Adverts

Nov 2, 2010

CHADEMA YAVUNA UBUNGE MBOZI MAGHARIBI, CCM MBOZI MASHARIKI

Na Danny Tweve Mbozi.

Matokeo ya ubunge katika majimbo mawili ya Mbozi mashariki na Magharibi yanaonyesha vyama vya CCM na CHADEMA kugawana majimbo.
Wakati chama cha Mapinduzi kikichukua jimbo la Mbozi Mashariki kupitia mgombea wake Godfrey Zambi, Chama cha Demokrasia na Maendeleo kimechukua jimbo la Mbozi Magharibi kupitia Mgombea wake David Silinde.

Akitangaza matokeo hayo Msimamizi wa majimbo hayo mawili Bw. Levison Chillewa ametangaza kuwa kwa jimbo la Mbozi Mashariki Godfrey Zambi wa CCM amepata kura49,095, wakati Allamis Mwampamba (CHADEMA) kura 31,997 na Nkunyutila Siame kupitia CUF amepata kura 839.

Kwa upande wa jimbo la Mbozi Magharibi Msimamizi huyo alimtangaza David Silinde CHADEMA baada ya kupata kura 20835, huku mgombea wa chama cha mapinduzi Dr Luka Siame akipata kura 20,203 na kasabuni Asukile ca CUF akiwa na kura 220.

Kwa upande wa madiwani jimbo la Mbozi mashariki CCM imechukua viti 16 kati ya 18 vilivyopo huku viti viwili vikienda CHADEMA kwa miji ya Vwawa na Mlowo. Jimbo la Mbozi magharibi CCM imeshinda viti 12 vya Udiwani na ChADEMA viti viwili ( 2) vya miji ya Tunduma na Ndalambo.



MWISHO