Rais aliwaapisha pia Makatibu tawala wa mkoa wa Mwanza Bi.Doroth Mwanyika na katibu Tawala wa Mkoa wa Mtwara Bwana Yusuf Athumani Matumbo.
Bi Mwanyika anakumbukwa vyema na wananchi wa wilaya ya Mbozi kwa jinsi alivyoweza kusimamia mradi wa TANZA KESHO-ama CAPACITY 21 uliokuwa ukitekelezwa na halmashauri ya wilaya ya Mbozi kwa ushirikiano na UNDP.
Utendaji wake unatajwa kuwa ndiyo mafanikio yaliyomwezesha kufanya kazi maeneo mbalimbali, ofisi ya katibu tawala mkoa wa mbeya, UNICEF na sasa huko kwenye ukatibu TAWALA.
Picha kwa hisani ya Blog ya Mawasiliano Ikulu.
May 3, 2009
HONGERA DOROTH MWANYIKA, MBOZI WANAKUKUMBUKA KWA KUSIMAMIA VYEMA TANZA KESHO
Rais aliwaapisha pia Makatibu tawala wa mkoa wa Mwanza Bi.Doroth Mwanyika na katibu Tawala wa Mkoa wa Mtwara Bwana Yusuf Athumani Matumbo.
Bi Mwanyika anakumbukwa vyema na wananchi wa wilaya ya Mbozi kwa jinsi alivyoweza kusimamia mradi wa TANZA KESHO-ama CAPACITY 21 uliokuwa ukitekelezwa na halmashauri ya wilaya ya Mbozi kwa ushirikiano na UNDP.
Utendaji wake unatajwa kuwa ndiyo mafanikio yaliyomwezesha kufanya kazi maeneo mbalimbali, ofisi ya katibu tawala mkoa wa mbeya, UNICEF na sasa huko kwenye ukatibu TAWALA.
Picha kwa hisani ya Blog ya Mawasiliano Ikulu.
MBEYA PRESS YAPATA VIONGOZI WAPYA
Mwandishi wa TBC bwana NICO MWAIBALE jana aliibuka kwa ushindi wa kimbunga kuwa mwenyekiti wa chama cha wandishi wa habari mkoa wa mbeya.
Katika uchaguzi huo ambao haukupata uwakilishi kutoka Umoja wa Vyama vya wandishi wa habari mikoani UTPC, ulifanyika kwa amani katika ukumbi wa chuo cha wafanyakazi Mbeya.
Mwaibale ambaye katika nafasi ya uenyekiti alikuwa akishindana na mwenyekiti aliyemaliza muda wake bwana Christopher Nyenyembe, aliibuka na kura 26 dhidi ya 10 za Nyenyembe.
Makamu mwenyekiti alichaguliwa Jane Lawa ambaye hata hivyo hakuhudhulia kwenye uchaguzi huo kwa kulamba kura 20 dhidi ya 15 za Richard Kilumbo.
Katibu mkuu alichaguliwa Patrick Kossima (27) na kumshinda Kenneth Mwazembe (9), Katibu msaidizi alichaguliwa Merali Chawe kwa kura 31 za Ndiyo kati ya 36 zilizopigwa.(chawe hakuwa na mpinzani).
Mweka hazina alichaguliwa Pendo Fundisha aliyepata kura 31 za Ndiyo na kura 3 za hapana baada ya kukosa mshinani, wajumbe wa kamati kuu walichaguliwa Danny Tweve aliyepita bila kupingwa baada ya kuwania nafasi hiyo peke yake.
Wajumbe wengine katika kamati hiyo waliochaguliwa kwa kushindanishwa ni pamoja na Ester Macha, Sada Matiku.
Kamati zingine waliochaguliwa ni Charles Mwakipesile(Nidhamu), Festo Sikagonamo (Mafunzo na Ujenzi) na Emanuel Simfukwe (Uchumi).
Kwa uchaguzi huo Chama cha wandishi wa habari mkoa wa Mbeya kimetimiza masharti na maelekezo mapya ya UTPC kwa kila klabu kuwa na uwakilishi sawa kijinsia katika nafasi zote za maamuzi.
