MEZA KUU WAKIFUATILIA HOJA ZA MADIWANI KWENYE MAKABLASHA
NDIVYO MKAO WA MADIWANI WAKATI WA KUJADILI BAJETI ZA WILAYA HIZO MBILI ILIVYOKUWA
MWEKA HAZINA MBOZI BWANA MBEGU MOJA AKIELEKEA UKUMBINI BILA MKOBA WA BAJETI KABLA YA KUWASILISHA BAJETI YA WILAYA ZOTE MBILI ZA MOMBA NA MBOZI
Na Danny Tweve
Hatimaye zimesalimia saa chache wenye kuangua kilio, na wenye kuchelekea kufahamika wakati orodha ya watumishi watakaoliacha boma la awali na kuhamia katika wilaya ya Mpya ya Momba kutangazwa hapo kesho jumapili imefahamika.
Kwa kipindi kirefu kumekuwepo mvutano wa ugawaji mali na raslimali zingine kwaajili ya halmashauri za Momba na Mbozi ambapo wakati fulani hali ya kuelekea kutishiana ilianza kujitokeza
baada ya mvutano huo kipyenga cha mwisho kinatarajiwa kujulikana kesho ambapo akifunga mkutano wa baraza la madiwani waliokutana kupitisha bajeti za wilaya ya Mbozi na Momba leo, Mwenyekiti wa halmashauri mama ya Mbozi aliwataka wajumbe kwenda kusali na kuombea mkutano wa baraza la madiwani wa kesho jumapili ambao utagawa mali na raslimali watu.
Wakati pia kwa upande wa watumishi orodha ya awali ya waliopangwa huko inadaiwa kukataliwa, zoezi la kupitia jina hadi jina kwa kutumia orodha ya watumishi kwa kila idara ilifanyika kwa siku kadhaa wiki hii na hatimaye watumishi wanaoitwa majembe waliorodheshwa na kutakiwa wapelekwe kwenye wilaya changa ili kuleta changamoto za maendeleo
Ingawa wapo waliotaka kuhamia wilaya ya MOMBA kwa hiari yao, uteuzi huo haujazingatia hiari ya watu hatua ambayo inaleta hofu kama kweli wote waliochaguliwa kuelekea huko wataitikia kwa moyo mkunjufu safari hiyo
Miongoni mwa maeneo yanayodaiwa kuleta mvutano ni pamoja na mgawanyo wa mali kama magari ambapo kumekuwa na kutupiana lawama baina ya madiwani wa eneo la Momba na wale wa eneo la Mbozi
Habari zaidi zinadokeza kuwa mvutano mwingine kwa wilaya ya Momba umeanza kujitokeza mahala pa kuweka makao makuu ya halmashauri ya wilaya na kituo kikuu cha polisi, huku ikipendekezwa eneo la Utambalila wakati makao makuu ya wilaya yalishatamkwa kuwa CHITETE
Mvutano huo unaleta dhana aliyowahi kuipinga mwalimu Nyerere ya uzanzibara na uzanzibari ambapo sasa maeneo ya ukanda wa juu ya wilaya ya Momba wanataka makao makuu yasogee upande wao ili kurahisisha ufikiwaji wa huduma kwa wananchi wakati ambapo pia kwa upande wa ukanda wa chini unavutia makao makuu kuwa maeneo mawili wengine wakitaka yawe kwenye msitu wa Utambalila na wengine Chitete kutokna na umbali wa eneo la Kamsamba
Yote bin yote ni kesho majira ya saa tano kama mungu ataongoza zoezi hilo limalizike kwa amani, kamera yetu itakuwa eneo la tukio kufuatilia ugawaji huo kutokana na jioni ya leo kuwepo fununu za baadhi ya madiwani kutaka kugomea zoezi hilo kwa madai kuwa baadhi ya mali zilizoitishwa hazijaletwa mbele ya kamati ya ugawaji
stay tuned