Ilianza hapa baada ya konda wa daladala kumtukana abiria tusi la mseeeee........... aise jamaa akapandisha maruhani, unasema nini(mwenye shati jeupe) hebu nishikie hiyo nanihii yangu
Hapa siyo wanacheza shamkware pesa mbongoo ya defao, ngumi zimeanza wakaanza kuburuzana kati ya dereva na abiria baada ya Konda kuzidiwa na kutoka mbio.
Hapa mtu akajipendekeza, abiria akaonekana mtaalamu wa kuniga(ama kukaba koo) dereva akapoteza pumzi kwa dakika chache huku akipumulia mlango wa nyuma!!!!!!!!!!!!!!!
Konda akashtukia bosi wake(dereva) anaichungulia Izraeli ikabidi aingilie kati, mwananchi akaangushwa chini lakini fasta fasta akabilingika na kwenda kuchukua jiwe, kabla hajarusha wapiga debe wakawahi kumzingira na kuwaokoa konda na dere wasilambe ngeuuu! Ilikuwa mazingira yale yale ya kituo cha mabasi Vwawa cha Makaburini leo mchana