Tunamshukuru bwana Christopher Nyenyembe kwa Uongozi wake kwa kipindi cha miaka 3 iliyopita ambapo ameiwezesha klabu kupata heshima ndani ya nchi kutokana na wanachama wake watatu akiwemo yeye mwenyewe kutwaa tuzo za uandishi bora wa habari za uchunguzi kwa miaka miwili.MBEYA PRESS CLUB >>> PEOPLE’S VOICE
WANDISHI MBEYA WASIKITISHWA NA VIFO VYA WENZAO
Mkutano mkuu wa Chama cha wandishi wa habari mkoani Mbeya, umepokea kwa masikitiko taarifa ya vifo vya wanachama wake 6 katika kipindi cha miaka 3 iliyopita.
Kifo cha hivi karibuni ni cha Mhariri Mkuu wa Radio Uhuru Deogratius Kiduduye aliyefariki Lagos Nchini Nigeria alikoenda kwaajili ya maombi katika Kanisa la Synagogue church of All Nation linaloongozwa na Nabii Tb Joshua.
Deo alikuwa mwanachama wa chama hicho hadi alipohamia jijini Dar es salaam kuchukua majukumu ya uhariri katika kituo cha Radio Uhuru, ambapo katika kipindi chote cha uhai wake amekuwa akitoa ushauri namna ya kuiendeleza klabu hiyo.
Wanachama wengine waliofariki dunia ni pamoja na Niko Mwakatumbula, John Lubungo, Silvester Kikungwe, Rose Nkuba, Albano Wikedzi, Erasto Palick na Mariam Ngole ambao kwa pamoja wamefariki katika vipindi tofauti vya miaka mitatu ya uongozi uliomaliza muda wake hapo jana.
Wanachama waliozungumza na blog hii wamesema katika jumuiya ya wanachama 60 kupotelewa na wanachama wake 8 ni jambo la kusikitisha na kumwomba mungu awatunze na kuwafikisha mahala salama marehemu wote hao. AMEN
Apr 30, 2009
MCHUNGAJI ALIYEJIFANYA KUIBANIA MAHAKAMA, YAMKUTA HATIMAYE AREJEA KUAPA
Hatimaye Mchungaji Simon Kitwike wa Kanisa la EAGT Ichenjezya wilayani Mbozi mkoa wa Mbeya, aliyekataa kuapa mahakamani na kupelekea kufungwa kifungo cha miezi sita jela, amekubali kuapa na hivyo kuruhusiwa kuendelea kutoa ushahidi wake.Marchi 23,mwaka huu kesi yake ilipotajwa kwa mara ya pili
Mchungaji huyo ambaye anatumikia kifungo chake akiwa nje ya Gereza, alifika mahakamani hapo alipoulizwa kama atakuwa tayari kuapa alikubali kufanya hivyo kasha alipewa Biblia na kuapa kwa mujibu wa sheria.Kesi hiyo inawakabili washitakiwa watatu akiwemo mwanamke mmoja ambao ni Telezia Mtega, Hekima Simkoko na Emmanuel Lwinga ambao walikutwa na baadhi ya vifaa vya wizi ambavyo vinasadikiwa kuwa mali ya mchungaji Simon Kitwike.Hata hivyo baadqa ya kutoa ushahidi wake kesi iliahirishwa hadi Marchi 31 itakapotajwa tena, na kuwa washitakiwa wawili wako nje kwa dhamana, ambapo mshitakiwa mmoja anashikiliwa kutokana na kuwa na kesi nyingine inayomkabili.Februari 4, mwaka huu mchungaji huyo alifika katika mahakama ya wilaya ya Mbozi ili kutoa ushahidi kwa watuhumiwa watatu waliokamatwa na baadhi ya bidhaa zilizoibiwa nyumbani kwake Oktoba 25 mwaka jana, lakini kutokana na imani ya dini yake alikataa kuapa mahakamani kwa mujibu wa kifungu katika Biblia cha Injili ya Mathayo 5:33 – 37 ambacho kinaeleza kuwa “Tena mmesikia watu wa kale walivyoambiwa usiapa uongo ila mtimizie Bwana nyapo zako lakini mimi nawaambia msiape kabisa hata kwa Mbingu kwa maana ndicho kiti cha enzi cha Mungu”.Baada ya kukataa na kusoma kifungu hicho Hakimu Nyasige Kajanja aliahirisha kesi hiyo kwa muda ili akajiridhishe na sheria, hata hivyo alipporejea tena mahakamani hakimu huyo alimsomea sheria kuwa asiyeapa anatenda kosa la kuidharau mahakama ambalo adhabu yake ni kifungo cha miezi 12 jela kwa kutumia kifungu cha sheria namba 198(1) kama