Radio Maarufu Mkoani Iringa ambayo tayari imeanza kupasua anga katika mikoa ya Nyanda za Juu Kusini pamoja na nchi jirani za Malawi na Zambia ya Ebon FM imezindua mpango wake wa kushirikisha wadau katika vipindi vyake wilayani.
Katika mpango wake huo tayari wandishi wake wameanza kutembelea wilaya mbalimbali za mikoa jirani na sasa timu hiyo ipo wilayani Mbozi.
Jana Asubuhi majira ya saa tatu hivi Mtangazaji Raymond Francis alitia timu na kufanya kipindi cha Live kilichokuwa kikizungumzia utekelezaji wa mpango wa serikali wa ununuzi wa mahindi ya wananchi kupitia National Strategic Grain Reserve kituo cha Vwawa.
Kama ilivyo desturi ya viongozi wetu, meneja wa kituo hicho aliyefahamika kwa jina la Rwegoshora alishindwa kutoa ushirikiano kwa wanahabari hao na kuishia kuwafukuza kwenye mazingira yake.
Hata hivyo Bw. Raymond katika kuonyesha kukomaa katika kazi yake alijivuta nje ya majengo ya ghala hilo ambako dhahiri kulionyesha malalamiko Lukiki ya wafanyabiashara kulalamikia utaratibu wa kutumia mzani mmoja wa kusogeza jiwe ama kupandanisha jiwe ili kupata uzito wa juu, kitu ambacho kimerudisha zoezi hilo kwenye hatua za awali za binadamu ama ujima.
Aidha pamoja na adha hiyo pia kuna kila dalili kuwa shehena hiyo inayozidi kuingia eneo hilo itakumbana na mvua za vuli zinazotarajiwa kuanza kunyesha kuanzia tarehe 12 ya mwezi October hali ambayo itawaingiza kwenye hasara wafanyabiashara hao.
Kwa ujumla wakazi wa wilaya ya Mbozi pamoja na mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo Levison Chilewa wameipokea redio EBON kwa herufi kubwa baada ya kueleza wazi kuwa atatoa kila ushirikiano unaohitajika kwa kuzingatia kuwa ni redio ya watu.
Ebony ambao inakita kupitia masafa ya 94.7 tayari imeshachukua umaarufu katika mji mdogo wa Tunduma ambako watu wamekuwa wakihemea juu juu kama pelege kutokana na mchaka mchaka wake katika kukamua ngoma zinazotoka sasa hivi, kuwa na vipindi vyenye mrejesho wa jamii(feedback provision) na hata mahojiano na wadau mbalimbali hali ambayo inawafanya wasikilizaji waone wamefika.
Kwa ujumla wadau wa blog wanapongeza hatua hiyo na kwamba Ebony imekuja kufunika na kasi hiyo imeanza kupokelewa na upande wa ng'ambo ya mipaka kwani Zambia tayari wameanza kutambaa kwa kujifunza kiswahili ili waweze kwenda pamoja na matangazo ya redio hiyo.
Karibu ebony tupo pamoja, Blog hii inawatakia kila zuri liwe nanyi!!!!!