Hawa Watanzania wenzetu hawa tunashukuru baada ya kelele nyingi sasa wanajitokeza na kushiriki shughuli za maendeleo, sasa nadhani bado kuwawekea mikakati ya namna gani wasijiweke kwenye mazingira hatarishi wakati wa kutafuta riziki, nadhani baada ya hapo tuwawezeshe wawe na miradi ya kiuchumi yenye ulinzi manake nimeendelea kuwaona wengine wakiwa omba omba pale mbeya mjini unadhani huo ni ulinzi?.
Ila zile bidhaa kama mafuta na kofia zinawafikia kweli? sijui manake nakumbuka shughuli hii ilikuwa kwenye mbio za mwenge wilayani Mbozi.
Hawa ndiyo viongozi wa chama cha albino wilaya ya Mbozi ambao kwa uwezo wao naamini wanaweza kujenga hoja na kuwezesha chama kuanzisha miradi ya kiuchumi inayostahiki kulingana na risks of their security!! kama sijakosea kingereza namaanisha kwamba wawe na miradi ambayo haitawaweka kwenye mazingira hatarishi manake wakiwa wanakimbizana na bidhaa ambazo mteja anaweza kumvuta vuta mpaka uchochoroni biashara itabadilika na kuwa hatari kwao.