ilivyorekebishwa mwaka 2002.Hata hivyo Hakimu Kajanja alimtaka Mchungaji huyo kusoma kitaBU CHA Warumi 12;1-2 kinachoeleza kuwa;” Kila mtu na aitii Mamlaka iliyo kuu kwa maana hakuna mamlaka iliyopo imeamriwa na Mungu, hivyo amwasiye mwenye Mamlaka hushindana na agizo la Mungu nao washindanao hujipatia hukumu”Mchungaji huyo alifungwa jela miezi sita kufuatia kukataa kuapa mahakamani ambako alitakiwa kuapa kabla ya kuanza kutoa ushahidi wake juu ya kuvunjiwa nyumba yake na kuibiwa mali zenye thamani ya shilingi milioni 2.2.Akizungumzia mkasa uliompata alisema kuwa Oktoba 25 mwaka jana majira ya saa sita za usiku kundi la majambazi lilifika nyumbani kwake na kumuamuru kutoa fedha la sivyo wangemuua.Mchungaji huyo alitaja mali alizoibiwa kuwa ni pamoja na fedha taslimu shs. 1.212 milioni, godoro moja, seti moja ya luninga, radio mbili masanduku mawili ya safari (Brief case) na simu za mkononi mbili na rewinder moja, hata hivyo majambazi hayo hayakuwadhuru
CHELE BOVU LAMWAGWA!!!!! KWELI NDOMONDO ANATISHA
Jumla ya tani 11 za mchele uliokuwa ukisafirishwa kutoka nchi ya Vietnam kuingia nchini na kukamatwa na Mamlaka ya Mapato nchini, katika mpaka wa Tanzania na Zambia katika mji wa Tunduma wilayani mbozi mkoa wa Mbeya ukivushwa kutokea jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo baada yan kukataliwa nchini humo, umeteketezwa jana
Kwa mujibu wa Meneja Msaidizi wa mamlaka hiyo mkoani Mbeya Rogasian Shirima ameeleza kuwa mchele huo ulivushwa katika mpaka wa Tunduma ukipelekwa nchini Kongo Februari 9 mwaka huu ukiwa jumla ya tani 16 ambapo mamlaka ya chakula na afya nchini Kongo iliukataa mchele huo kwa sababu za kiafya na ikaamuru urudishwe Vietnam .Alisema kuwa nchini Kongo walipokea tani 6 tu ambazo zilizokidhi kiwango kwa afya ya binadamu na mwingine kukataliwa ambapo imeelezwa katika nyaraka za usafirishaji wa mchele huo hazikuwa na maelezo ya mzalishaji, mwaka uliozalishwa na tarehe ya mwisho ya kutumika.Naye Afisa Mkaguzi wa Mamlaka ya uthibiti wa chakula na madawa nchini (TFDA) Kalekayo Emmanuel amethibitisha mchele huo kuwa haufai na hivyo kuamuri kuteketezwa ili kuwanusuru wananchi ambao wangeweza kuuziwa chakula hicho.Shehena hiyo ya mchele ilikuwa ikisafirishwa na gari lenye usajili namba T193 AAL na tela T353 AKV aina ya Scania likiendeshwa na dereva Bakari Athuman (51) ambaye ameeleza kuwa alipakia mzigo huo katika bandari ya Dar es Salaam Februari 6 na kuvuka mpaka Tunduma na Nakonde Februari 9 na kwamba amelazimika kukaa Kongo kwa muda wa mwezi mzima baada ya kukataliwa kupakuliwa mzigo huo.Mmiliki wa lori hilo Komuni Sirai amesema kuwa yeye alikodisha gari lake kwa Gabriel Luxo raia wa Kongo ambaye aliingiza mchele huo kutoka Vietnam na kwamba kitendo cha mchele huo kukataliwa kumemfanya apate hasara zaidi ya dola za kimarekani 7000 baada ya mteja wake kutoroka bila kumlipa.Hata hivyo ameshukuru kwa mamlaka hizo kwa kutoa uamuzi ambao umempa nafasi ya kuondoa mchele na kwamba gari lake litaweza kufanya kazi zingine.Baadhi ya watu ambao walishuhudia tukio la uteketezaji wa mchele huo walisema kuwa, kusafirishwa kwa mchele huo kupitia mipaka ya nchi yetu inaonesha kuwa idara zinazohusika na udhibiti wa uingiaji wa bidhaa kutoka nje bado hazijawa makini, hali ambayo imepelekea mzigo huo kufika hadi Kongo na kasha kurejeshwa tena jambo ambalo wamesema linaonesha udhaifu mkubwa.
