegemea au ameushika ulingo.
51
Bondia
atakayeangushwa chini kutokana na kupigwa pigo halali atafahamika kuwa amepigwa
knockdown na atahesabiwa nukta nane ( 8 mandatory count) na atakatwa pointi
moja (1) au mbili (2).
52
Bondia atakayeangushwa nje ya ulingo kutokana na kupigwa
pigo halali atafahamika kuwa amepigwa knockdown na atahesabiwa nukta ishirini (
20 mandatory count) na atalazimika kurudi ulingoni bila msaada wa mtu yeyote atakatwa
pointi moja (1) au mbili (2).
53
Bondia atakayeonyesha kupoteza fahamu baada ya kupigwa pigo
halali atahesabiwa nukta nane ( 8 standing count) na atakatwa pointi moja (1).
54
Bondia akishindwa kuamka kuendelea baada ya kuhesabiwa
hesabu yoyote ya lazima (mandatory count) baada ya kuangushwa chini (
knockdown) basi atakuwa ameshindwa pambano kwa Knock Out.
55
Bondia akijiuzulu au msaidizi wake akitupia taulo ulingoni
au msaidizi wa bondia akimwomba refa asimamishe pambano ili bondia wake asipate
kipigo zaidi, bondia atakuwa ameshindwa kwa TKO.
56
Refa akisimamisha pambano kumwokoa bondia basi bondia huyo
takuwa
ameshindwa kwa TKO.
57
Kuangushwa chini (knockdown) mara tatu (3) katika raundi
kutokana na kipigo kichwani ni kushindwa wa Knock Out moja kwa moja.
58
Hata hivyo refa anaruhusa ya kumhesabia bondia kutokana na
pigo lolote lile halali litakalomfanya bondia apoteze fahamu.
Pambano
litakalosimishwa kutokana na pigo batili (Kichwa).
59
Pambano lolote litakalosimamishwa kutokana na mpinzani
mmoja kuumia juu ya jicho kwa kupigwa kichwa kwa bahati mbaya, basi mshindi ni
yule aliyekuwa akiongoza kwa pointi iwapo pambano lilikuwa limevuka raundi tatu
(3).
Kama pambano
litakuwa halijavuka raundi tatu (3) basi litahesabiwa ni sare ya kiufundi
(Technical Draw).
60
Pambano lolote litakalosimamishwa raundi yoyote ile
kutokana na mpinzani mmoja kuumia juu ya jicho kwa kupigwa kichwa kwa kusudio,
basi mshindi ni bondia aliyepigwa kichwa.
61
Ni refa pekee ndiye mwenye uamuzi kuhusu pigo la kichwa
kuitwa ni bahati mbaya au kusudio.
Pigo chini ya
mkanda (Kinena).
62
Pigo la kusudio kwenye kinena litamfanya mpigaji apototeze
pointi moja (1) iwapo pigo la namna hii ni rudio.
63
Pigo la kusudio kwenye kinena halimpi ushindi wa
disqualification mtu aliyepigwa bali refa ana mamlaka ya kutoa pumziko
lisilozidi dakika tano (5) kwa mtu aliyepigwa ili aweze kupata ahueni. Akikataa
kuendelea basi atashindwa kwa TKO.
Pambano litakalosimishwa
kutokana na sababu nyingine.
64
Pambano likisimamishwa kutokana na giza
ndani ya ulingo au fujo ya watazamaji au sababu nyingine ambazo ziko nje ya
uwezo wa binadamu basi pambano hilo
halitakuwa na mshindi (No contest).
---------Mwisho-----