Adverts

Oct 23, 2013

MAISHA NDIVYO YALIVYO, HATUJUI YA KESHO

Kula ni sehemu ya utaratibu wa mzunguko wa maisha ya Binadamu, tendo kama hili kila siku hufanyika lakini mara ngapi tumbo limeshukuru kwa kulishwa na hatmaye likaahidi halitapokea tena kwa kipindi cha siku kadhaa, miezi kadhaa?

KAMATI YA BUNGE YAOMBA IKAJIFUNZE KUTENGENEZA MVUA MALAYSIA

Na Danny Tweve Mbozi

Mjumbe wa kamati ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji na Mbunge wa jimbo la Mwanakwerekwe Mh Haji Jumaa Sereweji amesema kuna haja kwa wizara ya Kilimo kuipeleka kamati hiyo kwenda kujifunza namna mvua  za kutengenezwa zinavyoweza kuleta ufanisi

Mbunge huyo akichangia hoja iliyoanzishwa na Mbunge wa Rungwe magharibi Profesa David Mwakyusa kuwa serikali ianze kubadilisha mfumo wa kusaidia maeneo yenye njaa kwa kupeleka chakula na badala yake fedha zinazotengwa kwaajili ya kununua chakula cha akiba zielekezwe kujenga miundombinu ya umwagiliaji kwa maeneo yenye ukame.
Mwenyekiti wa Mtaa wa Mwenge wilayani Mbozi bwana Mwaipwisi akitoa malalamiko juu ya uharibifu wa barabara unaofanywa na magari yanayopeleka shehena ya mahindi kwenye maghala hayo pasipo kutozwa fedha za matengenezo ya barabara hizo na kuliacha jukumu hilo kwa mamlaka ya mji wa Vwawa

Mtendaji Mkuu wa wakala wa taifa wa hifadhi ya chakula Bw. Charles Walwa akizungumza na wakulima na mawakala waliouza mahindi yao kwenye kituo cha Vwawa wilayani Mbozi

Miongoni mwa zana za kuchambua uchafu wa mahindi yanayofikishwa kituoni hapo na wakulima kwa njia za udanganyifu kwa kuweka takataka kwenye magunia yao 

shenena ya mahindi ambayo inasubiri kusafirishwa kwenda Makambako na jijini Dar es salaam kutokana na maghala kutotoshereza wingi za mahindi yaliyopo

 Mtendaji wa NFRA BW. CHARLES WALWA akijibu hoja za kamati ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji liyofanya ziara kwenye maghala ya Vwawa wilayani Mbozi ambako shehena kubwa imeanza kusafirishwa kupelekwa jijiji
 sehemu ya shehena ya mahindi yaliyopo kwenye ghala la Vwawa


 Wabunge wakihoji ubora wa magunia yanayotumika katika uhifadhi wa nafaka kwenye ghala la NFRA Vwawa Mbozi
 Mbunge wa Sikonge Mh Said Nkumba akizungumza na wafanyabiashara, mawakala na wakulima waliouza mahindi yao kwa wakala wa hifadhi ya chakula ya Taifa NFRA katka kituo cha Vwawa ambapo wanalalamikia kucheleweshewa malipo yao
Ujumbe wa kamati ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji wakifuatilia taarifa iliyokuwa ikiwasilishwa na mtendaji mkuu wa wakala  NFRA