MTUMISHI WA MUNGU MWAKASEGE KUFANYA MKUTANO BIRGHAM
NI MTUMISHI ALIYE JUU KATIKA HUDUMA ZA KIROHO, ANAHESHIMIKA, NI VIFAA MUHIMU KATIKA MASUALA YA KUMWOKOA BINADAMU KIROHO NA KIMWILI: MHUBIRI MSOMI ELIMU YA UCHUMI NA BIBLIA
DARAJA LA MNING'INIZO
Hii picha nimedowea kwa mdau wangu maisha ni vita.blogspot.com.
Hili ni ja ya madaraja yaliyojengwa na Mfuko wa maendeleo ya jamii TASAF wilayani Mbozi, ila daraja kama hili ukiwa chicha unaweza kujiachia, manake linanesa eeeee, hadi unamwaga pombe zote kichwani.
Hongera Tasaf Mbozi kwa kuwasogezea wananchi huduma manake walikuwa wanaogolea kwenye mto kwenda upande wa pili, sasa wanafunzi inakuwaje pale wanahitaji kwenda shuleni?
ALBINO ANAPOKARIPIWA NA POLISI
MANAMBAZI WATOROKA KWA HELKOPTA BAHARI YA HINDI
The two crew members of the hijacked helicopter were unhurt A convicted sex offender and cult leader has escaped by helicopter from a prison on the French Indian Ocean island of Reunion, officials say. Juliano Verbard, 27, serving a 15-year term, and two followers, were pulled on to the helicopter by three accomplices. The accomplices had pretended to be tourists when boarding the helicopter, but then forced the pilot to land in the prison grounds before flying off. They then landed a few hundred metres away, and drove off in a waiting van. The island's police force said a major search was now under way for Verbard and his fellow prisoners, Alexin Jismy and Fabrice Michel. Verbard, the leader of the pseudo-religious cult, the Sorrowful and Immaculate Heart of Mary, was jailed in 2008 for rape and sex attacks on children, and the other two for their roles in a kidnap. At the time of his trial, psychiatrist Gerard Toulfayan described Verbard as an "extremely powerful manipulator with great intelligence". The two helicopter crew members were unhurt.
AFRICAN JOURNALISTS FELLOWSHIP
UC Berkeley Fellowships for African Journalistshttp://www.journalism.berkeley.edu/press/african_journalists/The Graduate School of Journalism at the University of California at Berkeley is pleased to invite applications for two yearlong fellowships for accomplished African journalists, beginning in August 2009.The fellowships will each total $36,000, including roundtrip airfare, professional stipends, and rent while in Berkeley . The initiative will also offer dedicated funding for both domestic U.S. and Africa travel for research and reporting work.The selected fellows will join the School’s Visiting International Scholars Program and participate in a new journalism training initiative aimed at producing high quality coverage of agricultural development issues in Africa for dissemination in U.S., African, and international media.Requirements:Selected fellows must bring at least five years experience in journalism in sub-Saharan Africa , in any medium including print newspaper, magazine, television, radio, documentary, or new media format such as blogging, podcasting, and other online publishing.Applicants also must demonstrate a proven track record of commitment to the truth-seeking craft, and a willingness to effectively investigate problems of food access and production on the continent.A B.A. degree, at minimum, is strongly desired, along with experience and knowledge about agricultural issues in African countries.Selected African fellows will enroll with other Visiting Scholars in background courses at Berkeley examining the global food crisis starting in late August 2009, while also contributing their knowledge about Africa and journalism to their U.S. and international peers.Applications must include a CV, three examples of work, and a one- page cover letter containing a statement of interest. Please send applications to the following email address, c/o dean’s assistant Julie Hirano: africa@journalism.berkeley.eduDeadline for applications: May 1, 2009This opportunity is part of a new two-year grant provided by the Bill & Melinda Gates Foundation to the Graduate School of Journalism at the University of California at Berkeley .
