Adverts

Nov 1, 2011

KENYA NA SOMALIA ZIMEOMBA MSAADA WA KIMATAIFA DHIDI YA AL-SHABAAB

Waziri Mkuu wa Somalia Abdiweli Mohamed Ali (kushoto) na Waziri Mkuu wa Kenya Raila Amollo Odinga wakionesha haki za makubaliano ya kupambana na al-Shabaab jijini Nairobi Oktoba 31,2011.Picha na Reuters
Somalia na Kenya zitafanya mazungumzo na wanadiplomasia leo mjini Nairobi kujaribu kuhamasisha uungaji mkono kimataifa kwa operesheni inayoendelea hivi sasa dhidi ya kundi la Kiislamu la al-Shabaab. Katika taarifa ya pamoja, waziri mkuu wa Kenya, Raila Odinga na mwenzake kutoka Somalia, Abdiweli Mohammed Ali, wameomba msaada wa kimataifa jana kusaidia ulinzi katika pwani ya Somalia na bandari ya Kismayu, ambayo wanaamini ni nguzo ya kiuchumi ya kundi hilo la al-Shabaab.
Ali amesema kuwa serikali ya mpito ya Somalia inaiunga mkono Kenya , ambayo imetuma vikosi vyake vya jeshi ndani ya mipaka ya Somalia mwezi uliopita kupambana na wapiganaji wa al-Shabaab, ambao wanalalamikiwa kuwa wanahusika na wimbi la utekaji nyara na mauaji.