Mh Sereweji alisema yeye kwa mtazamo wake Tanzania ya sasa haipaswi kuendelea kusubiria umwagiliaji wa kutegemea mvua za mwenyezi mungu ambazo zinaathiriwa na mabadiliko ya tabia nchi, na kwamba ubunifu na matumizi ya teknolojia za umwagiliaji zaidi zikiwemo mvua za kutengeneza
Ningeshauri kamati hii ipelekwe kuleee wapi kule malasia ili ikajifunze na kuona ufanisi wa mvua hizo ili teknolojia hiyo iletwe nchini na kutumika kwaajili ya kuongeza uhakika wa chakula hasa kwa maeneo yenye ukame.
Akizungumza kwenye ziara yao ya kushtukiza walioifanya kwenye ghala la kusafirishia nafaka la Wakala wa hifadhi ya Taifa ya Chakula NFRA  lililopo eneo la Vwawa wilayani Mbozi , Mbunge wa Rungwe Magharibi Profesa David Mwakyusa alisema kuna baadhi ya maeneo nchini yamejipa hati miliki ya misaada ya chakula kila msimu licha ya maeneo hayo kuwa na fulsa zingine za uzalishaji.
Profesa Mwakyusa alisema kuna umuhimu kwa maeneo hayo kuhamasishwa kuanzishwa mifumo ya umwagiliaji ambayo itawezesha  kufanya umwagiliaji pale mvua za zinaposimama na kwamba fedha zinazotengwa kununua nafaka zielekezwe kwenye miradi hiyo ya umwagiliaji.
Katika taarifa yake Mtendaji Mkuu wa wakala wa hifadhi ya Chakula nchini NFRA Bwana Charles Walwa alisema wakala yake imepokea kiasi cha shilingi Bilion 70 kwa mwaka wa fedha 2013/2014 kati ya Bilion 100 ilizozitarajia kwaaajili ya kulipa kwa wakulima na mawakala kutokana na ununuzi wa nafaka
Alisema wakala yake ina imani kuwa deni la bilioni 30.2 litalipwa mapema ili kuwezesha wakulima kuendelea na hatua za maandalizi ya msimu ulioanza wa kilimo na kwamba wakulima na mawakala wawe wavumilivu kwa muda mfupi huu ambao maalipo hayo yanaandaliwa hazina.
Mtendaji huyo amesema katika hatua za kuipunguzia gharama za uendeshaji, wakala hiyo inafanya mazungumzo na makampuni ya hapa nchini kuanza kutengeneza mifuko ya visalfeti kwaaajili ya kuhifadhi nafaka badala ya kutumia magunia ambayo bei zake zimekuwa zikipanda msimu hadi msimu.
Alisema wakala imekuwa ikitumia kiasi cha shilingi Bilion 5 kwa kila msimu kwaajili ya kununua magunia ya katani kwa ajili ya kuhifadhi nafaka ambayo yamekuwa yakiharibika katika kipindi kifupi tofauti na teknolojia ya visalfet ambayo inatumiwa na nchi jirani kama Zambia ambayo imeonekana inapunguza gharama zaidi ya nusu ya ile wanayotumia sasa.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa kamati ya Bunge inayosimamia Kilimo, Mifugo na Maji Mh SAID MKUMBA  ameelezea kuridhishwa na jitihada za wakala hiyo katika kujipanga kwaajili ya kujitegemea
Alisema hatua za sasa za kuanza kujenga na kupanua maghala ni hatua muhimu ya kuonyesha uwezo wake katika ukusanyaji wa mazao na kulipa kwa bei nzuri kwa wakulima.
Alisema kiwango cha shilingi 500 kwa kilo kiliweza kuvutia wakulima wengi kuuza mazao yao kwa NFRA  hivyo hatua iliyobakia ni kuendelea kujenga imani hiyo kwa wakulima kwa kuhakikisha wanalipwa kwa wakati ili waendelee kushiriki uzalishaji kwa tija.
Kamati hiyo ya Bunge ilizungumza pia na mawalaka na wakulima ambao wanaidai NFRA ambao miongoni mwao walionyesha kuchoshwa na ahadi za malipo yaliyocheleweshwa yanayofikia Bilion 30.2kwa nchi nzima huku kiasi kikubwa kikiwa ni wakulima wa mikoa ya Mbeya na Rukwa.

Mwisho   

Oct 21, 2013

UWANJA WA NDEGE WA SONGWE WAKARIBISHA WAWEKEZAJI KWENYE UJENZI WA MAGHALA

Mwendeshaji wa mtandao wa Indaba africa akiwa nje ya  uwanja wa ndege wa songwe mwishoni mwa wiki iliyopita 

Afisa uendeshaji na Masoko wa uwanja wa Ndege wa Songwe bwana Kyomo akizungumza na wandishi wa habari kuhusiana na fulsa zilizopo kufuatia ujenzi wa uwanja huo

Meneja usalama wa anga wa uwanja wa ndege wa Songwe akionyesha njia za ndege kwenye moja ya zana zake katika chumba cha kuongozea ndege kwenye uwanja wa ndege wa songwe mkoani Mbeya

SUMBAWANGA ASUBUHI YA LEO

Mtaa maarufu kuelekea bar ya Kilimanjaro ambako hapo kila jambo la mjini linapatikana 

Moto wa Sumbawanga ni Ng'ara  bila shaka wapo vizuri kwenye suala la Usafi wa mji 

Moja ya minara ya mji wa Sumbawanga 

WADAU WA ZAO LA MPUNGA WALALAMIKIA UINGIZAJI MCHELE KUTOKA NJE

Akina mama wanaouza mchele kwenye eneo la Soko la Sumbawanga wakiwaeleza maofisa kutoka Shirika la Maendeleo la Uholanzi SNV changamoto ya soko la mchele wa ndani kushindwa kupenya baada ya uamuzi wa serikali kuingiza mchele kutoka nje ambapo wanunuzi wa awali ambao ni kutoka mkoani Dar es salaam sasa hawafiki Sumbawanga kufuata mchele huo

Mama huyu aliamua kusimama na kutoa ufafanuzi namna wanavyokwamishwa na hali ya sasa ya wanunuzi kutofika mkoani Rukwa kufuata mchele huo kutokana na mchele kutoka nje kuuzwa bei ndogo ikilinganisha na ule unaozalishwa na wakulima mkoani humo

Wadau wa zao la Mpunga mkoani Rukwa wakitoa maoni yao juu ya mnyororo wa thamani  wa zao hilo na kuweka mikakati ya kujenga mtandao wa wazalishaji wa mpunga mkoani Rukwa 

miongoni mwa watoa maamuzi kwenye ngazi ya halmashauri ambao ni madiwani walishiriki katika mjadala huo ambao unalenga kuweka mikakati ya kulifanya zao la Mpunga kuwa eneo muhimu la kiuchumi linalochangia pato la wananchi wa mkoa wa Rukwa  kama yalivyo mazao mengine ya biashara ambayo yameundiwa bodi zake

Mratibu wa MVIWATA mkoa wa Rukwa  akifutilia michango ya wadau wa zao la Mpunga kwenye mkutano huo ambao ulihusisha wadau mbalimbali vikiwemo vyombo vya fedha, makampuni ya mbegu na vifaa vya kilimo mkoani Rukwa

Afisa kutoka Shirika la Maendeleo la Uholanzi SNV Bw Joel Mwakitalu akizungumzia nafasi ya wakulima katika kuchukua hatua za kujenga mtandao utakaowawezesha kuwa na mawasiliano ya pamoja baina yao,vyombo vya fedha na wasambazaji mbegu na huduma zingine ili kuongeza uzalishaji wenye tija na kulifanya zao muhimu kiuchumi kwa vijana na jamii kwa ujumla

Afisa  Kilimo wilaya ya Sumbawanga kushoto akifuatilia michango ya wadau kwenye mkutano huo

MJOMBA SIKU ALIPOPOKEWA MBEYA KWA MASHAMSHAM

Mjomba Mrisho Mpoto akipewa mikono ya karibu na wandishi wa habari mkoani Mbeya, siku alipotua uwanja wa ndege wa Songwe kwaajili ya shughuli maalimu mkoani mbeya 

MDAU KYANDO APATA JIKO

Bwana Aitwa Kyando akiwa na mkewe wakipata baraka za mwisho baada ya ibada ya Ndoa iliyofanyika katika Kanisa la KKKT Bwawani mkoani  Pwani  hivi karibuni

Bwana na Bi Harusi na wapambe wao wakiwa mbele ya Usharika kuthibitisha kuanza maisha mapya ya ndoa

Ndugu jamaa na marafiki wakifuatilia ibada ya ndoa 

AAAAAAMEEEEENIIII  NDIVYO WANAVYOITIKIA WAUMINI 

MASHUHUDA WAKIWA KANISANI KUFUATILIA IBADA YA NDOA

IBADA IKIENDELEA 

Oct 14, 2013

KLABU YA WAPINGA RUSHWA NANSWILU MBOZI YAZINDULIWA

Kikundi cha wanafunzi wanachama wa klabu ya wapinga rushwa katika shule ya sekondari ya Nanswilu kilichozinduliwa wakati wa mbio za mwenge wilayani Mbozi  ni chembe ya aladari katika kueneza kampeni za kupinga rushwa kuanzia kizazi cha watoto hadi watu wazima. Kampeni hzi zinapaswa kuenezwa nchi nzima ili ziweze kusaidia kukabiliana na changamoto za rushwa nchini

Oct 13, 2013

MAUZA UZA YA DUNIA-KIJANA AMWOA MAMA YAKE MZAZI! RUVUMA

 Katika hali inayoonyesha dunia ipo Ukingoni kijana ajulikanaye kwa jina la Joseph Mapunda mkazi wa Mbinga mkoani Ruvuma amemweka kimada mama yake mzazi na kuendelea kushiriki naye tendo la ndoa kwa kipindi cha miaka 10 imefahamika.
Huyu ndiye Joseph Mapunda aliyemwoa mama yake mzazi 
 Katika hali ya kuonyesha dunia ipo ukingoni, kijana mmoja anayefahamika kwa jina la Joseph Mapunda amefanya laana ya mwaka kwa kumuoa mama yake kwa kipindi cha miaka 10 hadi juzi alipoumbuliwa mbele ya mganga wa tiba za asili ajulikanaye kama Bibi Ndembo.
Tukio hilo ambalo kulingana na kipindi cha Kanjanja Time cha Channel Ten, limetokea mkoani Ruvuma katika wilaya ya Mbinga ambapo serikali ya kijiji inaangalia uwezekano wa kumkabidhi kijana huyo kwa mamlaka za dola ili achukuliwe hatua.
Kulingana na mahojiano na timu ya kanjanja time, kijana huyo Joseph Mapunda anasema kuwa alishaoa wake zake watatu lakini aliwaacha wote kutokana na kuwa na mapenzi zaidi na mamaye ambaye walianza kushirikiana tendo la ngono miaka kumi iliyopita.
Akizungumza pia mama Mapunda anaeleza kuwa alimweleza wazi mtoto wake huyo wa mwisho kuwa anampenda na anataka waoane jambo ambalo mwanaye huyo hakukataaa na wakaendelea kula maisha kama mke na mme.
Hata hivyo inadaiwa kuwa kulikuwa na mambo ya dunia ya tatu zaidi(ushirikina) katika masuala yao ya mahusiano na ndiyo sababu wananchi walipoona jambo hilo si la kawaida waliama kuliwasilisha kwa mganga wa tiba za asili Bi Ndembo ambaye aliwaita wote na kuwaweka hadharani
Anaeleza kuwa walinyolewa na ndipo wakaweza kutoa maelezo namna walivyojihusisha na ushirikina na pia ushirika wao wa mapenzi ulilenga kuiamrisha zaidi mtandao wao wa kiushirikina kama mama na mwana na mke na mme! Jambo ambalo lilidumu kwa miaka  kumi.
Akizungumza  baada ya kutolewa kwa mganga huyo Kijana Joseph Mapunda anaeleza  kuwa hatarudia tena kumfanya mama yake mkewe na kwamba akitaka kutii kiu yake atatafuta wa kumfurahisha na siyo mama yake tena.
Hata hivyo katika maelezo yake mama mtu anaeleza wazi kuwa hayupo tayari kukubali kuachana na bwana wake Joseph kwakuwa bado anampenda! Huku akizungumza lafudhi ya kingoni mama huyo anasisitiza kuwa anampenda mno Joseph kama bwana wake.
Naye Joseph baada ya mahojiano ya muda mrefu anasema” nitaangalia uwezekano wa kuachana na mama  kama mke wangu, ila najua ni suala gumu “
Mashuhuda wa  jambo hilo  akiwemo Bi Isabela Ponera anayeleza kuwa alifika kwa mganga huyo  Julai  3 mwaka huu na baadaye kukutana na kesi ya Joseph na Mama yake  ambayo yeye binafsi hajawahi kukutana na tukio kama hilo tangu azaliwe mwaka 1960!
Wengi wa waliohojiwa kuhusiana na tukio hilo wanapendekeza Joseph afungwe miaka kadhaa ili ajifunze kuwa ni kosa kufanya ngono na mama yake mzazi, angawa kwa upande wa mama Joseph ambaye anaonekana kuwa na umri mkubwa karibu miaka 70 wanamwonea huruma kuwa akifungwa anaweza kufia jela.

Huyu ni mamayake Joseph aliyeolewa na mwanaye  kwa kipindi cha miaka 10 huku akieleza kufurahia unyumba na mwanaye!!


SHAMBA LA KAHAWA LINAUZWA

SHAMBA LA KAHAWA LENYE UKUBWA WA EKARI 20 PAMOJA NA NYUMBA VINAUZWA KWA PAMOJA WILAYANI MBOZI,  SHAMBA LIPO UMBALI WA MITA 850 KUTOKA BARABARA KUU YA TANZANIA NA ZAMBIA

BEI NI TSHS 55 MILION   
WASILIANA NASI KWA 0764 947555 ama indabaafrica@gmail.com
SHAMBA LINA NYARAKA ZOTE MUHIMU IKIWEMO HATI MILIKI ILIYOHAI